Posti hii inahusu zaidi mapendekezo muhimu kwa wajawazito, haya ni mapendekezo yaliyotolewa na wataalamu wa afya ili wajawazito waweze kule mimba zao vizuri na kuweza kujifungua vizuri na kupata watoto wenye afya njema na makuzi mazuri pasipokuwepo na ule
Mapendekezo muhimu kwa wajawazito.
1.Kwanza kabisa wajawazito wanapaswa kuwa na mlo kamili na kupata chakula cha kutosha na pia akina mama wanapaswa kula vyakula vyenye wanga , protini, mafuta, mboga za majani, matunda na kunywa maji walau kwa siku glass nane na pia akina mama wajawazito wanapaswa kuachana na vyakula ambavyo havina faida yoyote mwilini kama vile kula pembe, Mawe na vitu vya aina hiyo na pia wanawake wajawazito wanapaswa kuachana na vileo vikali pamoja na uvutaji wa bangi kwa sababu ni hatari kwa afya ya mtoto.
2. Pia akina Mama wanapaswa kuangaliwa kila mwezi kwa Upande wa Mama anapaswa kuangaliwa kama anavimba miguu, ana damu ya kutosha,ana malaria au anaumwa ugonjwa wowote kama kina shida kati ya hayo anapaswa kwenda kupata matibabu Mara moja, na kwa upande wa mtoto aliyeko tumboni anapaswa kuangaliwa jinsi alivyolala tumboni,kama anapumua , kupima kimo cha mtoto na kutabiri tarehe na siku ambayo mtoto atazaliwa kwa kufanya hivyo kila mwezi kwa asilimia tisini na tano mtoto atazaliwa salama.
3.Kuzuia magonjwa nyemelezi kwa Mama na mtoto.
Kwa kuzuia magonjwa nyemelezi kama vile Malaria, kupungua kwa damu mwilini, kupima maambukizi ya virus vya ukimwi ni pendekezo la Muhimu sana ambalo homkinga mtoto na maradhi mbalimbali, kwa hiyo ili kupambana na magonjwa hayo kila baada ya mwezi Mama utumia vidonge vya sp, vidonge vya follic asidi kwa ajili ya kuongeza damu,kutumia dawa za minyoo pale anapoanza mahudhurio na pia Mama hupewa neti bure anapoanza mahudhurio kwa kufanya hivyo tunaweza kupambana na magonjwa nyemelezi kwa Mama na mtoto.
4.Uangalizi wa Mama baada ya kujifungua na uangalizi mkubwa pale ambapo mimba inaonekana kubwa na vikwazo vingi, katika kipindi hiki Mama ambaye ana matatizo wakati wa kujifungua anapaswa kuja hospitalini mapema anapofikisha miezi ile inayofikiliwa kubwa huwa anapata matatizo, mama huwa kwenye uangalizi wa manes na wataalamu wa afya walio na ujuzi ili likitokea jambo lolote awe tayari kupambana nalo na kumfanya Mama akifungua salama.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inakwenda kukueleza jinsi ya kuwjuwa kama mtoto ni wa kike ama wa kiume.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za kutangulia kwa kitovu wakati wa mtoto anapozaliwa.
Soma Zaidi...Dalili za kuharibika kwa ujauzito na dalili za kuharibika kwa ujauzo
Soma Zaidi...Uzazi wa Mpango hutoa chaguo kwa familia kuwa na idadi ya watoto wanaotaka katika muda maalum, wanahisi na mbinu iliyoamuliwa. Uzazi wa mpango una faida kadhaa kwa mama wa mtoto, wanandoa na jamii Ujuzi wa mzunguko wa hedhi humwezesha mtoa huduma kumshaur
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi kuvunjika kwa mtoto wakati wa kuzaliwa, hali hii utokea kwa watoto wadogo wakati wa kuzaliwa kwa sababu maalum kama tutakavyoona.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mda ambao mama anapaswa kukaa bila kufanya tendo la ndoa mara tu baada ya kujifungua.
Soma Zaidi...Utajifunza dalili za minyoo, sababu za minyoo na namna ya kujiepusha na minyoo. Dalili kuu 5 za minyoo mwilini
Soma Zaidi...Jifunze muda ambao mjamzito hatatkiwa kishiriki tendo la ndoa. je kuna madhara kwa mjamzito kushiriki tendo la ndoa.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo mtu anaweza kupata ikiwa homoni ya estrogen imeongezeka, hizi dalili zikitokea mama anapaswa kuwahi hospital ili kuweza kupata matibabu au ushauri zaidi.
Soma Zaidi...Hii ni orodha ya dawa ambazo hutumiwa sana na watu kutoka maduka ya dawa lakini sio salama kwa wajawazito.
Soma Zaidi...