picha

Fahamu dawa ya kuzuia enzymes zinazotengenezwa na bakteria

Post hii inahusu zaidi dawa ya cloxacillin ambayo Iko kwenye kundi mojawapo la penicillin ambalo uzuia enzymes zinazotengenezwa na bakteria.

Dawa ya cloxacillin katika kupambana na bakteria ambao utoa enzymes Ili kuzuia kazi ya dawa kufanya kazi vizuri .

 

1. Kama tulivyoona hapo mwanzoni kwamba Kuna kundi mojawapo la penicillin ambalo usaidia kuzuia kazi ya bakteria ambao utoa enzymes Ili kuweza kuzuia kazi ya dawa kufanya kazi ipasavyo, hili kundi kwa kitaamu huiitwa penicillin resistance penicillase, kwa hiyo kwenye kundi hili Kuna dawa mojawapo ambayo huitwa cloxacillin, ni dawa ambayo imetengenezwa kwa ajili ya kupambana na bakteria hao .

 

2. Dawa hii ya cloxacillin imo kwenye makundi ya penicillin na pia dawa hii usaidia kutibu au kuzuia kukua kwa bakteria kwenye seli, ambapo Kuna bakteria ambao ukua  na kuzaliana kwenye seli kwa ajili ya kazi hii ya cloxacillin uzuia kukua na kuongezeka kwa bakteria kwenye seli na hivyo usaidia seli kuendelea na kazi zake za kuulinda na kuutunza mwili.

 

3. Vile vile dawa hii ya cloxacillin usaidia katika matibabu ya kwenye Koo , na pia usaidia kwenye matibabu ya mafua na vikohozi kwa ujumla, pia kwenye damu usaidia kuuua kila aina yeyote ya bakteria ambao ufanya kazi ya kuudhuru mwili kwa hiyo ni dawa nzuri kwa maambukizi ya bakteria kwenye damu.

 

4. Pia dawa hii huwa kwenye unga ambapo unga huo uchanganywa na maji rasmi ambayo Kwa kitaamu huiitwa water for injection na pia maji hayo na unga uchanganywa mpaka kuhakikisha hiyo poda haionekani kwa macho ila maji tu yaliyochanganyikana na dawa na pia dozi upewa kutegemea a na umri, kwa mtoto na mtu mzima na uzito pia. Kwa kawaida makasha ya dawa huwa na milligrams tofauti Kuna mengine Yana milligrams mia mbili hamsini na mengine milligrams mia tano zote utolewaa kulingana na wataalamu wa afya.

 

5. Dawa hizo utolewa kwa kupitia kwenye paja au Tako na utolewa kila masaa manane mpaka sita kadri ya maagizo ya wataalamu wa afya, na pia dawa hizi zinaweza kupitia kwenye damu , za kwenye damu utolewa taratibu na zenyewe utolewa kuanzia masaa manne mpaka matano kadri ya wataalamu wa afya. Vile vile Kuna nyingine uweza kuwa kwenye mfumo wa maji maji na pia kwenye vidonge kwa hiyo zote utolewa  kwa mgonjwa kwa kadri ya uhitaji au tatizo kwa sababu dawa hii utibu magonjwa mengi.

 

6. Dawa hii ya cloxacillin utolewa na watu mbalimbali ila wale  wenye aleji na dawa hii hawapaswi kuitumia, na pia wakati wa kutumia dawa hii umaskini unahitajika kwa sababu dawa Ina tabia ya kupunguza damu kwa hiyo wale wenye tatizo la upungufu wa damu wanapaswa kuitumia kwa taahadhari au kwenye uangalizi maalumu Ili kuweza kuzuia kuwepo kwa tatizo jingine au kusababisha Anaemia.

 

7. Dawa hii ya cloxacillin Ina maudhi madogo madogo wakati wa kutumia na maudhi hayo ni pamoja na kichefuchefu na kutapika, maumivu ya tumbo kuhisi kizunguzungu na wakati mwingine kuishiwa hamu ya kula, kupungukiwa damu, kwa hiyo kwa watumiaji baada ya kuitumia dawa hii mambo kama haya yanaweza kutokea kwa hiyo taahadhari ni muhimu ila hali ikiwa mbaya ni vizuri kuwaona wataalamu wa afya hasa kwa upande wa upungufu wa damu.

 

8. Pamoja na hayo yote ikumbukwe kwamba dawa hii haipaswi kutumiwa kiholela ila kinapaswa kuwepo kwa wataalamu wa afya Ili kuweza kuepuka madhara amabayo ya aweza kutokea , kwa sababu ikitumiwa nyumbani na mgonjwa mweye upungufu wa damu na dawa ikaendelea kupunguza damu ,hali inawezekana kuwa mbaya badala ya kutibu tunaleta tatizo juu ya tatizo.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Dawa Main: Post File: Download PDF Views 1748

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 ai web app     👉3 Dua za Mitume na Manabii     👉4 Bongolite - Game zone - Play free game     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zinazofanana:

Dawa ya Panadol au paracetamol katika kutuliza maumivu

Posti hii inahusu zaidi kazi ya paracetamol katika kutuliza maumivu, ni Aina ya dawa ambayo utumiwa sana katika kutuliza maumivu kwa wagonjwa.

Soma Zaidi...
Fahamu dawa zinazotumika kwenye matibabu ya kansa

Post hii inahusu zaidi dawa ambazo zinatumika kwenye matibabu ya kansa, dawa hizi usaidia kuharibu seli ambazo ambazo hazistahili kwa kitaalamu huitwa malignant seli.

Soma Zaidi...
Fahamu matumizi ya Ampicillin.

Ampicillin ni antibiotic yenye msingi wa penicillin ambayo inafanya kazi kupambana na maambukizi ya ndani ya bakteria. Ampicillin hufanya kazi ya kuharibu kuta za kinga ambazo bakteria huunda ndani ya mwili wako na kuzuia bakteria wapya kutokeza. Ampici

Soma Zaidi...
Penicillin dawa ya kutibu maambukizi ya bakteria mwilini

Post hii Inahusu zaidi dawa za kutibu maambukizi yoyote Yale yanayosababishwa na bakteria dawa hizi kwa kitaamu huiitwa antibiotics Kuna dawa mbalimbali zinazotibu maambukizi ya bakteria leo tutaanza na dawa ambayo inaitwa penicillin.

Soma Zaidi...
Dawa ya quinenes katika kutibu Malaria

Post hii inahusu zaidi dawa e quinine katika kutibu Malaria ni dawa inayotibu Ugonjwa wa Malaria ikiwa dawa nyingine zimeshindwa kufanya kazi.

Soma Zaidi...
Ijue dawa ya kutibu ugonjwa wa ukoma

Post hii inahusu zaidi dawa ya kutibu ukoma,na dawa hiyo ni dawa ya Dapsoni, hii dawa usaidia kuzuia nerve zisiendelee kupoteza kazi yake pia na ngozi iendelee kuwa kawaida

Soma Zaidi...