Njia za kupunguza tatizo la kutanuka kwa tezi dume.
Posti hii inahusu zaidi njia ambazo tunaweza kutumia ili kuweza kupunguza tatizo hili la kutanuka kwa tezi dume, kwa hiyo tunaweza kutumia njia zifuatazo ili kuweza kupunguza tatizo hili kwenye jamii kama ifuatavyo.
Njia za kupunguza tatizo la kuvimba kwa tezi dume.
1.Kwanza kabisa tunajua kubwa Ugonjwa huu umeweza kusambaa kwa kiasi kikubwa na kusababisha madhara kwa hiyo tunaweza kutumia njia zifuatazo ili kuweza kupunguza tatizo hili
2. Tunapaswa kula vizuri.
Kula vizuri kwa maana ya kula mchanganyiko wa vyakula sio kula chakula kimoja hata kama una uwezo wa kawaida unaweza leo kula viazi kesho ugali, siku nyingine wali na pia kutumia mboga za majani na matunda hata sio lazima kuwa na mafuta ili utumie mboga za majani au kama una uwezo kula chakula kadri ya uwezo wako maana katika vyakula tunaweza kutibu mambo mengi bila kujua.
3. Jaribu kupunguza sumu mwilini.
Kwa wakati huu tunakula sana vyakula vyenye sumu kama vile mafuta mengi kwenye chakula, vyakula vya Makopo, chips, baga na vyakula vingine vya namna hiyo na pia kuna unywaji wa pombe kali kupita kiasi na pia kutumia dawa bila ushauri wa kitaalamu , mambo hayo yote uongeza sumu mwilini kwa hiyo tunapaswa kuepuka vyakula hivyo kuvila kwa muda mrefu badala yake punnguza matumizi ya mafuta na kunywa sana maziwa.
4. Daima epukana na ngono zembe.
Kwa wakati huu kuna mlipuko wa magonjwa ya zinaa kila wakati kama vile kaswende, kisonono na mengine mengi kwa hiyo tunapaswa kutumia kondomu wakati wa kujamiiana au kutibu maambukizi ili kuweza na kuendelea kuwepo kwa kuvimba kwa tezi dume.
5. Pia wanaume wanapaswa kufanya mazoezi.
Kwa kufanya mazoezi tunaweza kuna vitu vingi tunapata kwa sababu pale mtu akitoa jasho uchafu mwingi utoka na mwili huwa huru na kutokana na mazoezi tunaweza kuepusha Magonjwa mengi tusiyotafahamu.
6. Kuepuka Matumizi ya pombe kali na sigara.
Kwa matumizi ya pombe kali na sigara usababisha viungo mbalimbali vya mwili kulegea na kutofanya kazi vizuri hali hii inaweza kusababisha maambukizi sehemu mbalimbali za mwili na mwili kuwa dhaifu hatimaye Magonjwa mengi yanaweza kutokea hata kuvimba tezi dume.
7. Kuepuka na msongo wa mawazo.
Siku hizi kuna tatizo hili la kuwa na msingi wa mawazo kwa walio wengi hali ambayo uwafanya eatu kubwa na matatizo mengi ya kiafya. Kama kuna shida yoyote shirikisha rafiki, angalia mpira, au kitu chochote unachokipenda ili mradi kupunguza mawazo.
8.Katika maisha yetu tuwe na tabia ya kuchukua vipimo kwa ajili ya kuangalia afya zetu na tabia ya kuwahi hospitali unapohisi kubwa kuna kitu ambacho hakipo sawa kwa sababu, Ugonjwa wowote kama hata hauna tiba ukiwahi hospitalini madhara yanakuwa madogo kuliko pale ukienda umechelewa,
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Simulizi za Hadithi Audio 👉2 Madrasa kiganjani 👉3 Dua za Mitume na Manabii 👉4 ai web app 👉5 web hosting 👉6 kitabu cha Simulizi
Post zinazofanana:
Zifahamu sababu za kuziba kwa mrija wa kizazi.
Posti hii inahusu zaidi sababu za kuziba kwa mrija wa kizazi ambayo kwa kitaalamu huitwa follapian tube, ni sababu ambazo ufanya mirija ya follapian tube kuziba.
Soma Zaidi...Dalili za ujauzito: Nini kinatokea kwanza
Je, unafahamu dalili za mwanzo za ujauzito? Kutoka kwa kichefuchefu hadi uchovu, ujue nini cha kutarajia.
Soma Zaidi...Kuvunjika kwa mtoto wakati wa kuzaliwa.
Post hii inahusu zaidi kuvunjika kwa mtoto wakati wa kuzaliwa, hali hii utokea kwa watoto wadogo wakati wa kuzaliwa kwa sababu maalum kama tutakavyoona.
Soma Zaidi...Tiba mbadala ya fangasi wa uumeni
Somo hili linakwenda kukuletea tiba mbadala ya fangasi wa uumeni
Soma Zaidi...Sababu za Kukoma hedhi (perimenopause)
Kukoma hedhi hufafanuliwa kuwa hutokea miezi 12 baada ya kipindi chako cha mwisho cha hedhi na huashiria mwisho wa mizunguko ya hedhi. Kukoma hedhi kunaweza kutokea katika miaka ya 40 au 50. Kukoma hedhi ni mchakato wa asili wa kibaolojia. Ingawa pia in
Soma Zaidi...Mambo ya kuzingatia kwa mama ili apate huduma endelevu.
Posti hii inazungumzia kuhusiana na huduma kwa mama wajawazito na waliojifungua.
Soma Zaidi...