Hspa utajifunza taratibu za kuonana na mchumba katika uislamu.
Ruhusa ya Wachumba Kuonana Kabla ya Ndoa
Pamoja na sifa ya ucha-Mungu na wema, tunatakiwa tuwaoe wanawake tunaowapenda kwa sura na umbo; hivyo hivyo wanawake nao wachague wanaume wanaowapenda kwa sura na umbo ili kuzidisha mapenzi na upendo baina yao katika familia. Kwa mantiki hii Mtume (s.a.w) ameruhusu wachumba kuonana kabla ya kufunga ndoa kama tunavyojifunza katika hadithi zifuatazo:
Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa mwanamume mmoja alikuja kwa Mtume (s.a.w) akasema: "Ninakusudia kumuoa mwanamke miongoni mwa answari." Akasema Mtume
(s.a.w), 'Mwangalie kwanza kwa sababu kuna dosari katika macho ya Answari." (Muslim)
Jabir (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) amesema: "Mmoja wenu atakapochumbia, na akawa na uwezo wa kumtazama yule anayemchumbia na afanye hivyo." (Bukhari na Muslim)
Pamoja na ruhusa hii, bado waislamu wanalazimika kuendelea kuzingatia mipaka ya "Hijaab", kwamba hawaruhusiwi kukaa faragha au kutembea faragha mwanamke na mwanamume wasio maharimu.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu swala ya Istikhara
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukugundisha kuhusu swala ya ijumaa taratibu zake na jinsi ya kuiiswali.
Soma Zaidi...Mwanadamu anatakiwa aishi huku akikumbuka kuwa ipo siki atakufa. Hivyo basi inatupata lujiandaa mapema kwa ajili ya kifo.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha maana ya kusimamisha swala kama inavyotumika kisheria.
Soma Zaidi...