vitamini B vipo katika makundi mengi kma aB1, B2, B3, B5, B6, B7 na B12. Makala hii itakwenda kukutajia kazi kuu za Vitamini B katika miili yetu
Kazi za vitamini B mwilini Na upungufu wa vitamini B mwilini
Kama tulivyoona kuwa kazi za vitamini B ni kuhakikishha kuwa mipambano ya kikemikali inafanyika ndani ya seli. Sasa hapa tutaona kazi za vitamini hivi kulingana na makundi yake:-
B1 hii husaidia mfumo wa fahamu (mfumo wa neva) kufanya kazi vyema. Upungufu wa vitamini hivi B1 huweza kuleta maatizo kwenye mfumo wa fahamu, moyo na mupotea kwa misuli.
B2 huhitajika kwa ajili ya uzalishwaji wa nishati, lipi, vitamini, madini na husaidia katika utengenezwaji wa antioxidant. Upungufu wa vitamini hivi huweza kusababisha kuvimba (imflamation) kwenye ngozi, ulimi, midomo, na matatizo kwenye mfumo wa fahamu.
B3 hii huhitajika katika kufanyika mchakato wa metabolism kwenye seli. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea ngozi kuwa na matatizo kama miwasho, mapele, ukurutu na kadhalika. Pia upungufu wa vitamini hivi huweza kusababisha tumbo kuvurugika na kuleta misongo ya mawazo
B6 hii hufanya kazi ya kuhakikisha metabolisma inayohusima katika kuchakata hamirojo asidi za amino, kuchakata hemoglobin hizi ni chembechembe za kwenye seli nyekundu za damu zinazo saidia katika kusafirisha hewa mwilini, pia katika kuthibiti kiwango cha sukari kwenye damu. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea madhara kwenye ubongo, shida kwenye fahamu ya mtu na pia ugonjwa wa anemia unaonasibiana na upungufu wa hewa ya oksijeni mwilini.
B9 huhusika katika kuchakata DNA, kuchakata amino acid, katika kukua na kukomaa kwa seli mwilini hasa hasa seli hai nyekundu. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea matatizo katika ukuaji, utengenezwaji na ukomaaji wa seli hai nyekundu za damu, uchovu, maumivu ya kichwa, kutokea uvimbe kwenye mdomo na hata kuathiri mtoto aliyepo tumboni.
B12 huhitajika kwa ajili ya utengenezwaji wa seli mpya, utengenezwaji wa damu na pia kwa ajili ya mfumo wa fahamu kufanya kazi vyema. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea kuvurugika kwa tumbo, shida kwenye mfumo wa fahamu pamoja na matatizo kwenye ulimi.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kisamvu
Soma Zaidi...Tangaizi ni katika mimea yenye asili na bara la asia hususan nchi ya China.
Soma Zaidi...Pera ni tunda bora lakini pia ni dawa, tambua umuhimu wa tunda hili kiafya
Soma Zaidi...Matunda yenye vitamni C kwa wingi ni machungwa, maembe, ndimu na limao, endelea kusoma
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula korosho
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi magonjwa nyemelezi kwa watoto wadogo chini ya miaka mitano,. Ni magonjwa yanayowapata watoto wadogo kwa sababu kinga Yao bado ni ndogo.
Soma Zaidi...Ukubwa wa tikiti unasadifu yaliyopo, kwani kuna fgaida akubwa sana za kiafya katika kula tikiti
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha utaratibu wa lishe kwa wagonjwa wenye kisukari pamoja na vyakula salamakwao.
Soma Zaidi...