4.
4.2 Sheria Katika Uislamu
? Maana ya Sheria
Kilugha: njia ya Kufuata
Kimatumizi: ni taratibu, sharti, kanuni na amri zilizowekwa kuongoza jamii.
Kazi ya Sheria katika Jamii
i. Kulinda binaadamu binafsi dhidi ya madhara mbali mbali ya mwenendo wake mbaya.
ii. Kulinda na kuhifadhi maisha ya watu na mali au rasilimali zao kutokana na kuuliwa, kujeruhiwa, kuharibiwa, kuibiwa, n.k bila sababu ya msingi.
iii. Kuhifadhi na kulinda amani na usalama katika jamii kutokana na migongano, vurugu, n.k.
iv. Kuhifadhi na kulinda maadili ya jamii kama njia ya msingi ya kumbakisha mwanaadamu katika mwenendo mema.
v. Kuweka na kupanga utaratibu wa namna ya kuendesha shughuli na maisha ya kila siku kibinafsi na kijamii.
vi. Sheria ya Kiislamu ina kazi ya kulinda na kuhifadhi misingi mitano ya mwanaadamu ambao ni; imani, uhai, akili, heshima na hadhi na mali.
Chimbuko la Sheria za Kitwaghuti
- Zimetungwa na binaadamu kwa kutumia vipawa vya akili, elimu, mila, desturi, uzoefu, mazingira na matashi ya nafsi zao.
- Katiba ndio msingi (chombo) mkuu wa sheria za Kitwaghuti ambayo hugawanya utekelezaji wake katika vyombo vikuu vitatu;
1. Bunge (Legislature) โ chombo kikuu cha kutunga sheria
2 Serikali (Executive) โ chombo kikuu cha utendaji
3 Mahakama (Judiciary) โ chombo kikuu cha kutafsiri sheria na kutoa haki.
Udhaifu wa Sheria za Kitwaghuti
- Pamoja na mwanaadamu kupewa na vipawa vya akili, ujuzi, elimu, n.k bado ana madhaifu mengi kama ifuatayo;
i. Mwanaadamu ana ujuzi wa mambo machache sana juu ya ulimwengu na yale yanayomzunguka.
Rejea Qurโan (17:85)
ii. Mwanaadamu anaathiriwa sana na matashi ya ubinafsi, uchoyo, upendeleo, chuki, n.k.
iii. Binaadamu wametofautiana mno katika fikra, uoni, vipawa, uzoefu
(mazoea).
iv. Mwanaadamu pia anaathiriwa sana na mabadiliko ya kimazingira na zama
(nyakati).
- Kutokana na mapungufu haya, usimamizi na utekelezaji wa sheria za kitwaghuti hufanywa na watu wachache (watawala) kwa ajili ya manufaa yao tu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utakwenda kujifunza maana ya twahara katika uislamu. Pia utakwenda kujifunza hukumu za twahara, aina za twahara na mambo mengineyo
Soma Zaidi...Hapa utajifunza utaratibu wa kusherekea ifil fitir. Pia utajifunza sunnah zinazoambatsns na idil fitir
Soma Zaidi...Maana ya Swala Maana ya Swala kilugha(a) Kilugha Katika lugha ya Kiarabu neno ยSwalaatย lina maana ya ยombi au ยdua.
Soma Zaidi...