Posti hii inazungumzia kuhusiana na Mambo yanayoweza kuadhiri Uponyaji wa jeraha.jeraha huleta maumivu makali sana, vilevile Uvimbe, kutoa usaha. Pia jeraha hutofautiana katika kupona kwa mtu mzima na Mtoto.
Mambo Yanayoathiri Uponyaji wa Jeraha
1. Ukubwa au Kiwango cha jeraha: Jeraha dogo la juu juu hupona haraka kuliko jeraha kubwa na
majeraha ya kina zaidi.
2. Hali ya lishe: Lishe duni huchelewesha uponyaji wa jeraha na kwa watu wenye majeraha wanatakiwa kupata lishe Bora zaidi ambayo inaweza kuponesha kidonda kwa haraka.
3. Utoaji wa kiasi cha kutosha cha protini, vitamini C na kalori huharakisha uponyaji kwa Sababu huupatia mwili nguvu hivyo kupelekea sehemu penye jeraha kuwahi kupona lakini akisa protein vitamini C lazima kidonda kuchelewa kupona.
4. Mahali kidonda kilipo: Majeraha kwenye miguu na mikono au kutosafishwa kidogo hupona polepole kuliko majeraha usoni au kichwani.
5. Umri wa mgonjwa: Uponyaji ni wa haraka zaidi kwa watoto na vijana kuliko wazee na watu wazima kwa sababu tishu,Ngozi na hata mifupa ya Mtoto mdogo (viungo) Huma haijakomaa na huwahi kupona kuliko viungo vya mtu mzima.
6. Kitu kilichoingia kwenye jeraha Kama vile msubari, mwiba n.k Uponyaji hautafanyika hadi miili ya kigeni iondolewe kwenye hilo jeraha. Miili hii ya kigeni inaweza kuwa katika mfumo wa tishu zilizoharibiwa, vipande vilivyoingizwa vya mbao, na metali za mirija ya mifereji ya maji.
7. Kuvuja damu na kutokwa na damu: Hizi huongeza muda wa uponyaji kwa vile hutoa nzuri njia ya utamaduni kwa ukuaji wa viumbe vidogo.
8.Uwepo wa magonjwa mengine: Magonjwa kama vile kisukari (diabetes mellitus) huongeza muda wa kupona, majeraha yanayotokana na kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu.
8. Dawa fulani: Dawa zinazoweza kubadilisha kiwango cha uponyaji ni pamoja na dawa za kuzuia uchochezi, kama vile dawa za kukandamiza kinga na saratani.
Mwisho; Ni vyema ukipata jeraha uende kituo Cha afya ili kupata matibabu Kama vile kidonda kusafishwa, kutolewa uchafu ulioingia Ndani ya kidonda, kutolea usaha na majimaji machafu yanayoleta Uvimbe kwenye kidonda, pia matibabu hayo yatakusaidia na dactari atakupa maelekezo zaidi ya kukusaidia jeraha lako kupona.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Mtoto mdogo ni mtoto chini ya miaka mitano, yaan kuanzia pale anapozaliwa mpaka anapafikisha miaka mitano
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi faida za maji ya uvuguvugu, hasa hasa maji haya ni vizuri kabisa kuyatumia hasa wakati wa asubuhi na pia wakati tumbo likiwa halina kitu, kwa hiyo zifuatazo ni faida za maji ya uvuguvugu.
Soma Zaidi...Kama mtu anatokwa na damu za pua, basi juwa kuwa anahitaji huduma ya kwanza.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi juu ya kuhakiki kama kidonda kimepona kwa mgonjwa mwenye vidonda, kwanza kabisa tunajua kuwa vidonda uwanyima Watu raha na pengine kuwafanya wakate tamaa kama wapo hospitalini kwa hiyo tunapaswa kutumia njia zifuatazo ili kuweza ku
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu madhara ya upungufu wa protini
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu madhara ya upungufu wa vitamin
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa kutumia dawa za kujikinga na maambukizi ya ukimwi, ni faida ambazo upatikana kwa watu wanaodhani wameambukizwa na virus vya ukimwi na kuweza kujikinga.
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea kuhusiana na mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa walio na majeraha ya macho kutokana na aina mbalimbali ya jeraha
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyepaliwa
Soma Zaidi...