Madhara ya kutoka kwa mimba

Madhara ya kutoka kwa mimba

Post hii inahusu zaidi madhara ya kutoka kwa mimba, kwa kawaida tunafahamu kwamba mimba ikitungwa na mwili mzima huwa na wajibu wa kutunza kilichotungwa kwa hiyo ikitokea mimba ikatoka usababisha madhara yafuatayo.

Madhara ya kutoka kwa mimba.

1. Kutokwa sana na damu .

Kwa kawaida mimba ikitoka mama utokwa sana na damu hali ambayo usababisha madhara mbalimbali kwa akina mama ambayo ni pamoja na upungufu wa damu mwilini,kuzimia na wakati mwingine kuwa  na matatizo katika sehemu mbalimbali za mwili au kwa wakati mwingine kama mimba zinatoka mara kwa mara usababisha ugumba kwa akina mama.

 

 

 

 

2. Wakati mwingine kutoka kwa mimba mara kwa mara usababisha mimba zingine kutungwa nje ya kizazi kwa sababu ya kuharibikiwa kwa mfuko wa kizazi.

 

 

 

 

3. Pengine kuwepo kwa msongo wa mawazo kwa sababu kuna familia nyingine mama kama ameolewa na mimba zinatoka usababisha kutengwa na ndugu hasa wanaume zao kuwatenga hali inayosababisha kuwepo kwa msongo wa mawazo.

 

 

 

4. Kutoka kwa mimba mara kwa mara usababisha kuwepo kwa magonjwa ya kuambukiza utokea pale mama anapopewa damu labda pengine kuna virusi vya Ukimwi na homa ya ini.

 

 

 

5. Kusababisha kuharibika kwa mfuko wa uzazi.

Kwa sababu wakati mwingine vyuma utumika ili kuweza kutoa uchafu uliopo hali ambayo usababisha kuharibika kwa mfuko wa uzazi.

 

 

 

6. Kubadika kwa siku za kawaida za mwezi.

Kwa sababu ya kutoa mimba mara kwa mara hali hiyo pia usababisha kuharibika kwa mfumo wa mzunguko wa mwezi.

 

 

 

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Uzazi Main: Post File: Download PDF Views: 2470

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Dua za Mitume na Manabii     👉3 web hosting     👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉5 Bongolite - Game zone - Play free game     👉6 ai web app    

Post zinazofanana:

Madhara ya mwili kushindwa kutengeneza projestron ya kutosha

Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo mtu anaweza kupata ikiwa mwili utaeweza kutengeneza progesterone ya kutosha.

Soma Zaidi...
Dalili za hatari kwa mama aliyejifungua.

Posti hii inaelezea kiufupi kabisa kuhusiana na Dalili za hatari kwa mama aliyejifungua.

Soma Zaidi...
Je, wajua sababu zinazopelekea maumivu ya Matiti kwa wanawake?

Maumivu ya matiti ni malalamiko ya kawaida miongoni mwa wanawake yanaweza kujumuisha uchungu wa matiti, maumivu makali ya kuungua au kubana kwenye tishu zako za matiti. Maumivu yanaweza kuwa ya mara kwa mara au yanaweza kutokea mara kwa mara tu. Maumiv

Soma Zaidi...
Tabia za Ute wa siku za hatari kupata mimba au ovulation

Posti hii inahusu zaidi tabia mbalimbali za Ute wa ovulation kwa sababu Ute huu huwa tofauti na Ute mwingine kwa sababu ya kuwepo kwa tabia zake za kipekee kama tutakavyoona.

Soma Zaidi...
Madhara ya vidonge vya P2

Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea kwa sababu ya kutumia mara kwa mara vidonge vya P2,

Soma Zaidi...
Siku za kupata mimba

Nitakujulisha siku ya kupata mimba na sifa zake, na namna ya kuweza kuitafuta

Soma Zaidi...