VYNZO VYA MINYOO
Kama tulivyoona hapo mwanzo kuusu aina za minyoo, pia tumeona vyanzo vya minyoo hao kulingana na aina zao. Hapa ninakwenda kukuorodheshea kwa ufupi vyanzo hivi vya minyoo kwa ujumla wao na makundi yao:
1.kula kitu kisichooshwa kwema kwa maji yaliyo safi na salama. Wakati mwingine kuosha tu haitoshelezi, maana unaweza kuosha kwa maji ambayo yana vimelea vya minyoo, hivyo unajikuta hukufanya kitu. Kwani minyoo wanaishi ardhini, kwenye majani na kwenye maji.
2.Kunywa maji ambayo si masafi na si salama. Maji machafu yanaweza kuwa na mayai ama lava wa minyoo hii. Maji ambayo yamechanganyika na choo kikubwa yanakuwa na mazalia ya minyoo hii. Ni vyema kuchemsha maji hata yachemke, yapozwe na yahifadhiwe vyema kwa matumizi ya nyumbani na hata biashara.
3.Kula nyama ambayo haikuiva vyema, ama nyama mbichi. Upikaji wa nyama yeyote unatakiwa uwe wa makini sana. Kuhakikisha kuwa nyama imewiva vyema. Kuna baadhi ya nyama zinashauriwa kuwa makini sana katika kuzipika kama nyama ya ngurue na ya punda. Pia kuna aiana za samaki nao wanahitajika kuwapika vyema kama samaki aina ya kaa.
4.Kutembea pekupeku kwenye ardhi yeye minyoo. Minyoo huweza kuishi kwenye udongo, na ikitokea my akatembea bila ya viatu katika eneo hili, minyoo hawa wanaweza kupenya kwenye ngozi yake na kuingia mwilini.
5.Kula udongo, tunaona sana mara nyingi watu wanakula udongo, ukweli ni kuwa sio kila udongo unakuwa na minyoo. Kama utakuwa umeandaliwa vyema unaweza kuwa hauna minyoo. Lakini kula udongo kunaweza kusababisha minyoo. Pia kuna madhara makubwa sana ya kiafya katika kula udongo.
6.Kinyesi cha wanyama na binadamu. Hivi ni vyanzo vizuri sana vya minyoo. Kwani minyoo wanaweza kuishi kwenye kinyesi vyema na kwa muda mrefu zaidi kuliko maeneo mengine.