Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya tumbo wakati wa tendo la ndoa
MAUMIVU YA TUMBO WAKATI WA TENDO LA NDOA
Maumivu wakati wa tendo la ndoa hutokea sana na pengine ni kawaida hasa kwa wanawake. Ijapokuwa kwa wanaume sio sana. Maumivu haya yanaweza kuwa ya tumbo, ya kiuno, ama viungo vya siri yaani uume na uke. Pia maumivu haya yanaweza kutokea wakati wa tendo la ndoa ama baada.
Je na wewe ni katika wanaopatwa na maumivu makali wakati wa tendo la ndoa. Na je umepata kujuwa chanzo cha tatizo lako?. makala hii ni kwa ajili yako. Katika makala hii tutakwenda kuona maumivu ya tumbo wakati wa tendo la ndoa.
Sababu za maumivu ya tumbo wakati wa tendo la ndoa.1.Mkao uliotumika. Ipo baadhi ya mikao inaongeza uwezekano wa kupatwa na maumivu ya tumbo wakati wa tendo. Mikao hii ni ile ambayo inaruhusu uume kuingia ndani zaidi. Kama unasumbuliwa na tatizo hili jaribu kutumia mikao ambayo utaweza kudhibiti uingiaji wa uume.
2.Kama tumbo la uzazi (uterus) limeinama kidogo. Hii hutokea pale tumbo la uzazi linapolalia nyuma kidogo kuelekea kwenye shingo ya uzazi. Hali hii huwewa kupelekea maumivu ya tumbo wakati wa tendo la ndoa.
3.Maka una tatizo la kuota tishu zinazopaswa kuota kwenye tumbo la uzazi zikaota sehemu nyingine. Hali hii hutambulika kama endometruisis. Haki hii huweza kupelekea maumivu ya mgongo, nyonga na tumbo wakati wa tendo la ndoa. Dalili za hali hii ni pamoja na:-
A.Maumivu makali zaidi wakati wa tendo la ndoaB.Kupata hedhi yenye damu nyingiC.Kutokwa na damu kabla na baada ya kumaiza hedhiD.Maumivu ya tumbo
4.Kama ovari ina matatizo yaani inajaa maji, hali hii hutambulika kama ovarian cysts. Hii hutokea endapo juu y aovari ama ndani kunkuwa na kama vijifuko vijidogo vinajaa maji. Sasa vikiwa vidogo havinaga maumivu ila vikiwa ni vikubwa vinaweza kupelekea maumivu ya chini ya tumbo. Maumivu haya yanaweza kuwa makali zaidi wakati wa tendola ndoa. Pia mtu anaweza kupata dalili zifuatazo:-
A.Maumivu ya mgongo wa chini ama kwenye mapajaB.Unahisi tumbo limejaa ama kushiba, ama tumbo linakuwa zitoC.Tumbo kujaa gezi na kucheua gesi kwa mdomoni.
5.Kama kuna mashambulizi kwenye kibofu kitaalamu hali hii huitwa interstial cystitis. Misuli ya kwenye kibofu inashambuliwa na kuvimba na baadaye kutoa dalili kama:-A.Maumivu ya tumbo na nyongaB.Kukojoa mara kwa maraC.Kujihisi kukojoa tena punde baada ya kukojoaD.Kuvuja kwa mkojo yaani kutoka mkojo bila ya wewe kujuwa.E.Maumivu kwenye uke na mashavu ya uke (papa)
6.Kuwa na uvimbe kwenye tumbo la mimba kitaalamu huitwa fibroid. Huu ni uvimbe usiosabababishwa na saratani. Uvimbe huuu huweza kuleta dalili kama:-A.maumivu ya tumbo na mgongo sehemu ya chiniB.Kupata damu nyingi ya hedhi pamoja na maumivu makaliC.Maumivu wakati wa tendo la ndoaD.Kukosa choo.
7.Kama mtu ana maradhi ya ngono kama gonoria na chlamydia. Hapa mtu anaweza kuona dalili kama:-A.Kutokwa na uchafu ukeniB.Kutoka na harufu mbaya ukeniC.Maumivu wakati wa kukojoa na kuhisi kama unaunguwaD.Maumivu ya tumbo kwa chini pamoja na nyongaE.Maumivu na kutokwa na damu wakati wa hedhi na baada ya hedi
8.UTI na PID; kwa pamoja haya ni mashambuizi ya bakteria ama fangasi ama virusi. Mashambulizi haya huathiri mfumo wa uzazi hapa itakuwa na PID na endapo yatashambulia mfumo wa mkojo itakuwa ni UTI. ugonjwa wa UTI na PID huweza kusababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa.
Dalili za PIDA.Maumivu makali ya nyonga wakatii wa tendo la ndoaB.Maumivu wakati wa kukojoaC.Kutokwa na damu wakati wa hedhi na baada
Dalili za UTIA.Maumivu ya tumbo ambayo huongezeka wakati wa tendo la ndoaB.Maumivu wakati wa kukojoaC.Kukojoa mra kwa maraD.Mkojo mchafu na wenye harufu kali.
9.kama kuna uvimbe katika tezi dume.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi ongezeko la homoni ya estrogen, kwa kawaida homoni hii ya estrogen inapaswa kulingana ikitokea ikaongezeka uleta madhara mbalimbali kwenye mwili na Kuna dalili ambazo zzz inaweza kujionesha wazi mpaka tukafahamu kuwa ni tatizo la o
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Dalili ambazo ujitokeza kama kuna Maambukizi yoyote kwenye kitovu cha mtoto mdogo, kwa kawaida kitovu cha mtoto kama kiko vizuri kinapona kwa mda mchache na kinakauka mapema iwezekanavyo bila kuwa na tatizo lolote ila kama kuna Dal
Soma Zaidi...Kama unapata maumivu wakati wa tendo la ndoa, suluhisho lako lipo kwenye makala hii
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za kuwepo kwa Ugonjwa wa fangasi,ni sababu mbalimbali ambazo zinaweza kusababisha fangasi.
Soma Zaidi...Post huu inahusu zaidi mambo yanayopelekea ugumba kwa wanaume, ni mambo ambayo uchangia au upelekea mwanaume kukosa uzazi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi maji ya Amniotic ni maji ambayo uzunguka mtoto na kufanya kazi mbalimbali kama ifuayavyo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo mwanamke hapaswi kufumbia macho.
Soma Zaidi...Je unawaza nini endapo bikra itatolewa bila wewe kukusudia, je imetolewa kwa njia ya kawaida yaani uume ama ilikuwa ni ajali?
Soma Zaidi...