image

Dhana ya haki na uadilifu katika uislamu

HAKI NA UADILIFU KATIKA UISLAMU.

Dhana ya haki na uadilifu katika uislamu

HAKI NA UADILIFU KATIKA UISLAMU

HAKI NA UADILIFU KATIKA UISLAMU.
1. Dhana ya Haki na Uadilifu katika Uislamu.
Maana ya Haki kwa Mtazamo wa Uislamu.
Ni muunganiko wa sheria na maadili kwa lengo na madhumuni ya kuilea jamii katika amani, furaha, udugu wa kweli na mahusiano mema kati ya wanaadamu.


Misingi ya Haki na Uadilifu katika Uislamu.
Maisha ya furaha na amani ya kweli hupatikana kwa kusimama misingi ya haki na Uadilifu katika jamii kama ifuatavyo;
i.Tawhiid.
Haki na Uadilifu wa kweli hupatikana kwa kumuamini na kumpwekesha Mwenyezi Mungu (s.w) ipasavyo katika maamrisho na makatazo yake.

ii.Utume.
Katika kumuamini na kumpwekesha Mwenyezi Mungu (s.w) ni kufuata misingi ya miongozo ya mitume wake wote kupitia vitabu vyao.

iii.Siku ya Mwisho.
Kumpwekesha Mwenyezi Mungu (s.w) katika maisha yetu ni kuzingatia kuwa kila kitendo kitahukumiwa na kulipwa kwa haki siku ya Kiyama.


Aina au migawanyo mbali mbali ya Haki katika Uislamu.
1.Haki za Allah.
2.Haki za Nafsi.
3.Haki za Viumbe na Mazingira.
4.Haki za Binadamu kwa ujumla.
5.Haki za Raia katika Dola ya Kiislamu.
6.Haki za Maadui katika Vita (mateka).

1.Haki za Mwenyezi Mungu (s.w).
Katika Uislamu haki za Mwenyezi Mungu ziko makundi mawili;
i.Haki ya Uungu.
Ni kumsifu na kumtii kwa sifa zake kama za uumbaji, umilikaji na ulezi wa viumbe vyote na ukamilifu wake tofauti na viumbe alivyoviumba.
Rejea Qur’an (45:23), (25:68), (9:31) na (31:13).

ii.Haki ya Kuabudiwa.
Ni Mwenyezi Mungu (s.w) peke yake ndiye anayestahiki kuabudiwa na viumbe vyake muda wote, na ndio lengo kuu la kuumbwa mwanaadamu.
Rejea Qur’an (51:56), (5:44), (11:25-26) na (29:16-17).

2.Haki za Nafsi.
Haki za nafsi imekokotezwa kuanzia binafsi, familia, wazazi, n.k kama ifuatavyo;
(a)Mtu Binafsi.
Haki za msingi ni chakula, makazi, malezi, elimu, mavazi, matibabu na kufanyia kazi vipaji na neema alizonazo inavyostahiki ikiwemo;


Haki ya Macho.
Ni kutazama yaliyoamrishwa na kuyaepusha na yaliyoharamishwa.
Rejea Qur’an (17:36), (41:20), (24:30-31) na (20:131).

Haki ya Masikio.
Ni kusikiliza yaliyoamrishwa na kutosikiliza yaliyoharamishwa pia.
Rejea Qur’an (8:22) na (6:25).

Haki ya Midomo na Ulimi.
Ni kula, kunywa na kuzungumza yaliyohalalishwa na sio yaliyoharamu.
Rejea Qur’an (16:114), (17:26-29), (17:53), (41:33) na (31:6).

Haki ya Mikono na Miguu.
Ni kushika na kuendea vyote vilivyoamrishwa na kuacha vilivyokatazwa.
Rejea Qur’an (25:72) na (31:18).

(b) Haki za Familia.
Ni kusimamia malezi, elimu, uadilifu na wajibu wa kila mmoja katika familia kwa muongozo wa Qur’an na Sunnah ili kuleta kufikia lengo la kuumbwa.
Rejea Qur’an (52:21).

(c) Haki za Watoto.
Watoto wana haki ya kupata malezi na makuzi bora kulingana na mahitaji yao kwa mujibu wa mafundisho ya Qur’an na Sunnah katika sehemu zifuatazo;

Haki ya Uhai.
Uhai wa mtoto ni haki itokayo kwa Mwenyezi Mungu (s.w) kupitia malezi na makuzi ya wazazi.

Haki ya Nasaba.
Mtoto kupata nasaba ni haki kisheria ili kuwa mwanafamilia halali.
Rejea Qur’an (33:4).

Haki ya Makuzi na Malezi bora.
Makuzi na malezi bora ya mtoto ni kupata haki zake za msingi na elimu inayomuwezesha kumuabudu Mwenyezi Mungu (s.w) ipasavyo.
Rejea Qur’an (66:6).

(d) Haki za Wazazi.
Ni kuwahurumia, kuwaheshimu, kuwafanyia wema, kuwahudumia na kuwalea ipasavyo.
Rejea Qur’an (31:14), (17:23-24), (4:36), (6:151), (19:14) na (19:32).

(e) Haki za Jamaa na Majirani.
Ni kutunza uhusiano na kusaidiana pale inapohitajika kwa kuzingatia mipaka.
Rejea Qur’an (2:215).

(f) Haki za Mayatima, Wajane na Masikini.
Ni kuwahifadhi na kuwasaidia wanapokuwa na shida na mahitaji ya kimaisha.
Rejea Qur’an (2:220), (4:2), (4:10), (2:262) na (2:267).

(g) Haki za Udugu wa Kiimani na za Watu wengine.
Udugu wa kiimani ni haki na bora zaidi kuliko udugu wa damu au nasaba.
Rejea Qur’an (49:10), (49:13), (7:172-173), (4:7) na (5:8).

3.Haki za Viumbe na Mazingira.
Uislamu umeweka kipaumbele katika kuhifadhi mazingira na kutunza viumbe hai na visivyo hai kupitia sera mbali mbali zikiwemo;
?Haki ya Hifadhi ya Mazingira na misitu.
Rejea Qur’an (6:38), (27:60), (16:10-13), (50:7-9), (56:63-64) na (39:62).

Mazingira ni amana katika kulinda uhai wetu na wa viumbe wengine.
Rejea Qur’an (7:10) na (16:112).

Sera na Mafundisho ya Mtume (s.a.w) juu ya hifadhi ya mazingira katika kuleta ustawi wa jamii.

Sera ya mapinduzi ya kitabia katika kutunza na kuhifadhi mazingira yote yanayotuzunguka.

Sera ya usafi na uhifadhi wa mazingira ili kuleta ustawi wa viumbe hai.
Rejea Qur’an (6:141) na (25:2).

4.Haki za Binaadamu kwa Ujumla (Basic Human Rights).
Uislamu umezingatia, kulinda na kusimamia haki za msingi za kibinaadamu bila kujali tofauti zao. Haki hizo ni pamoja na;
1. Haki za kuishi (maisha).
Rejea Qur’an (5:32), (6:151) na (17:33).

2. Haki ya Usalama wa Maisha.
Rejea Qur’an (5:32).

3. Haki ya kulinda na kuheshimu hadhi na usafi wa mwanamke.
Rejea Qur’an (17:32) na (24:2).

4. Haki ya kupata mahitaji ya lazima ya maisha.
Rejea Qur’an (70:24-25).

5. Haki ya Uadilifu na Usawa katika Hukumu (Righ to justice).
Rejea Qur’an (5:8), (49:13) na (4:135).

6. Haki ya Uhuru (kila mtu kuwa huru).
Uislamu umezingatia kila mtu kuwa huru kifikra na kutomilikiwa kama bidhaa ya baishara.

5.Haki za Raia katika Dola ya Kiislamu.
1. Haki za msingi za raia waislamu na wasiokuwa waislamu katika Dola ya Kiislamu ni pamoja na;
2. Haki ya kuendesha maisha binafsi bila kuingiliwa na mtu yeyote.
3. Haki na uhuru wa kutoa maoni na kuamrisha mema na kukataza mabaya.
Rejea Qur’an (3:104), (9:71), (9:67).

4. Haki na Uhuru katika kufuata na kuabudu dini yeyote aipendayo mtu.
Rejea Qur’an (2:256), (6:108), (29:46) na (16:125).

5. Haki ya Kuwashtaki Viongozi wa juu wa Dola bila upendeleo na ubaguzi wowote.
6. Haki ya kumiliki mali au rasilimali zozote za halali na zisizoleta madhara kwa raia na Dola kwa ujumla.
Rejea Qur’an (2:262), (2:267) na (18:32-43).


6.Haki za Maadui Katika Vita (mateka wa Kivita).
Uislamu unajali, kusimamia na kulinda haki ya kila mtu hata kwa maadui waliokamatwa katika vita (mateka) walifanyiwa haki na uadilifu kama ifuatavyo;

1. Kuhurumiwa na kutofanyiwa ukatili wowote maadamu wamedhibitiwa.
2. Kuwapa mahitaji yao ya lazima ya kibinaadamu na kimaisha pia.
3. Kulinda uhai na usalama wa maisha yao mpaka mwisho wa uhasama.
4. Mateka wa kivita walikuwa na haki ya kujikomboa kwa njia zifuatazo;
5. Kulipa kiasi fulani cha pesa au mali yeyote inayokubalika.
6. Kubadilishana na mateka Waislamu waliokamatwa na maadui.
7. Kulipa fidia kwa kufanya jambo fulani lenye manufaa kwa jamii ya waislamu.
Rejea Qur’an (47:4).

Masuria na mateka wanawake walikuwa na haki ya kulindwa na kuhifadhiwa kwa kupewa wanaume waliokwenda vitani na kuishi nao katika maisha ya ndoa ili kupata mahitaji yao ya msingi.

Haki ya kumiliki mali au uchumi ulio wa halali na usio leta madhara yeyote katika Dola ya Kiislamu.                              

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 443


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Hii ndio hutuba ya ndoa ya kiislamu
Hapa utajifunza utaratibu wa hutuba ya ndoa ya kiislamu. Sharti za jutuba ya ndoa na jinsibya kuozesha Soma Zaidi...

Funga za Sunnah na umuhimu wake
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Umuhimu wa uchumi katika uislamu
2. Soma Zaidi...

Namna ya kutambuwa kibla na umuhimu wa kuelekea kibla wakati wa kuswali
4. Soma Zaidi...

Ni zipi funga za suna, na faida na fadhila zake pamoja na wakati wake wa kufunga
Soma Zaidi...

Funga ya ramadhan na nyinginezo
Nguzo za uislamu (EDK form 2; dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

MTAZAMO NA HUKUMU YA KUPANGA UZAZI WA MPANGO KWENYE UISLAMU
Atika uislamu swala la kupanga uzazi linaruhusiwa endapo kutakuwa na sababu maalumu za kisheria. Soma Zaidi...

Sera ya uchumi katika Uislamu
4. Soma Zaidi...

Njia haramu za uchumi.
Njia hizi ni haramu katika kukuza uchumi wako. Soma Zaidi...

Swala ya tarawehe jinsi ya kuiswali
Post hii itakwenda kukufundisha kuhusi swala ya tarawehe, faida zake na jinsi ya kuiswali. Soma Zaidi...

Namna ya kutayamamu hatuwa kwa hatuwa
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu jinsi yavkutayamamu. Soma Zaidi...

Hekma katika hukumu za mirathi katika uislamu, na ni kwa nini wanaume wanazidi katika kurithi katika uislamu
Soma Zaidi...