picha

Maumivu ya tumbo baada ya kula

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya tumbo baada ya kula

MAUMIVU YA TUMBO BAADA YA KULA

 

Baada ya kula ni wakatiwa wa kupumzika, lakini sivyo kwa baadhi ya watu. Wao anapomaliza tu, anangojewa na maumivu ya tumbo. Je unajuwa sababu?, je na wewe unapatwa na maumivu ya tumbo baada ya kumaliza kula? Makala hii ni kwa ajilli yako.

 

Kwa ufupi maumivu haya yanaweza kusababishwa na mchafuko wa tumbo. Tunapozungumzia mchafuko wa tumbo tunazungumzia mmeng’enypo wa chakula unakuwa na hali ambayo si ya kawaida.

 

Dalili za mchafuko wa tumbo ni kama:-A.KichefuchefuB.KuharaC.Kiungulia ama kucheuaD.Kujaa tumbo na kutoa hewa kwa mdomoni. Kwa kucheuaE.Maumivu ya tumboF.Kushiba kusikkokuwa kwa kawaidaG.Lushiba kwa harakaH.Maumivu ya sehemu ya juu ya tumboI.Kuhisi kuunguwa chini ya tumboJ.Kuhisi kuunguwa kifuani na maumivu ya kifuaK.Kutapika

 

Nini husababisha maumivu ya tumbo baada ya kula?Kwa hakika kuna sababi nyingi ambazo zinaweza kupelekea maumivu ya tumbo baada ya kula. Sio hivyo tu pia tumbo linapatwa na machafuko makubwa kwa mfano kutapika, kichefuchefu, kuharisha na mengineyo. Sasa ni zipi sababi hizo zinazoletwa maumivu ya tumbo baada ya kula?

 

1.Aleji ya chakula.2.kuna baadhi ya vyakula huwa vina aleji, hii hutokea pale mwili mwili unapokidhania chakula kuwa hakipo salama, na kuanza kukishambulia ili kukitoa. Hali hii hupelekea maumivu ya tumbo kama matokeo ya mpambano. Baadhi ya vyakula vyenye aleji ni kama:-1.Maziwa2.Maharagwe ya soya3.Baadhi ya samaki4.Vyakula jamii ya karanga na korosho5.Mayai6.Ngano

 

3.kama mfumo wa kumeng’enya chakula umeshindwa kukivumilia aina ya chakula ulichokula. Yaani mfumo wa chakula unashindwa kukimeng’enya kabisa ama kinameng’enywa lakini si kwa ufasaha. Kwa mfano baadhi ya vyakula vilivyotengenezwa na maziwa kwa baadhi ya watu inakuwa ni tatizo na hupelekea mvurugiko wa tumbo.

 

4.kama ukuta wa utumbo mdogo umeathiriwa na protini ya gluten, protini inayopatikamna kwenye nafaka kama ngano na shayiri. Hali hii hutambulika kama celiac disease.

 

5.Kama una tatizo la kupanda kwa tinikali za tumboni kuja juumkwenye koo sehemu inayojulikana kama esophagus. Tindikali hii inaweza kuathiri kuta za kiungo hiki na kusababisha machafuko ya tumbo. Hali hii kitaalamu hutambulika kama Gastroesophageal disease (GERD)

 

6.kama una matatizo kwenye utumbo mkubwa kwa kitaalamu huitwa irritable bowel syndrome. Hali hiii inaweza kuonyesha dalili kama:-A. Maumivu ya tumboB.Kujaa kwa tumboC.KuharishaD.Kukosa chooE.Kujaa gesi

 

7.Kuvimba kwa baadhi ya sehemu kwenye mfumo wa kumeng’enya chakula. Mgonjwa anaweza kuona dalili kama maumivu ya tumbo, kuhara, damu kwenye kinyesi n.k

 

8.Kama una vidonda vya tumbo. Vidond vya tumbo vinaweza kusababisha maumivu ya tumbo baada ya kumaliza kula.

 

9.Kukosa choo. Hali hii hutokea pale chakula kinapotembea kidogokidogo katika njia ya mmeng’enyo wa chakula.

 

Namna ya kujikinga na maumivu ya tumbo baada ya kula.1.Kama kuna chakula unakumbuka kilikuletea matatizo kama haya hebu kiepuke2.Kula chakula chenye kambakmba kwa wingi na matunda3.Kunywa maji mengi4.Punguza unywaji wa pombe5.Punguza matumizi ya caffein (majani ya chai kwa wingi)6.Punguza misongo ya mawazo

 

?

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Vyakula Main: Post File: Download PDF Views 4326

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Dua za Mitume na Manabii     👉3 Bongolite - Game zone - Play free game     👉4 ai web app     👉5 web hosting     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zinazofanana:

Je ulaji wa boga unafaa kwa mgonjwa wa kisukari?

Je ulaji wa boga unafaa kwa mgonjwa wa kisukari?

Soma Zaidi...
je ni vipi vyakula vyenye protini kwa wingi?

Makala hii iatakuletea aina kuu tano za vywkula vyenye protini nyingi zaidi. Kama ulikuwa unajiuliza kuwa ni vyakula ipi hasa vinaweza kukupatia protini kwa wingi ni vipi, makala hii ndio majibu yako kwa swali hilo.

Soma Zaidi...
Faida za kiafya za peaz/ peas

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula peazi

Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula tango

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula tango

Soma Zaidi...
Vitamini na kazi zake

Posti hii inahusu zaidi vitamini mbalimbali na kazi zake kwenye mwili,vitamini ufanya kazi mbalimbali kwenye mwili kama ifuayavyo.

Soma Zaidi...