Kama tulivyosema hapo juu kuwa afya ni kuwa mzima kimwili na kiakili.
Kama tulivyosema hapo juu kuwa afya ni kuwa mzima kimwili na kiakili. Hata hivyo nadharia ya afya haiishii hapa ila inaendelea hata kujengwa katika mambo makuu sita. Mambo haya wataalamu wa afya wanayaita components of health. Mambo haya nitayataja hapa chini kwa ufupi tuu kama ifuatavyo
1.afya ya kimwili (physical health); hapa ni kuwa mzima kimwili, na afya hii huweza kujenga kwa kula vizuri, kufanya mazoezi ya mara kwa mara, kuepuka unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara na matumizi ya madawa ya kulevya. Ukifanya hivi unaweza kuboresha mwili wako na kuboresha afya ya kimwili.
2.afya ya kiakili (mental health); hapa tunaangalia kuwa salama kiakili. Mtu akiwa na afya salama ya kiakili anakuwa na uwezo wa kujiamini, anapenda kujifunza vitu vivya na anavifurahia. Mtu mwenye hali hizi tunasema ana afya ya kiakili. Uwoga wa kuogopa watu ni katika maradhi ya kiakili.
3.afya ya mawazo na hisia (emotional health); hapa mtu anauwezo wa kuelezea hisia zake na mawazo yake. Kama kuna jambo limemuudhi analisema. Matu mwenye afya hii anauwezo wa kutaka msaada kwa mtu mwingine bia ya wasi.
4.Afya ya kiroho (spiritual health); hii ni afya inayojengwa na kuwa na imani juu ya mambo fulani. Na mara nyingi hapa tunazungumzia kuwa na imani juu ya dini. Watalamu wa afya wanaonesha mahusiano makubwa kati ya dini na mtu. Wataalamu wanatuambia zaidi matu mwenye imani ya kuna uwezekano mdogo wa kupata maradhi ya moyo kuliko mtu asiye na imani ya dini.
5.afya ya kijamii (social health); hii ni afya inayojengwa na kuwa na mahusiano mazuri na jamii. Kusaidia watu, kuitikia watu wanapokuita na kucheka nao na kuzungumza nao ni katika mambo yanayojenga afya hii. Wataalamu wa saikolojia wanatueleza mengi kuhusu afya hii.
6.afya ya mazingira (environmental health); hii afya hujengwa na mazingira yanayotuzunguka. Mtu awe na uwezo wa kupata hea safi na maji safi. Hivi hujenga afya hii. Mazingira kuwa safi na salama huweza kutengeneza afyahii.
Umeionaje Makala hii.. ?
Mlo kamili ni mkusanyiko kuu wa vyakula mbalimba kwa pamoja huimarisha na kuujenga  mwili wa binadamu na wanyama kwa sababu vinaleta virutubishi vyote vinavyohitajika.  Mkusanyiko wa vyakula vinavyotengeneza mlo kamili Kuna majina ya vyakula
Soma Zaidi...hapa Tutakwenda kuona Vyakula Vya vitamini B, kazi za Vitamini B na dalili za Upungufu wa Vitamini B mwilini
Soma Zaidi...Je ulaji wa boga unafaa kwa mgonjwa wa kisukari?
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula kisamvu
Soma Zaidi...Post hii itakwenda kukufundisha vyakula ambavyo ni vizuri kwa mwanamke anayenyonyesha ili kumsaidia kupata maziwa kwa wingi.
Soma Zaidi...Somo hili litakwenda kukueleza kuhusu faida za kula zabibu na umuhimu wake kiafya
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula apple/tufaha
Soma Zaidi...Hpa utafahamu faida za maji mwilini pamoja na athari za upungufu wa maji mwilini na dalili zake
Soma Zaidi...