picha

ijuwe namna ya kufanya ihram na Vazi la ihram

ijuwe namna ya kufanya ihram na Vazi la ihram

Ihram



Mwenye kunuia Hija au ‘Umra katika Miiqaat anakuwa katika hali ya kuchunga masharti kadhaa mpaka akamilishe matendo kadhaa ya Hija au ‘Umra. Hali hii ya kuchunga masharti hujulikana kwa jina la “Ihram ”.



Wanaume wanapokuwa katika Ihram hulazimika kuvaa vazi rasmi la Ihram.Vazi la Ihram kwa wanaume ni kuvaa shuka mbili nyeupe zisizo shonwa.Shuka moja hufungwa kiunoni na mkanda huweza kutumika ili kuhakikisha isivuke. Shuka la pili huvaliwa lubega kwa kufunika bega la kulia na kuacha wazi bega la kushoto. Katika hali ya Ihram, ni haram kwa mwanamume kuvaa nguo nyingine yoyote, ni haramu kufunika kichwa, ni haram kuvaa soksi au kuvaa viatu vinavyofunika miguu.



Wanawake hawana vazi rasmi la Ihram. Akiwa katika Ihram Hajat analazimika kama kawaida kujifunika mwili wake wote isipokuwa uso na viganja vya mikono na atavalia ushungi. Hijab yaweza kuwa ya rangi yoyote isiyovutia kama kawaida ya vazi la mwanamke wa Kiislamu lakini vazi jeupe ni bora. Mwanamke akiwa katika Ihram ni haramu kufunika uso au kuvaa soksi za mikononi(gloves). Pia wanawake katika Ihram hawaruhusiwi kuvaa soksi wala kuvaa viatu vinavyofunika miguu.



Yaliyoharamishwa kwa Mwenye kuwa katika Ihram
(i)Kujimai (kufanya tendo la ndoa) au kubusu au kukumbatiana au kufanya vitendo vingine vya kimapenzi kati ya mume na mke ambavyo vitawaletea fikra za kufanya ten do la ndoa.
(ii)Kusema maneno maovu na machafu kama vile kusengenya,kugombana, kugombanisha, kusema uwongo, kubishana, n.k. Na anayekusudia kufanya Hija katika (miezi) hiyo basi asiseme maneno machafu wala asifanye vitendo vichafu wala asibishane katika hiyo Hija ... (2:197).
(iv) Kunyoa au kung’oa nywele, kukata kucha au kukata au kupunguza sehemu yoyote ya mwili ila kwa matibabu kama vile kuumika, kutolewa damu kwa ajili ya matibabu na mengineyo.
(vi)Kuoa au kufanya mipango ya ndoa au hata kupeleka posa.
(vii)Kujipaka manukato
(viii)Kuvaa nguo ya rangi yenye kuvutia
(ix)Kwa wanaume kuvaa nguo iliyoshonwa, na kufunika kichwa.
(x)Kwa wanawake kufunika uso na kufunika viganja vya mikono kwa kuvaa glovu (gloves).
(xi)Kuvaa viatu vinavyofunika miguu na kuvaa soksi.
(xii)Kuwinda au kusaidia kuwinda angalau kwa kuonyesha mnyama anayewindwa.
(xiii)Kula nyama iliyowindwa au iliyopatikana kwa msaada wa mtu aliyekuwa katika Ihram.
(xiv)Kula mayai ya ndege waliopatikana kwa kuwindwa.




                   


Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Vyakula Main: Post File: Download PDF Views 2535

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 ai web app     👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    

Post zinazofanana:

Mafidodo (mafindofindo) au tonsils kweye koo je inaweza ikawa Ni moja kati ya dalil za ukimwi

Tezi za lymph huanza kuonyesha dalili za kuwa mwili upo katika mapambano dhidi ya vijidudu vya maradhi. Ishara ni pale utakapoona tezi za lymph zina maumivu. Tezi hizi hupatikana kwenye mapaja, kwapa nashingo.

Soma Zaidi...
Tango (cucumber)

Somo hili linakwenda kukuletea faida za kiafya za kula tango

Soma Zaidi...
VYAKULA VYA MADINI

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
Faida (matunda) ya kusimamisha swala katika jamii

Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...