Hatari ya kutokwa na damu wakati wa ujauzito

Posti hii inahusu zaidi hatari za kutokwa na damu wakati wa ujauzito, hali hii utokea wakati wa ujauzito ambapo Kuna baadhi ya wajawazito utokwa na damu jambo ambalo hatupaswi kutarajia kwa sababu tunafahamu kabisa mama akishapata ujauzito na damu zinakom

Hatari ya kupata ya kutokwa na damu wakati wa ujauzito.

1. Ikitokea mtu akapata damu kwenye kipindi cha ujauzito Kuna hatari ya mimba kuharibika na kutojifungua mtoto.kwa hiyo kama Mama ana mimba na akaona damu inatoka kawaida kama yupo kwenye siku za mwezi nai vizuri kabisa kuwahi hospital Ili kuangalia zaidi kwa sababu uenda kukatokea hatari ya mimba kuharibika kwa sababu dalili hii sio nzuri kwa mama Mjamzito.

 

2. Pia Kuna hatari ya kujifungua mtoto kabla ya wakati wake.

Na tatizo hili la kutokwa na damu wakati wa ujauzito Kuna hatari ya kujifungua mtoto kabla ya wakati wake, kwa sababu mimba ikishatungwa hakuna mfumo wowote wa urutubishaji unaotoka na mtu akatokwa na damu kama vile Hana mimba kwa hiyo kama ikitokea Mama akatokwa na damu labda inawezekana Kuna maambukizi zaidi ambayo usababisha damu kutoka na hali hiyo usababisha mtoto kuzaliwa kabla ya wakati.

 

3. Vile vile kutokwa na damu wakati wa ujauzito usababisha kuzaliwa kwa mtoto mwenye uziti wa chini.

Kwa kawaida uzito wa mtoto ni kuanzia kilo mbili na nusu mpaka kilo tatu na nusu, uzito wa mtoto ukianzia kilo tatu na nukta sita na  kuendelea hii nayo ni shida na ikitokea mtoto akazaliwa chini ya uzito wa kilo mbili na point nne ni uzito mdogo kwa hiyo Kuna sababu mbalimbali ambazo usababisha mtoto kuzaliwa akiwa na uzito mdogo ni kwa sababu ya kuwepo kwa kitendo cha kutokwa na damu wakati wa ujauzito, kwa hiyo ni vizuri kabisa kuwahi hospitals endapo tatizo hili likijitokeza Ili kuepukana na changamoto hii.

 

4. Tatizo lingine ambalo linaweza kutokea ni kupungukiwa na damu wakati wa kujifungua.

Kwa kawaida Mama akikaribia kujifungua ni vizuri kabisa kuwa na damu ya kutosha kwenye mwili Ili kuweza kujifungua salama kwa sababu wakati wa kujifungua utokea matatizo mbalimbali kama vile kumwaga damu au pengine mtoto anaweza kuwa amekaa vibaya na wakaamua kufanya upasuaji na damu umwagika kwa hiyo ni vizuri kabisa kuwepo kwa damu ya kutosha ila kwa sababu ya kuwepo kwa tatizo la kutokwa na damu wakati wa ujauzito usababisha damu kupungua mwilini.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/07/19/Tuesday - 06:02:44 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1032


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-