Fahamu ugonjwa wa kifafa cha mimba.

Post hii inahusu zaidi Ugonjwa wa kifafa cha mimba ambapo kwa kitaalamu huitwa eclampsia, utokea pale ambapo Mama anapokuwa na degedege wakati wa mimba na baada ya kujiunga.

Ugonjwa wa kifafa cha mimba.

1. Kama tulivyoona hapo juu kwamba Ugonjwa huu usababishwa na kuwe kwa kifafa wakati wa ujauzito na mtu anakuwa hana historia yoyote ya kifafa au Magonjwa ya akili au Malaria, ila utokea tu hasa wakati wa ujauzito na wakati baada ya kujifungua, kwa hiyo tatizo hili halijapata ufumbuzi zaidi kwamba kisababishi ni nini.

 

2.Pamoja na kukosa kisababishi Tatizo hili uwapata hasa hasa wanawake wenye shinikizo la damu wakati wa ujauzito na kuwepo kwa kiasi kikubwa cha protini kwenye mkojo, kwa hiyo hali hii ikitokea kwa wajawazito ni lazima kutibu mapema ili kuepuka kuwepo kwa tatizo la kifafa wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua kwa hiyo wauguzi na ndugu wa karibu ni jukumu la kuwa sana karibu na wanawake walio katika hatari ya kupata tatizo hili na kuwasaidia wale walio kwisha pata Ugonjwa huu.

 

3. Kwa hiyo ili kuweza kuepuka tatizo hili wanawake wote wanapaswa kuhudhuria kliniki mapema pale wanapogundua kwamba ni wajawazito kwa sababu kwa kufanya hivyo wakiwa kliniki wanapata mafunzo mbalimbali kuhusu Dalili za hatari wakati wa ujauzito na pia kupima presha kila udhulio ili kuhakikisha kama hali ya Mama iko sawa ikitokea Mama akakutwa na presha au protini kwenye mkojo matibabu uanza mapema na tatizo haliwezi kuwa kubwa kama yule ambaye hakutambua mapema.

 

4. Vile vile kuna mila na desturi ambazo ufanyika kwenye jamii kwa kutumia matibabu yasiyo sahihi kwa kuwatumia waganga wa kienyeji pale Mama akipata kifafa hali ambayo Usababisha hali za wamama kuwa mbaya na kusababisha vifo wakati wa ujauzito,kwa hiyo ni vizuri elimu ikatolewa kwa jamii ili kuweza kuepuka vifo visivyo vya lazima kwa watoto na akina Mama, kwa hiyo akina Mama wawe Macho ili kuokoa maisha yao na watoto wao .

 

5.Endapo Mama wajawazito wakihisi dalili ambazo si za kawaida wanapaswa kuwahi mapema hospitali na kuwahi mapema kliniki mara tu wanapohisi wana mimba ili kuweza kupata huduma muhimu na za kweli.

 Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/04/10/Sunday - 06:30:48 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1110


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-