picha

Fahamu kuhusu michubuko kwa watoto wakati wa kuzaliwa

Post hii inahusu zaidi michubuko ambayo mara nyingi utokea kwa watoto wakati wa kuzaliwa,na mara nyingi uweza kupona baada ya masaa ishilini na manne au ndani ya masaa ishilini na manne.

Michubuko kwa watoto wakati wa kuzaliwa.

1. Kwanza kabisa tunafahamu mtoto anapozaliwa upitia sehemu mbalimbali na hatua mbalimbali Ili kuweza kutoka nje ya tumbo la uzazi la mama ,Kuna wakati mwingine kichwa cha mtoto na kiuno cha mama ambapo mtoto anapaswa kupitia huwa havilingani hali ambayo usababisha mtoto kutumia nguvu Ili kutoka nje na hivyo kusababisha michubuko kwenye kichwa cha mtoto kwa hiyo wataalamu wa afya ni vizuri kabisa kugundua  hali hizi Ili kuweza kuepuka na hali ya michubuko wakati wa mtoto kuzaliwa.

 

2. Tunaposema kuhusu michubuko sio kama Ile ya Kawaida  ya kuchubuka kwa ngozi, michubuko mingine uingia ndani ya layer za ndani hali ambayo usababisha mtoto kuvuja kwa ndani na dalili mojawapo ni mtoto kuwa na macho mekundu au kuvimba uso na wakati mwingine mtoto anakuwa analia kila unapomgusa kichwani au kumshika kwa sababu ya kutojisikia vizuri mtoto anaweza kushindwa kunyonya na pengine kukosa Raha na kulia mara kwa mara , kwa hiyo ni vizuri kabisa kwa wataalamu wa afya kugundua tatizo mapema na kufanyia utafiti Ili kuweza kuepuka madhara mengine zaidi.

 

3. Vile vile Kuna michubuko ambayo ujitokeza nje yaani mtoto anakuwa amevimba kichwani pindi anapozaliwa,hali hii utokea hasa kwa akina mama wanaojifungua kwa mara ya kwanza ,kwa sababu utumia nguvu kubwa wakati wa kusukuma na pia utumia masaa mengi wakati wa kujifungua kuliko akina mama ambao wamejifungua Zaid ya mara Moja kwa hiyo, watoto wakizaliwa hivyo kwa kawaida upona ndani ya masaa ishilini na manne na pia usafi ni lazima, kwa hiyo akina mama hawapaswi kiwa na wasiwasi endapo mtoto akiwa amepata mikwaruzo kwenye kichwa ambayo uonekana kama uvimbe.

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2023/03/16/Thursday - 08:47:48 am Topic: Huduma Main: Afya File: Download PDF Views 1959

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 web hosting    👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉3 Simulizi za Hadithi Audio    👉4 kitabu cha Simulizi    👉5 Dua za Mitume na Manabii    👉6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana:

Zijue kazi za ini

Post hii inahusu zaidi kazi za ini, ni kiungo muhimu kwenye mwili ambacho Kina umuhimu sana, bila ini maisha ya mwanadamu yanaweza kuishia pabaya

Soma Zaidi...
Fahamu kuhusu madhara ya uzito mkubwa

Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea kwa mtu mwenye uzito mkubwa,kwa kawaida ili mtu aweze kuwa na uzito wa kawaida ni vizuri na kiafya kupima urefu ukilinganisha na uzito wa mtu.

Soma Zaidi...
Njia za kuzuia kiungulia

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kuzuia kiungulia

Soma Zaidi...
Huduma ya Kwanza kwa mtu aloanguka kifafa

Somo hili linakwenda kukueleza jinsi ya kumfanyia huduma ya Kwanza kwa mtu aloanguka kifafa

Soma Zaidi...
Nini husababisha kizunguzungu?

Posti hii inazungumzia kuhusiana na Mambo mbalimbali ambayo husababisha kizunguzungu.

Soma Zaidi...
Njia za kuzuia damu isiendelee kuvuja

Posti hii inahusu zaidi njia za kuzuia damu isiendelee kuvuja, ni njia ambazo utumika ikiwa kuna damu inavuja kwenye sehemu yoyote ya mwili,kwa hiyo tunaweza kutumia njia hizi ili kuepuka kuendelea kuvuja kwa damu.

Soma Zaidi...
HUDUMA YA KWANZA KWA MTU ALIYEZIMIA (CARDIOPULMONARYRESUSCITATION) AU CPR

Kuzimia ni hali ya kupoteza fahamu ambako kunaendana na kutokuhema.

Soma Zaidi...
Mbinu za kupunguza magonjwa yanayohusiana na figo

Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa figo. Ni ugonjwa unaotokana pale figo linaposhindwa kufanya kazi, tuone mbinu za kufanya Ili kuepuka na tatizo hilo.

Soma Zaidi...
Sababu za michubuko kwa watoto wanaozaliwa

Post hii inahusu zaidi sababu za michubuko kwa watoto wanaozaliwa,ni sababu ambazo uweza kuchangia kuwepo kwa michubuko kwa watoto wanaozaliwa.

Soma Zaidi...