Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Bani Israil
Kutokana na historia ya Bani Israil (Mayahudi) tunapata mafunzo ya msingi yafuatayo:
(i) Baada ya Mayahudi kufanya makosa hayo yaliyoainishwa walighadhibikiwa na Allah(s.w) na kunyang'anywa hadhi yao
ya kuwa Taifa teule na kupewa Waumini wa Ummat Muhammad(s.a.w) kama inavyoainishwa katika Qur'an:
Nyinyi ndio Umma bora kuliko umma zote zilizodhihirishiwa watu (ulimwenguni) - mnaamrisha yaliyo mema na mnakataza yaliyo maovu, na mnamwamini Mwenyezi Mungu. Na kama wale waliopewa Kitabu wangaliamini (kama walivyoamrishwa) ingalikuwa bora kwao. (Lakini) miongoni mwao wako wanaoamini; na wengi wao wanatoka katika taa ya Mwenyezi Mungu' (3:110).
(ii) Cheo cha kuwa bora walichopewa Waumini kina masharti yale yale ya kusimamisha ufalme wa Allah(s.w) hapa ulimwenguni na kuwa kiigizo chema.
"Na vivyo hivyo Tumekufanyeni Ummah bora (kama Qibla chenu Tulivyokifanya bora) ili muwe mashahidi juu ya watu na Mtume awe shahidi juu yenu.........” (2:143).
(iii) Waislamu wa Ummah huu na wao hawatasalimika na ghadhabu pamoja na laana ya Allah(s.w) endapo wataiga mwenendo wa Mayahudi na kurudia makosa yao yaliyoorodheshwa hapo juu na mengineyo yaliyoainishwa katika Qur'an.
Umeionaje Makala hii.. ?
Luqman ni katika watu wema kabisa waliopita zama za nyuma.
Soma Zaidi...NASABA YA MTUME (S.
Soma Zaidi...Kama ilivyokuwa katika kaumu zilizotangulia, waliomuamini Shu’ayb(a.
Soma Zaidi...Maryam akamtwaa mwanawe, akaenda naye kwa jamaa zake amembeba.
Soma Zaidi...