Baada ya kuonywa wasionyeke, Allah(s.
Baada ya kuonywa wasionyeke, Allah(s.w) aliwaangamiza kama walivyoangamizwa akina Ad, Thamud, n.k.
Basi mtetemeko wa ardhi uliwatoa roho zao, wakawa wasiojimudu, (wamekufa) humo mjini mwao. Wale waliomkadhibisha Shu’ayb wakawa kama kwamba hawakuwako (mahala hapo). Wale waliomkadhibisha Shu’ayb ndio waliokuwa wenye khasara. (7:91-92)
Na ilipokuja amri yetu, tulimuokoa Shu’ayb na wale walioamini pamoja naye kwa rehema yetu. Na wale waliodhulumu ukelele (wa adhabu) ulinyakuwa roho zao. Wakawa majumbani mwao wametulia tu (wamekufa).(11:94)
Kama kwamba hawakuwamo humo. Sikilizeni. Wameangamia (watu wa) Madiana kama walivyoangamia (kina) Thamudu. (11:95)
Kwa mujibu wa aya hizi, watu wa Madian waliangamizwa kwa ukelele ukifuatiwa na tetemeko la ardhi. Tukikumbuka kuwa:
Na majeshi ya mbingu na ardhi ni ya Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu; Mwenye hikima. (48:7)
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Uislamu unaitazama dini katika nyanja zote za maisha ya mwanadamu. Hii ni tofauti na mtazamo wa kikafiri juu ya dini.
Soma Zaidi...Mitume wameletwa kuwa Waalimu na viongozi wa kuwafundisha watu Uislamu na kuwaelekeza kuusimamisha Uislamu katika jamii kinadharia na kimatendo kama tunavyojifunza katika Qur-an:“Kwa hakika Tuliwapeleka Mitume wetu kwa dalili wazi wazi na Tukavitere..
Soma Zaidi...Tunajifunza katika Qur-an na hadithi sahihi kuwa Imani ya Kiislamu imejengwa juu ya nguzo sita zifuatazo:1 Kumuamini Allah (s.
Soma Zaidi...