Imam Muhammad Idris al-Shafii
Imam Shafii alizaliwa mwaka (150 A.D.) huko Gaza katika ukanda wa Pwani ya bahari ya Meditteranean. Yeye ni wa kabila la Quraysh. Akiwa bado kijana, Imam Shafii alihifadhi Qur’an na Kitabu cha Imam Malik, al-Muwata. Alisoma elimu ya sheria ya Kiislamu toka kwa mwanachuoni mashuhuri na Mufti wa Makka Muslim bin Khalid al-Zanji. Baada ya kifo cha Khalid, alikwenda Madinah ambapo alisoma kwa Imam Malik bin Anas. Wakati Imam Malik anafariki tayari Imam Shafii alikuwa ashavuma ndani ya Arabuni na kwingineko kwa ujuzi wake wa elimu ya sheria na Uislamu kwa ujumla.
Kutokana na elimu na uadilifu wake, Imam Shafii aliteuliwa kufanya kazi Serikalini. Hata hivyo hakudumu kwani kwa uadilifu na utendaji wake wa kazi kwa haki aligongana na wakuu wa Serikali wasiotaka haki. Alikamatwa na kuhamishiwa Iraq akiwa amefungwa minyororo kwa tuhuma kuwa anafanya uchochezi dhidi ya Serikali. Huo ulikuwa mwaka 187 A.H. (803 A.D.) wakati wa utawala wa Harun al-Rashid. Baadae aliachiwa huru kwa kuonekana hana hatia. Alibaki kwa muda Baghdad akisoma chini ya wanafunzi wa Imam Abu Hanifah. Alifanya kazi ya kudarasisha Makka na akapata wasikilizaji wengi akiwemo Imam Ahmad bin Hambal ambaye wakati huo alikuwa anasoma Makka. Pamoja na kuwa alikuwa na maoni ya kifiqh tofauti na yale ya Imam Malik na Abu Hanafi, aliwaheshimu na kuthamini juhudi na michango yao. Hakujenga kundi la Shafii dhidi ya Maimamu wengine kama ambavyo baadhi ya Masheikh hufanya hivi leo.
Maimamu ambao tunajinasibisha nao hivi leo wao walikuwa wamoja katika Uislamu. Pale walipokuwa na maoni tofauti katika ufahamu wa baadhi ya mambo walikubaliana kutofautiana, wakazikubali tofauti zao, lakini walibaki kuwa wamoja walioshikamana katika kamba (dini) ya Allah(s.w).
Kazi kubwa ya kufundisha na uandishi, Imam Shafii aliifanyia Misri katika mji wa Cairo ya leo. Huko alizungukwa na wanafunzi na wanachuoni toka sehemu mbalimbali. Walijifunza na kuandika kila alichosema. Imam Shafii alikuwa na kawaida ya kuwaamrisha wanafunzi wake kusoma kwa sauti kila walichoandika ili apate kusahihisha. Kazi kubwa muhimu za Imam Shafii ambazo zinaendelea kutoa mchango mkubwa katika elimu ya Fiqh na sheria ya Kiislamu mpaka hivi leo ni Kitab al-Umm na Kitab al- Risalah Fi-Usul-al Fiqh (al-Risalah). Imam Shafii alifariki na kuzikwa Cairo mwezi Rajabu mwaka 204 A.H/20/1/820 A.D.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
LAKINI UMRI WANGU MKUBWABaada ya kuwaza na kufikiri muda mrefu, bibi Khadija (Radhiya Llahu anha) akafikia uamuzi wa kutaka kuolewa na Muhammad (Swalla Laahu alayhi wa sallam).
Soma Zaidi...(i) Tuanze kulingania kwa Tawhiid – kumjua Allah(s.
Soma Zaidi...Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...(i) Suratul- ‘Alaq (96:1-5)“Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba Aliyemuumba mwanaadamu kwa ‘alaq.
Soma Zaidi...Kutokana na kisa cha Nabii Shu’ayb(a.
Soma Zaidi...Makafiri wa Kiquraish walikuwa na tabia ya kumghasi Mtume(s.
Soma Zaidi...