Mgawanyiko wa Elimu kwa mtazamo wa kikafiri

Kwa mtazamo wa kikafiri elimu imegawanyika katika makundi mawili ambayo ni Elimu ya dunia na Elimu ya akhera.

Katika akafiri na hata baadhi ya Waislamu kutokana na mtazamo wao finyu juu ya maana ya dini iliyowapelekea kuyagawanya maisha ya binaadamu kwenye matapo mawili; maisha ya dini na maisha ya dunia, wameigawanya elimu kwenye matapo hayo mawili.

 

Kwa mtazamo huu potofu elimu ya dini ni ile inayoshughulikia maswala ya kiroho (spiritual life) ya mtu binafsi inayoishia katika kumuwezesha mtu kuswali, kufunga na kutekeleza Ibada nyingine maalumu kama hizi bila ya kuzihusisha na maisha yake ya kila siku ya kibinafsi, kifamilia na kijamii.

 

Hivyo elimu hii haina nafasi ya kumuwezesha binaadamu kuendea maisha yake ya kila siku ya kijamii.

 

Elimu ya Dunia kwa mtazamo huu wa makafiri, ni ile inayojishughulisha na masuala ya kijamii kama vile uchumi, siasa, utamaduni, sheria na maongozi ya jamii kwa ujumla kwa kufuata maelekezo na matashi ya binaadamu bila ya kuzingatia mwongozo wa Allah (s.w).

 

Kwa mtazamo wa mgawanyo huu, elimu ya dini ndiyo iliyofundishwa na Allah (s.w) kupitia kwa Mitume na Vitabu vyake na elimu ya dunia imebuniwa na binaadamu wenyewe kwa msukumo wa matashi na mahitaji yao katika kuendea kila kipengele cha maisha yao ya kimaada (Physical or Material life)

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Tawhid Main: Dini File: Download PDF Views 1470

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 Kitau cha Fiqh    👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉5 Kitabu cha Afya    👉6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana:

Neema za Allah(s.w) Juu ya Bani Israil

Katika Qur'an tunakumbushwa neema mbali mbali walizotunukiwa Bani Israil (Mayahudi) na Mola wao ili kuwawezesha kusimamisha Ufalme wa Allah(s.

Soma Zaidi...
Mwanadamu hawezi kuishi bila ya dini kutokana na maumbile yake

Kuwa ni kwa nini mwanadamu hawezi kuishi bila ya dini kutokana na umbile la mwanadamu.

Soma Zaidi...
NGUZO ZA IMAN

Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala

Soma Zaidi...
Nafasi ya Elimu katika uislamu

Je ni ipi nafasi ya Elimukatika dini ya uislamu?

Soma Zaidi...
Kumuamini mwenyezi Mungu (S.W)

Nguzo za imani (EDK form 2: elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Tawhiid

Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Maamrisho ya kushikamana nayo

Yale tunayoamrishwa kushikamana nayo ni haya yafuatayo: (i)Kumuabudu Allah (s.

Soma Zaidi...