DALILI ZA MINYOO

DALILI ZA MINYOO
Wakati mwingine ni vigumu sana kujua kama una minyoo, kwani minyoo wanaweza kukaa ndani ya mwili kwa muda mrefu bila ya kuonesha dalili yeyote, ama madhara yeyote. Na dalili za minyoo pia hutofautiana sana, kulingana na aina za minyoo. Lakini zifuatazo ni katika dalili kuu:-
1.Kichefuchefu
2.Kukosa hamu ya kula
3.Maumivu ya tumbo
4.Kupungua uzito
5.Uchovu wa viungo
6.Kuona utelezi mwingi kama kamasi kwenye kinyesi
7.Kuona minyoo kwenye kinyesi.
8.Kuona damu kwenye kinyesi
9.Tumbo kujaa

Dalili hizi kama nilivyotangulia kusema kuwa zinatofautiana kulingana na aina ya minyoo. Sasa hebu tuone kwa ufupi dalili hizi kulingana na aina ya minyoo:-

1.minyoo aina na tapeworm dalili zao ni:
A.Kuvimba kwa ngozi ama kujaa ama kujaa kwa tumbo
B.Kuwa na alegi
C.Kuwa na homa
D.Matatizo katika mfumo wa fahamu, kama kifafa

2.minyoo aina ya hookworm dalili zao ni kama:-
A.Kuwashwa
B.Kupata ugonjwa wa anaemia (upungufu wa seli hai nyekundu kwenye damu) hivyo kukosa oksijeni ya kutosha mwilini
C.Kuwa na uchovu wa hali ya juu.

3.minyoo aina ya trichinosis, minyoo hawa wana dalili kama:-
A.Kupata homa
B.Kuvimba kwa uso
C.Maumivu ya misuli na kuchoka
D.Maumivu ya kichwa
E.Kutokupenda kupigwa na mwanga
F.Matatizo katika macho (conjuctivist)


Download kitabu cha Afya na Magonjwa
bofya hapa