Sababu za kutangulia kwa kitovu wakati Mtoto anazaliwa

Posti hii inahusu zaidi sababu za kutangulia kwa kitovu wakati wa mtoto anapozaliwa.

Sababu za kutangulia kwa kitovu wakati Mtoto anazaliwa.

1. Kwa kawaida tunajua kuwa mtoto utanguliza kichwa ila kwa wakati mwingine Kuna uwezekano mkubwa wa mtoto kutanguliza kitovu, na kwa wakati mwingine kitovu hicho kinaweza kuja kimejivilingisha kwenye shingo na mtoto akipata shida wakati wa kutoka kitovu kinaweza kumniga akafariki au kama Kuna ujuzi zaidi kwa wataalamu wa afya mtoto anaweza kuokolewa kwa hiyo zifuatazo ni sababu za kitovu kutangulia wakati mtoto anapozaliwa.

 

 2. Jinsi mtoto alivyolala.

Kwa kawaida mtoto tunamtegemea aanze kutoa kichwa wakati wa kuzaliwa ila Kuna watoto wanatanguliza matako, kichwa, uso, mgongo na vitu kama hivyo ambavyo ni kawaida na kichwa kwa hiyo katika kujigeuza geuza Ili aweze kupata sehemu ya kutanguliza saa nyingine kitovu kinatanguli mbele kabla ya mtoto.

 

3. Mtoto kuwa zaidi ya mmoja.

Kwa wakati mwingine hasa kwa akina Mama ambao ujifungua mapacha kwa sababu ya kuwepo mtoto Zaid ya mmoja kila mtoto utafuta jinsi ya kutoka Ili aweze kuzaliwa kwa hiyo katika kiangaika Ili kupata nafasi usababisha kutangulia kwa kitovu badala ya kichwa.

 

4. Kupasuka kwa membrane kabla ya mtoto kuingiza kichwa kwenye mlango wa kizazi.

Kuna wakati mwingine chupa upasuka mapema sana kabla ya mtoto kuingiza kichwa kwenye mlango wa kizazi hali hii nayo usababisha mtoto kutanguliza kitovu.

 

5. Muundo wa mlango wa kizazi.

Pengine Kuna akina Mama wameumbwa tofauti kabisa na kuwa na uwezo wa kupitisha mtoto na akifika wakati wa kusukuma mtoto hawezi kupita ingawa anahisi uchungu na sifa zote za kujifungua anakuwa Nazo katika kuangaika anajikuta mtoto ashatanguliza kitovu.

 

6. Kwa hiyo hali hii ni ya hatari endapo wahudumu wa afya hawana utaalamu wa kugundua mapema tatizo hili, ni vizuri kuligundua Ili kuweza kuokoa maisha ya Mama na mtoto wakati Mama akiwa anajifungua.

 Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/05/23/Monday - 06:39:31 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1517


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-