Maswali juu ya nguzo za Imani

Maswali juu ya nguzo za Imani

Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Zoezi la 2.

  1. “Mungu hayupo kwa sababu milango ya fahamu haitambui”. Hii ni kauli ya Charles Darwin na wenzake juu ya kupinga uwepo wa Mungu Muumba. Onesha madai yao na madhaifu ya kila dai.
  2. Suala la kuamini kuwepo Mwenyezi Mungu si la ububusa na kufuata mkumbo, bali linahitaji ushahidi na dalili. Thibitisha kauli hii kwa kutoa sababu kuu tano.

 

  1. (a)  Orodhesha nyanja tano zinazoonesha kuwepo Mwenyezi Mungu.

(b)  kwa kutumia historia ya maisha ya mwanaadamu, Onesha kuwepo kwa Mwenyezi Mungu.

  1. “Na katika nafsi zenu (kuna ishara) je, hamziyakinishi”? (51:21).

Kutokana na aya hii eleza ni kwa vipi nafsi (dhati) ya mwanaadamu inaonyesha uwepo wa Mwenyezi Mungu.

 

  1. Maisha ya Mitume ni uthibitisho tosha juu ya kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w).

Thibitisha kauli hii.

  1. Bainisha athari ya maisha ya kila siku ya muumini wa kweli aliyemuamini Mwenyezi Mungu (s.w).
  2. (a)  Nini maana ya shirki.

(b)  Nini maana ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu katika maisha ya kila siku.

(c)  Taja makundi ya shirki.

 

8.   (a) “Kwa hakika shirki ni dhulma kubwa” (31:13).

         Kutokana na aya hii, onesha kina cha uovu wa shirki kwa mwenye kushirikisha.

      (b) Ni ipi maana halisi ya kumuamini Mwenyezi Mungu (s.w) katika maisha ya kila siku?

    9.   (a)  Orodhesha sifa za Malaika unazozifahamu.

          (b)  Ni yapi majukumu ya Malaika?

          (c)    Ni upi umuhimu na maana ya kuamini Malaika katiaka maisha yetu ya kila siku?

    10. (a)  Bainisha Vitabu vilivyotajwa ndani ya Qur’an na Mitume walioteremshiwa kwayo.

          (b)  Kwa nini ni Kitabu cha Qur’an pekee ndio chenye sifa ya kuongoza maisha sahihi?

      (c)  Onesha dosari ya Vitabu vilivyotangulia kutoaminika kuwa muongozo sahihi wa maisha ya mwanaadamu.

 

11.  ‘Kwa hakika Kitabu cha Qur’an hakikaribiwi na batili mbele yake wala nyuma yake.’

          Kwa mujibu wa kauli hii, toa tofauti tano kati ya Qur’an na Vitabu vilivyotangulia.

    12.  Ni lipi lengo la kuteremshwa Vitabu vya Mwenyezi Mungu (s.w)?

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tawhid Main: Post File: Download PDF Views: 3118

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
πŸ‘‰1 kitabu cha Simulizi     πŸ‘‰2 web hosting     πŸ‘‰3 Simulizi za Hadithi Audio     πŸ‘‰4 Bongolite - Game zone - Play free game     πŸ‘‰5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     πŸ‘‰6 ai web app    

Post zinazofanana:

Mgawanyiko wa elimu usiokubalika katika uislamu

Ni mgawanyo upi wa elimu haukubaliki. Ni ipi elimul akhera na elimu dunia? (Edk form 1 Dhana ya elimu)

Soma Zaidi...
Maana ya uislamu.

Kwenye kipengele hichi titajifunza maana ya uislamu,na maana nyingine tofauti.

Soma Zaidi...
Himizo la kuwasamehe waliotukosea

β€œNa wasiape wale wakarimu na wenye wasaa miongoni mwenu, kujizuia kuwasaidia jamaa zao, maskini na wale waliohama kwa ajili ya Dini ya Allah; na wasamehe na waachilie mbali (wapuuze yaliyopita).

Soma Zaidi...
Mtazamo wa Uislamu juu ya maana ya dini

Uislamu unaitazama dini katika nyanja zote za maisha ya mwanadamu. Hii ni tofauti na mtazamo wa kikafiri juu ya dini.

Soma Zaidi...
Maswali juu ya dini anayostahiki kufuata mwanadamu

Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...