Mambo yenye kufunguza swaumu (funga)
Mambo yenye kufunguza Swaumu:
Huharibika funga kwa kuvunja nguzo ya funga pamoja na sharti zake. Haya yenye kubatilisha funga yamegawanyika katika makundi makuu mawili nayo ni:-
1.yenye kubatilisha funga na kulazimika kulipa nayo ni;-
A)kula na kunya kwa makusudi. Mtu aliyekula au kunywa kwa kusahau funga yake haita haribika. Amesema Mtume (s.a.w): mwenye kusahau na hali ya kuwa amefunga, na akala na kunywa na aendelee na funga yake kwani hakika Allah amemlisha. (Bukhari na Muslim). Mwenye kula au kunywa kwa makusudi atakujalipa funga hii.
B)Kujitapishwa kwa makusudi. Amesema Mtume (s.a.w): mwenye kutapika hana haja ya kulipa funga ila mwenye kujitapisha kwa makusudi na alipe funga.(Tirmidh)
C)Kupatwa na hedhi
D)Kupatwa na nifasi
E)Kujitoa manii kwa makusudi (punyeto)
F)Kukusudia kuvuja funga yaani kukusudia kuftari.
G)Kutoka kwenye uislamu.
2.yenye kubatilisha funga na kulazimika kulipa pamoja na kutoa kafara
Na hapa ni jambo moja tu nalo ni kufanya jimai. Amesimulia Abuu hurairah kuwa wakati tulipokuwa tumekaa na Mtume (s.a.w) ghafla akaja Mtu mmoja na akamwambia Mtume (s.a.w) ewe mtume nimeangamia Mtume akamuuliza una nini akajibu:nimefanya jimai na mke wangu na hali ya kuwa nimefunga. Mtume akamwambia je unae Mtumwa umuache huru, akasema sina, akamwambia:je unaweza kufunga kwa muda wa miezi miwili mfululizi? Akasema: siwezi. Akamwambia je unaweza kulisha masikini sitini? Akasema siwezi, basi pale Mtume akanyamaza. Akasema Abuu hurairah wakati tukiwa katika hali ile kukaletwa kwa mtume tende basi mtume akauliza yupo wapi aliyeuliza? Akasema nipo hapa, akamwambia chukuwa hizi tende ukatoe sadaka.…….” Hivyo kafara ya mwenye kufanya jimai ni kuacha huru mtumwa au kufunga miezi miwili mfululizo au kulisha masikini sitini. Na hukumu hii pia ni sawa na mwanamke.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 web hosting 👉2 Bongolite - Game zone - Play free game 👉3 Madrasa kiganjani 👉4 Kitabu cha Afya 👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉6 Dua za Mitume na Manabii
Post zinazofanana:
Jinsi ya kusherehekea siku ya idi katika uislamu
Uislamu umeweka taratibu maalumu za kuzifata katika kusherehekea siku ya idi.
Soma Zaidi...Jinsi ambavyo mtu anazuiliwa kurithi mali ya marehemu
Endapo mtu yupp katika orodha ya wanaotakiwa kutithi, anaweza kuzuiliwa kurithi kwa kuzingatia haya.
Soma Zaidi...Jinsi ya kutoa zakat al fitiri na umuhimu wa zakat al fitri kwa waislamu
Hapa utajifunza kuhusu zakat al fitiri, kiwango chake, watu wanaostahili kupewa na kutoa, pia umuhimu wake katika jamii.
Soma Zaidi...