Okoa afya yako kwa kula tunda papai, kwa hakika hutajuta, papai lina virutubisho vingi
11.Papai (papaya)
Papai ni katika matunda yanayoingiza afya sana kwenye mwili wa binadamu. Papai lina vitamin C na vitamini A kwa wingi pia kuna potassium na folate. Pia tafiti zinaonesha kuwa antioxidant aina ya lycopene iliyomo kwenye papai husaidia katika kuzuia kupata saratani.
Pia papai lina vitamin B, vitamin E na vitamin K. Pia lina madini ya calsium (kashiam) potassium, mgnessium na copper. Pia punje za papai ni dawa kwa baadhi ya matatizo ya ini na figo. Pia kwenye papai kuna protelytic enzymes hawa husaidia katika kuuwa bakteria na minyoo pamoja na wadudu wengine hatari ndani ya tumbo (mfumo wa kum eng’enya chakula).
Papai linatambulika kwa kuwa na uwezo wa kuulinda mwili na maradhi ya uzee kama macho, misuli na kuzeheka kwa haraka. Ndani ya papai kuna Zeaxanthin hii ni anti oxidant ambayo inakazi ya kuchija miale hatari ya jua. Pa inaaminika kuwa antioxidant hizi husaidia katika afya ya macho na husaidia katika kudhibiti kudhoofu kwa misuli.
Papai huaminika kusaidia kupunguza hatari ya kuwa na ugonjwa wa pumu. Hupunguza hatari ya kuuguwa pumu. Ndani ya papai kuna virutubisho vingi, lakini uwepo wa beta-carotene ndani ya papai husaidia kwa wagonjwa wenye pumu.
Ulaji wa antioxidanti zilizopo kwenye papai kama beta-carotene husaidia katika kupunguza athari za kupata maradhi ya saratan kwa vijana. Ulaji wa tunda hili husaidia katika kudhibiti upatikanaji wa saratani ya kwenye via vya uzazi hasa saratani ya korodani.
Papai ni katika matunda yenye vitamini K ambavyo ni muhimu katika afya ya mifupa. Hivyo ulaji wa tunda hili husaidia katika kuimarisha afya ya mifupa na kudhibiti kupasuka kwa mifupa. Vitamin k pia husaidia katika ufyonzwaji wa madini ya calcium na huzuia upotevu wa madini haya kupitia mkojo. Kupuka madini haya pia ni muhimu katika kuimarisha na kudhibiti afya ya mifupa.
Tafiti za kisayansi zinaonesha kuwa papai n I tunda zuri kwa wenye kisukari. Papai ni katika vyakula vya kambakamba ambacho kina maji kwa wingi. Tafiti zinaonesha kuwa watu wenye kisukari type 1 diabetes wameweza kupunguza kiwango cha sukari mwilini mwao. Wakati huohuo watu wenye kisukari type 2 diabetes wameweza kuimarisha kiwango cha sukari mwilini pamoja na kiwango cha homoni ya insulin.
Ndani ya papai kuna enzyme zinazoitwa papain hizi husaidia katika mmeng’enyo wa chakula. Pia kama tulivyo sema papai lina maji nmengi na kambakamba vyote kwa pamoja husaidia katika upatikanaji wa choo na kusaidia katika kudhibiti mmeng’enyo wa chakula.
Madini ya potassium (aina ya chumvi) na vitamini vilivyomo kwenye papai husaidia katika kulinda afya ya moyo dhidi ya maradhi hatari yanayoshambulia mfumo wa usukumwaji wa damu. Ulaji wa madini haya wakati huohuo ukiwa unapunguza ulaji wa ma\dini ya sodium (chumvi hii tunayotumia) husaidia katika kuulinda moyo dhidi ya maradhi hatari kama shambulio la moyo, presha na kiharusi (stroke).
Ndani ya papai kuna madini ya Choline, haya ni muhimu katika kusaidia miili yetu hasa kulala, kujongea kwa misuli (kukunja na kukunjuka, kutanuka na kusinjaa). pia husaidia katika kulinda mpangiliuo wa utando wa seli, husaidia katika kutunza kumbukumbu pamoja na kujifunza yaani kusoma. Pia husaidia katika ufyonzwaji wa fati (mafuta).
Kwa ufupi papai lina matumizi mengi sana kama ukuaji wa nywele na kuzifanya zing’ae, kupona kwa vidonda, ukuaji wa tishu na ukuaji wa mwili kwa ujumla. Na haya yote ni kutokana na kuwepo kwa vitamin c na vitamin A
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
Posti hii inahusu zaidi mabadiliko ya matiti yanayopaswa kutolewa taarifa mapema, kwa sababu ya kuwepo kwa saratani ya matiti, kuna dalili ambazo zikijitokeza zinapaswa kutolewa taarifa mara moja bila kuchelewa kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Ukosefu wa madini ya Shaba mwilini, ni Ukosefu wa madini ya Shaba mwilini ambao usababisha madhara kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea faida za embe na umuhimu wake kiafya
Soma Zaidi...Umeshawahi kula karoti mbichi, ama ya kupikwa, je unazijuwa faida zake? soma makala hii
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na Faida ambazo anaweza kupata mwanadamu Kama akila bamia Mara kwa mara. Bamia huliwa Kama tunda au Kama mboga pia na husaidia vitu vingi mwilini.
Soma Zaidi...Uyoga pia ni katika vyakula vya asili, ijapokuwa upatikanaji wake umekuwa mchache siku hizi. Shukrani ziwaendee wataalamu wa kilimo, kwa sasa tunaweza kuzipata mbegu za uyoga kutoka maabara na kulima uyoga popote pale. Wataalamu wa mimea wanaamini kuwa uy
Soma Zaidi...