12.Nyanya
Tomato tumezoea huliwa katika mboga, ila pia unaweza kuila bichi ila sio jambo zuri hususan uangalizi unahitajika. Tomato zimetaja na wataalamu wa Afya kuwa na faida nyingi. Tomato huweza kupunguza hatari ya kupata saratani na pia hupunguza athari za kisukari.

Ndani ya tomato kuna aina za carotenoid kama vile: lutein na lycopene. Hizi husaidia katika kuimarisha afya ya macho. Au kupunguza athari zinazotokana na mwanga zisidhuru macho. Tomato ni katika matunda ambayo yauwezo mkubwa wa kulinda mwili dhidi ya maradhi. Pia huweza kuuwa seli za saratani.

Tomato zina vitamini C kwa wingi. Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa vitamini hivi vina kazi kubwa ya kulinda mwili na maradhi mbalimbali. Pia vitamini hivi vinakazi ya kuzuia utengenezwaji wa seli bila ya mpangilio yaani seli za saratani.

Tomato huweza kupunguza presha kwa wale wenye tatizo la kupanda kwa presha yaani shinikizo la damu. Wataalamu wanaeleza kuwa kutumia kudhibiti kiwango cha sodium yaani madini ya sodiam hali hii husaidia katika kurekebisha shinikizi la damu.