Mambo yanayopelekea Mjamzito kutokwa na damu

Posti hii inahusu zaidi mambo mbalimbali ambayo yanapelekea Mjamzito kutokwa na damu, hizi ni baadhi ya sababu ambazo usababisha Mjamzito kutokwa na damu.

Mambo yanayopelekea Mjamzito kutokwa na damu.

1. Mimba kutishia kutoka au kuharibika kabla ya kujifungua.

Kuna wakati mwingine Kuna tatizo la mimba kuharibika au kutishia kutoka ni lazima damu inatoka kwa sababu Kuna baadhi ya maambukizi ambayo yanakuwepo kwenye via vya uzazi ambayo usababisha mimba kuharibika au kutishia kutoka, na pia damu utoka kwa sababu baadhi ya mishipa ya damu ambayo inakuwa imeshikilia mtoto uachia na kusababisha damu kutoka , ila mimba inayotishia kutoka mama akiwahi hospital upewa matibabu mapema na mimba urudia kwenye hali yake ya kawaida.

 

2. Pia damu  utoka wakati wa ujauzito kwa sababu kondo la nyuma linapotaka kujishikiza kwenye mji wa uzazi usababisha kupelekea damu kutoka wakati wa ujauzito ila kwa kawaida damu hiyo huwa ni ndogo na utokea kwa mda mfupi tu na kutoweka, hali hii uwapata hasa hasa akina Mama kwenye mimba za kwanza ambapo kwa kitaalamu huitwa prime gravida, kwa hiyo hii ni hali ya kawaida kabisa na Haina madhara yoyote kwa mama , kwa sababu hili kondo lenyewe ndilo baadae uja kusaidia mtoto kwa chakula na vitu vingine vingi wakati mtoto akiwa tumboni.

 

3. Mimba kutungwa nje ya mfuko wa uzazi.

Kuna wakati mwingine mimba utungwa nje ya mfuko wa uzazi mbali na sehemu yake ambapo inapaswa kutungwa, kwa hiyo mimba inaweza kutungwa kwenye sehemu mbalimbali za via vya uzazi ila kwa kiasi kikubwa utungwa kwenye mirija ya uzazi ambayo kwa kitaalamu huitwa follapian tube ni mara chache sana mimba kutungwa kwenye ovaries, kwa hiyo mimba haipaswi kabisa kutungwa hapo kwa hiyo mimba inaweza kufika mpaka kwenye wiki ya kumi na mbili, kwa hiyo kitendo cha mimba kutungwa kwenye follapian tube usababisha damu kutoka na ni vizuri kabisa kumpeleka mama hospital mapema ili kuweza kumsaidia kwa sababu hii huwa ni hatari.

 

4. Wakati mwingine damu utoka wakati wa ujauzito ni kwa sababu ambazo hazijulikani kwa sababu Kuna akina Mama wengi ambao upatwa na tatizo hili na chanzo utafutwa ila hakijulikanagi kwa hiyo ni vizuri kuwa kwenye uangalizi wa wataalamu wa afya na kuweza kuhakikisha kuwa mtoto anazaliwa Salama na Mama anakuwa salama Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/07/19/Tuesday - 06:27:19 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1369


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-