picha

Ifahamu dawa ya kutibu kifua kikuu

Post hii inahusu zaidi dawa ya Rifampin kama dawa mojawapo ya kutibu kifua kikuu.

Ifahamu dawa ya Rifampin kama dawa mojawapo ya kutibu kifua kikuu.

1.​​​​​1.Rifampsini ni mojawapo ya dawa ambayo imo kwenye daraja la kwanza katika matibabu ya kutibu kifua kikuu, tunafahamu kabisa kwamba ni bakteria anayesababisha kuwepo kwa kifua kikuu, kwa hiyo dawa aina ya Rifampin inapotumika kitu cha kwanza ni kuharibu protein ambayo inaitwa DNA ni protein ya bakteria kwa hiyo bakteria huyo anakuwa Hana uwezo wa kuishi tena na ugonjwa uweza kuishia hapo kwa sababu DNA iimeshaharibiwa.

 

2. Katika matibabu ya kifua kikuu dawa hii kwa kawaida haitibu yenyewe kama yenyewe Bali huwa na mchanganyiko na madawa mengine ambayo ni isoniazid, pyrazinamide na ethambutol na dozi yake huwa na muundo wa RHZE ambapo, R ni Rifampin, H ni isoniazid, Z ni pyrazinamide na E ni ethambutol kwa hiyo dawa hizo utumika zote kwa pamoja katika matibabu ya kwanza ya kifua kikuu na katika matibabu ya pili Rifampin huwa na isoniazid na muundo wao huwa ni RH ambapo R ni Rifampin na H ni isoniazid .

 

3. Kwa kawaida dawa ya Rifampin utolewa kwa muundo wa vidonge yaana umezwa kwa maji. na ni mara chache mno Kuna Rifampin ambazo utolewa kwenye mishipa ya damu, katika dawa zote za kifua kikuu dawa hii ya Rifampin ndio iliyo na nguvu zaidi na usaidia katika kupambana na bakteria ambaye kwa kitaamu huiitwa TB bacill na pia dawa hii utumika katika daraja la kwanza na la pili katika matibabu ya kutibu kifua kikuu pia ni dawa yenye nguvu kwa sababu uua bakteria wote walio sugu na wote wanaaoanza mashambulizi .

 

4. Dawa hii pia huwa na maudhi madogo madogo katika kutumia, maudhi hayo ni pamoja na kichefuchefu na kutapika, kuharisha, maumivu ya kichwa,na pia kuwepo kwa homa pia Kuna baadhi ya watu ambao huwa na viupele wanapokuwa wanatumia dawa hii ya Rifampin pia dawa hii inaweza kabisa kusababisha kupunguza kwa kwa kiasi cha aina ya protein ambayo Kwa kitaamu huiitwa platelate ,na pia kwa wakati mwingine kwa watumiaji wa dawa hii usababisha kupungua kwa kiwango cha damu kuganda .

 

5. Kiwango cha kupunguza kwa damu kuganda kwa kitaamu huiitwa clotting factors hali inayosababisha kupunguza kwa damu mwilini na kusababisha  hali Fulani ambayo Kwa kitaamu huiitwa Anaemia,na maudhi haya hayatokei kila mara ni mara chache na kwa watu wachache kwa hiyo watu wasiogope kutumia dawa hii kwa sababu ni sehemu ya matibabu .

 

6. Pia dawa hii inaweza kutumiwa na watu wote ila kwa wale ambao wanatumia uzazi wa mpango wenye vichocheo vya progesterone na oestrogen hawapaswi kutumia dawa hii kwa sababu dawa hii inaingiliana na hizi homoni na kusababisha kushika kwa mimba kwa sababu dawa hii ya Rifampin Ina nguvu kuliko hivi vichocheo kwa hiyo kwa wale wanaotumia dawa za kifua kikuu na pia wanatumia njia yoyote ya uzazi wa mpango wanapaswa kuomba ushauri kwa wataalamu wa afya kwa sababu wanaweza kupata mimba bila kutegemea au wanashauliwa kutumia njia nyingine za uzazi wa mpango kwa sababu ni nyingi.

 

7. Pia na akina Mama wenye maambukizi ya kifua kikuu na wamegundulika siku za mwisho karibia na kujifungua na kwa bahati mbaya na watoto au mtoto aliyezaliwa na yeye ana maambukizi ya kifua kikuu, kwa hiyo mama ataendelea na dawa na mtoto ataanzishiwa  Rifampin kwa hiyo mama hapaswi kumnyonyesha mtoto kwa sababu atamzidishia dozi au nguvu ya dawa itakuwa kubwa yaani dawa inayopitia kwenye maziwa  ya mama na dawa anayokunywa mototo. Kwa hiyo mtoto huyo  hapaswi kunyonya.

 

8. Pia katika matumizi ya dawa hii ni vizuri kabisa kupata ushauri wa daktari dawa hii haipaswi kutumika kiholela na ikitokea mtumiaji wa dawa amepata maudhi yakawa yasiyo ya kawaida ni vizuri kabisa kuwaona wataalamu wa afya kwa ushauri zaidi na pia kubadilishiwaa dawa kwa sababu katika matibabu ya kutibu kifua kikuu Kuna dawa za daraja la kwanza na la pili.

 

9. Pia kwa akina Mama wajawazito ni vizuri kabisa kupima kifua kikuu mapema Ili kuanza dawa mapema kuepuka na tatizo la kuambukiza mtoto na kusababisha mtoto kushindwa kunyonya kwa sababu maziwa ya mama ni ya muhimu na lazima kabisa kwa sababu mtoto asiponyonya ndicho chanzo cha utapiamlo na kidumaa kwa mtoto.

 

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Dawa Main: Post File: Download PDF Views 1697

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉2 Simulizi za Hadithi Audio     👉3 Dua za Mitume na Manabii     👉4 kitabu cha Simulizi     👉5 Bongolite - Game zone - Play free game     👉6 Kitau cha Fiqh    

Post zinazofanana:

Fahamau madhara ya flagyl (Metronidazole)

Flagyl ni nini? Flagyl (metronidazole) ni antibiotic. Inapigana na bakteria katika mwili wako. Flagyl hutumiwa kutibu maambukizo ya bakteria ya uke, tumbo, ngozi, viungo na njia ya upumuaji.

Soma Zaidi...
Ifahamu dawa ya kupunguza maumivu

Post hii inahusu dawa ya aspirin katika kupunguza maumivu,ni dawa ambayo upunguz maumivu ya Kawaida, kushusha homa na pia usaidia kwenye magonjwa ya moyo hasa kuzuia stroke kama imetokea mda ndani ya masaa ishilini na manne

Soma Zaidi...
Dawa ya kutibu mapunye

DAWA YA MAPUNYEMatibabu ya mapunye inategemea ni wapi mapunjye yapo.

Soma Zaidi...
Dapsone na kazi zake

Posti hii inahusu zaidi dawa ya Dapsone na kazi zake, hii ni dawa ambayo utumika katika kutibu ugonjwa wa ukimwi, dawa hii ufanya kazi kwa mchanganyiko wa dawa nyingine kama vile Rifampicin na clofaximine.

Soma Zaidi...
Matibabu ya ugonjwa wa uti wa mgongo

Posti hii inahusu zaidi matibabu kwa mgonjwa wa uti wa mgongo, kwa kawaida tunajua kuwa homa hii ya uti wa mgongo usababisha na wadudu mbalimbali kama vile bakteria, virus, fungasi, sumu mbalimbali kama vile madini ya lead na arseni, na vitu kama vile Mag

Soma Zaidi...