Menu



Historia ya Dhulqarnain

Dhulqarnain sio jina la mtu bali cheo, maana yake ikiwa: “Mwenye Pembe Mbili”.

Historia ya Dhulqarnain

Historia ya Dhulqarnain


Dhulqarnain sio jina la mtu bali cheo, maana yake ikiwa: “Mwenye Pembe Mbili”. Qur’an haibainishi Dhulqarnain aliishi wapi na wakati gani wa historia. Lakini kwa vile habari zake zinasimuliwa ndani ya Qur’an kama jibu la Mtume(s.a.w) kwa Maquraish kutokana na swali walilopewa na Mayahudi wamwulize Mtume; ni dhahiri kuwa:

(a) Dhulqarnain aliishi miaka mingi kabla ya Mtume (s.a.w).
(b) Historia yake haikuwa inafahimika Arabuni.
(c) Mayahudi walikuwa wakifahamu historia yake.



Wafasiri wengi wa Qur’an na watu wa historia wanamtaja Dhulqarnain kuwa ni mmoja wa wafalme wa Kifursi ambaye aliuangusha ufalme wa Babylon na kuwafanya Waisrail wawe huru. Hii ilitokea kiasi cha maika 1000 kabla ya Mtume(s.a.w). Akiitwa Dhulqarnain (Mwenye Pembe Mbili) kwa vile nchi aliyokuwa anatawala ilikuwa ni nchi mbili zilizoungana na kufanya umbo la Pembe Mbili. Dhulqarnain alikuwa mtawala mwenye nguvu lakini muadilifu pia. Aidha Mwenyezi Mungu alimneemesha kwa kumpa njia za kupatia kila kitu.

“Sisi Tulimmakinisha katika ardhi na Tukampa njia za kupatia kila kitu” (18:84).



Kwa uwezo aliopewa Dhulqarnain alipanua ufalme wake toka Magharibi kuelekea Mashariki na Kaskazini na Kusini. Haya yametajwa katika Qur’an kwa lugha ya Ishara kuwa alisafiri nchi za Maghabribi, Mashariki n.k. Rejea Qur’an (18:83-93).




Basi akafuata njia. Mpaka alipofika machweo ya jua. (Nchi za Magharibi) aliliona linatua katika chemchem (ziwa) yenye matope mengi. Na pale akawakuta watu. Tukasema: “Ewe Dhulqarnain waadhibu au wafanyie wema”. Akasema: “Ama anayedhulumu basi tutamuadhibu, kisha atarudishwa kwa Mola wake, naye atamuadhibu adhabu mbaya kabisa”. Na yule mwenye kuamini na kufanya vitendo vizuri, atapata ujira mwema, nasi tutamwambia (tutamfanyia) lililo jepesi katika amri yetu” (18:85-88).



Uadilifu na wema wa Dhulqarnain unaonekana pia pale alipowakuta watu wanaovamiwa na kuonewa na watu wa makabila mengine. Katika Asia ya Kati yalikuwepo makabila yaliyojulikana kama Tartus, Mongolis, Huns na Scythians. Katika hawa baadhi yao ndio waliotajwa kama Yaajuju na Maajuju. Hawa walikuwa wakizivamia baadhi ya tawala na kuleta uharibifu.



Raia wa tawala hizo walimuomba Dhulqarnain awajengee ukuta kuzunguka nchi hizo ili iwe kinga kuwazuia Yaajuju na Maajuju wasiwavamie. Japo walipendekeza wampe ujira Dhulqarnain kwa kazi hiyo, lakini Dhulqarnain hakutaka malipo. Aliwasaidia bure kwa kutaraji malipo bora zaidi kutoka kwa Allah(s.w). Rejea kisa hiki katika aya zifuatazo:



Wakasema: “Ewe Dhulqarnain! Hakika Yaajuju na Maajuju wanafanya uharibifu katika ardhi. Basi je; tukupe ujira ili utie baina yetu na baina yao kizuizi?” Akasema” Yale ambayo Mola wangu amenimakinishia (amenipa) ni bora (kuliko ujira wenu). Lakini nisaidieni kwa nguvu (kazi). Nitaweka baina yenu na baina yao kizuizi imara”. “Nileteeni vipande vya chuma”. Hata alipoijaza (kwa hicho chuma) nafasi iliyo katikati ya milima miwili alisema: “Pulizeni (moto)” mpaka alipokifanya (kile



chuma) kuwa (kama) moto alisema: “Nileteeni shaba iliyoyayuka niimwage juu yake”. Basi (Yaajuju na Maajuju) hawakuweza kuukwea wala hawakuweza kuutoboa”.
Akasema: “Hii ni rehema itokayo kwa Mola wangu”. Na itakapofika ahadi ya Mola wangu, atauvunjavunja. Na ahadi ya Mola wangu ni kweli tu” (18:94-98).



Katika juhudi za Maquraish kumpinga Mtume(s.a.w) walikuwa wakichukua maswali kutoka kwa Mayahudi na kumuuliza Mtume. Lengo likiwa kupata kisingizio cha kumkana endapo atashindwa kujibu kwa usahihi. Moja ya maswali waliyomuliza ni kutaka kujua juu ya Dhulqarnain.



“Na wanakuuliza habari za Dhulqarnain. Waambie
“Nitakusomeeni baadhi ya hadithi yake” (18:83).



Jawabu la Mtume halikuishia kuelezea tu kuwa Dhulqarnain alikuwa mfalme katika zama fulani. Lakini zilimbainisha kama mtu aliyekuwa Mcha-Mungu na Muadilifu. Mfalme aliyenemeshwa kwa mali na nguvu kubwa na juu ya hayo hakutakabari. Bali akawa anamkumbuka Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo maelezo ya Mtume(s.a.w) yakawa yanawaongezea Maquraish ujumbe wa Tawhiid.



Katika zama zetu za leo watawala walio wengi nguvu za kisiasa na kiuchumi walizo nazo, imekuwa ndio sababu ya wao kutakabari na kufanya ufisadi katika ardhi.



Nchi kama Marekani leo hii inaonekana ndio taifa lenye nguvu
– “Super Power”, lakini kwa vile limejengwa katika misingi ya kikafiri na ushirikina, viongozi wake wameshindwa kuwa waadilifu kwa amana waliyopewa. Pale wanapotetea maslahi yao ya kidunia hutumia maguvu yao kumwaga damu za watu na kuharibu mali za wengine kwa dhulma. Lakini hawapo tayari kutetea haki ya



mnyonge kama kufanya hivyo hakuna maslahi kwao. Ni tofauti na Dhulqarnain alivyotumia maguvu yake kuwakinga watu walioishi katikati ya milima miwili wasishambuliwe na Yaajuju na Maajuju, bila ya malipo. Hii inatufikisha kwenye fundisho la msingi kuwa, amani, utulivu na utengamano katika jamii, hauwezi kupatikana kwa watu wote bila ya watu kumtambua Muumba wao na kuishi kufuatana na Mwongozo wake.



                   

Download app yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download

Download Now Bongoclass

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu image Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Views 1306


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Watu waliovunja amri ya kuheshimu siku ya Jumamosi.
Katika zama za kale Mayahudi walikatazwa kufanya kazi siku ya Jumamosi. Soma Zaidi...

Waliomshambulia na kumuuwa Ali, makhawariji na si muawiya
Soma Zaidi...

Musa(a.s)Kupewa Utume Rasmi
Musa alipotimiza muda, alifunga safari na ahali zake kurejea Misri. Soma Zaidi...

Vitimbi vya Makafiri Dhidi ya Nabii Salih(a.s) na Waumini na kuangamizwa kwao
Makafiri wa Kithamud hawakuishia tu kwenye kuukataa ujumbe wa Nabii Salih(a. Soma Zaidi...

Wapinzani wa Ujumbe wa Nabii Salih(a.s)
Baada ya Nabii Salih(a. Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Hud(a.s)
(i) Tuanze kulingania kwa kuonesha upweke wa Allah(s. Soma Zaidi...

Kufunguliwa Yusufu(a.s) Kutoka Gerezani
Yusufu(a. Soma Zaidi...

CHANZO CHA VITA VYA VITA VYA AL-FIJAR NA ATHARI ZAKE
MAPIGANO YA AL-FIJAR (MAPIGANO YA UOVU). Soma Zaidi...

Mafunzo yatokanayo na maandalizi ya mtume ki-wahay
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Historia ya Dhana ya Kudhibiti Uzazi
Soma Zaidi...