Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kitunguu thaumu
FAIDA ZA KITUNGUU THAUMU
Kitunguu thaumu ni katika viungo vya mboga na chakula. Karibia maeneo yote duniani wanatumia kitungiuu thaumu. Kitunguu thaumu huweza kutumika kikiwa kibichi. Wataalamu wa afya wanaeleza faida nyingi za kiafya. Wataalmu wa afya wametengeneza kidonge kwa kutumia vitunguu thaumu ili kuwezesha upatikanaji wa virutubisho vya mmea huu.
Kitunguu thaumu kina chembechembe nyingi ambazo ndizo husaidia katika tiba. Miongoni mwa chembechembe hizo ni chembechembe za salfa ziitwazo allicin. Allicin hupatikana kwenye kitunguu kibichi pindi kinapopondwa ama kutafunwa. Chembechembe nyingine ni kama diallyl disalfide na s-allyl cysteine.
Zifuatazo ni faida za kiafya za kitunguu thaumu
1. Kunapatikana virutubisho vingi ndani ya kitunguu thaumu kama vitamini B6, B1 na vitamini C. madini ya calcium, copper, phosphoros, potassiumna selium.
2. Hushusha presha ya damu (hypertsnsion). kitunguu thaumu sio kizuri kwa wenye presha ya kushuka, kwani itashuka sana.
3. Hudhibiti cholesterol (kolesto) hivyo husaidia katika kuzuia hatari ya kupata maradhi ya moyo.
4. Kitunguu thaumu kina antioxidant ambazo husaidia kupunguza hatari ya kupata maradhi ya kusahausahau
5. Huimarisha mfumo wa kinga mwilini.
6. Huondoa sumu za vyakula mwilini.
7. Huimarisha afya ya mifupa.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Katika post hii utakwenda kujifunza aina 20 za vitamini. Utajifunza kazu zake mwilini, vyanzo vyake na madhara yanayoweza kutokea kutokana na upungufu wake.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula asali
Soma Zaidi...Kuchaguwa vinywaji si jambo rahisi, lakini inabidi iwe hivyo kama una tatizo la kisukari. Je unasumbuka kujuwa vinywaji salama? makala hii ni kwa ajili yako, hapa tutaona vinywaji ambavyo ni salama kwa mwenye kisukari.
Soma Zaidi...Matunda ya zamani, matunda ya asili, Zaituni tunda lipendezalo, zijuwe faida zake leo
Soma Zaidi...Zijuwe dawa za kuongeza nguvu za kiume, na vyakula salama vya kuongeza nguvu za kiume
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea matunda yenye vitamin C kwa wingi
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kitunguu thaumu
Soma Zaidi...Kitunguu saumu ni tiba mbadala ya presha yabkushuja. Hakitatui tatizo yaani hakiponyeshi, ila husaidia katika kushusha presha iliyo panda.
Soma Zaidi...