Mtazamo wa uislamu juu ya dini (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Kwa nini mwanaadamu hawezi kuishi bila ya dini?
Mwanaadamu yeyote hawezi kuishi bila ya dini hata kama atadai kuwa hana dini kwa sababu zifuatazo;
Maana halisi ya dini.
Dini ni utaratibu wa maisha anaofuata mwanaadamu katika kuendesha maisha yake ya kila siku kibinafsi na kijamii.
Umbile la mwanaadamu ni la kidini.
Umbile la mwanaadamu limefungamana na kanuni na sheria za maumbile yote yanayomzunguka.
Rejea Quran (30:30), (3:83).
Vipawa alivyotunukiwa mwanaadamu.
Tofauti na wanyama na viumbe wengine, mwanaadamu ametunukiwa vipawa vya ziada vifuatavyo;
Akili na Ufahamu wa hali ya juu.
Vinamsaidia kufikiri na kutafakari mambo yanayomhusu yeye mwenyewe na mazingira yanayomzunguka.
Utambuzi binafsi (self-consciousness).
Humuwezesha kuhusianisha yeye na mazingira (viumbe) yanayomzunguka.
Uwezo wa kujielimisha na kuelimika.
Elimu ni nyenzo pekee inayomuwezesha mwanaadamu kuyamudu mazingira kwa ufanisi.
Uhuru wa kufanya atakalo.
Mwanaadamu amepewa vipaji, elimu na ujuzi, ilivimuwezeshe kubainisha njia sahihi ya kufuata katika maisha yake ya kila siku.
Umeionaje Makala hii.. ?
Kwenye mada hii tutajifunza shahada mbili,tafsiri ya shahada kstika maisha ya kila siku.
Soma Zaidi...Ninichanzo cha Elimu? (EDK form 1 Dhanaya Elimu)
Soma Zaidi...Posti hii inaonyesha dalili,sababu na mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa aliyepata jeraha kwenye ngozi kwa kuingiliwa na kitu Kama mwiba,Pini,sindano n.k
Soma Zaidi...Allah hutumia maandishi kuwafundisha wanadamu. Mfano mzuri ni nabii Musa ambaye alipewa vibao vya maandishi.
Soma Zaidi...Ni nini maana ya Elimu na ni nani aliye elimika? Uislamu una mtazamo gani juu ya Elimu?
Soma Zaidi...