Allah anatutaka kuchunguza umbile na mbingu na ardhi ili kupata mazingatio.
“Katika kuumbwa mbingu na ardhi na mfuatano wa usiku na mchana,ziko alama (hoja) za kuonyesha kuwepo Allah (s.w) kwa wenye akili.” (3:190).
Mungu, Muumba wa kila kitu ndiye mmiliki pekee wa viumbe vyote. Ni Yeye anayebadili mielekeo ya upepo,anayekusanya mawingu, anayewasha jua na kuiangazia dunia na kudhibiti sayari zizunguuke katika mihimili yao.
Kudai maisha haya ya dunia na ulimwengu mzima yanatokana na bahati nasibu ni kutokitumia kipawa cha busara alichotunukiwa kila mwanaadamu mwenye akili timamu. Mpango bora wa dunia na ulimwengu kwa ujumla unapinga uwezekano wa kutokea kwa bahati nasibu tu, na kinyume chake ni ishara ya wazi ya uwezo wa Allah(s.w)usio na kikomo unaodhihirisha kuwepo kwake.
Wakati ambapo ni muhali hata kwa kitu chepesi kufanya mzunguko wa moja kwa moja katika njia yake bila kwenda kombo, dunia pamoja na ukubwa wake yenye mkusanyiko wa vitu visivyo na idadi hufanya hivyo.
Na imekuwa ikifanya hivyo kwa miaka dahari, na dahari, tangu dunia kuumbwa na kuanza mzunguko wake. Allah anasema Yeye ndiye mfanyaji wa mahesabu ya mzunguko huo.
Hakika Mw enyezi Mungu am ekw is ha kiw ekea kila kitu kipimo chake. (65:3)Utaratibu huo bora wa ulimwengu unaendeshwa kwa mfumo wa ajabu unaokwenda kwa kutegemea mihimili isiyo na mashiko.Wengine hudhani kuwa baada ya kuumba, Allah(s.w)amekiacha kila kitu kijiendeshe chenyewe tu. La hasha kila tukio litokealo mahala popote pale ulimwenguni hutokea kwa idhini ya Allah(s.w) na chini ya udhibiti wake. Qur’an inatufahamisha:
Je! Hujui ya kwamba Mwenyezi Mungu anajua yaliyoko mbinguni na ardhini? Bila shaka yote yamo kitabuni mwake. Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni sahali. (22:70)
Umeionaje Makala hii.. ?
Vipawa vya mwanaadamu ni sababu nyingine inayomfanya mwanaadamu asiweze kuishi bila ya kufuata dini moja au nyingine.
Soma Zaidi...Huwaoni wale wanaodai kwamba wameamini yale yaliyoteremshwa kwako na yaliyoteremshwa kabla yako?
Soma Zaidi...Nguzo za Imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Ni upi mgawanyo sahihi wa elimu kwa mtazamo wa uislamu (EDK form 1: mgawanyo sahihi wa elimu kwa mtazamo wa uislamu
Soma Zaidi...Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Hii ni njia ambayo mwanaadamu huongeleshwa moja kwa moja na Allah (s.
Soma Zaidi...