Post huu inahusu zaidi utaratibu wa chakula kwa Mama mjamzito, ni chakula anachopaswa kutumia na ambavyo hapaswi kutumia kwa Mama mjamzito mzito, kwa sababu Mama mjamzito anapaswa kuwa makini katika matumizi ya chakula ili kuweza kuongeza vitu muhimu mwil
Utaratibu wa chakula kwa Mama mjamzito.
1. Mama mjamzito anapaswa kutumia aina zote tano za vyakula kama vile vyakula vya wanga kwa kiasi kikubwa ili kuongeza nguvu kwa Mama, vyakula vya protini kwa wingi ili kujenga mwili, vyakula vya mafuta kwa kiwango kidogo, pia Mama anapaswa kutumia mboga mboga za majani na kunywa maji kwa wingi, anapaswa kunywa glasi nane au lita moja na nusu kila siku na pia Mama anapaswa kula vyakula vya wanyama kama vile maini na nyama kwa kufanya hivyo anaweza kumfanya mtoto akue vizuri.
2. Pia Mama anapaswa kula vyakula vyenye wingi wa vitamini C kama vile matunda mbalimbali yanayoweza kulinda mwili na kuzuia dhidi ya magonjwa ili kuongeza kiasi cha kuongeza kiasi cha damu mwilini na kuongeza madini ya chuma. Kwa hiyo tunajua kabisa mama mjamzito anapaswa kuwa na damu ya kutosha kwa hiyo mboga za majani ni lazima.
3. Pia Mama wajawazito wanapaswa kuachana kutumia kahawa, soda na chai wakati wa kula chakula kwa sababu uingiliana na madini ya chuma yaliyomo mwilini na baadae mama anaweza kupata upungufu wa damu na pia Mama mjamzito anapaswa kuachana na kunywa pombe kali na yenyewe uingilia na madini ya chuma na kusababisha kuwepo kwa upungufu wa damu.
4. Pia Mama wajawazito wanapaswa kutumia dawa mbalimbali za hospitali ambazo uongeza damu kuzuia Malaria na kuzuia minyoo, dawa hizo ni kama iron na folic acid, iron inapaswa kuwa na 200g ya ferrous sulphate, na 0.4 milligram of follic asidi. Na pia wajawazito wanapaswa kutumia calcium kuanzia 1.5 mpaka Mbili milligram, pia wanapaswa kutumia Mebendazole na sp, wanawake wajawazito wakifanya hivyo wataweza kuwa na damu ya kutosha na kuzuia mtoto dhidi ya Malaria na minyoo.
5. Pia wanawake wanapaswa kuachana na mila potofu ambazo ziko kwenye baadhi ya makabila kama vile kutotumia baadhi ya vyakula kama vile mboga za majani, mayai na vyakula vinginevyo na pia wanawake wanapaswa kuachana na mila mbaya za kutotumia dawa za hospitali na baadae utumia dawa za nyumbani ili kuongeza uchungu, hizi dawa usababisha mtoto kukatika tumboni na baadae matatizo mbalimbali yanaweza kutokea kama vile kifo cha mama na mtoto.
6. Pia Mama wajawazito wanapaswa kuachana na vileo vyovyote wakati wa Mimba kama vile uvutaji wa sigara, matumizi ya madawa ya kulevya, kutumia pombe kali hali huu usababisha Mama kujifungua mtoto njiti au mara nyingine mtoto kuzaliwa kabla ya wakati, kujifungua mtoto mfu na pengine kujifungua mtoto mwenye ulemavu, kwa hiyo jamii nzima inapaswa kujua kuwa vileo vyovyote hasa vikali kwa Mama mjamzito ni hatari na usababisha kupata watoto wengi wenye matatizo mbalimbali.
7. Pia Mama wajawazito wanapaswa kuachana na vyakula ambavyo havina faida yoyote mwilini, vyakula hivi ni kama vile matumizi ya pemba, udongo, mkaa na vitu mbalimbali kama hivyo iwapo Mama akijisikia kutumia vyakula vya hivyo anapaswa kwenda kuonana na mhudumu wa afya inawezekana ikawa ni kuwepo kwa minyoo au upungufu wa madini mwilini. Kwa hiyo jamii ijue kuwa vyakula vya hivi havina umuhimu wowote mwilini.
8. Kwa hiyo tunapaswa kujua kuwa Mama mjamzito anapaswa kula mara nyingi iwapo kama chakula kipo na chakula hicho kinapaswa kuwa na toka au vya muhimu kama tulivyoona hapo awali, kwa hiyo jamii yenye imani potovu na kuwawekea wajawazito mda wa kula ambao ni mdogo wanakosea kwa sababu Mama asipopata chakula cha kutosha anaweza kujifungua mtoto mwenye kilo chini ya mbili na nusu kwa hiyo chakula ni muhimu kwa wajawazito .
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Utajifunza sababu za kuweo kwa maumivu ya uume wbaada ya tendo la ndoa na wakati wa tendo la ndoa.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa uzazi wa mpango kwa watoto, sio akina Mama peke yao wanaofaidika na uzazi wa mpango vile vile na watoto wanafaidika na uzazi wa mpango kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufunza mambo mengi kuhusu tezi dume kama chanzo, dalili, matibabu, njia za kujikinga na mambo hatari yanayoweza kukusababishia kupata tezi dume.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi maji ya Amniotic ni maji ambayo uzunguka mtoto na kufanya kazi mbalimbali kama ifuayavyo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu mbalimbali ambazo zinafanya wajawazito kupata ugonjwa wa Bawasili, kwa sababu tatizo hili linawapa wakina mama wajawazito, kwa hiyo tutaona kwa nini wajawazito wanapatwa na tatizo hili sana.
Soma Zaidi...Je unaijuwa siku yako hatari ya kupata mimba. Na itakuwaje kama tayari umebeba mimba changa. Nakala hii inakwenda kukushauri machache kuhusu maswali haya.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna ya kuangalia maendeleo ya mtoto akiwa tumboni mwa mama, zoezi hili ufanyika kila mwezi pale mama anapokuja kwenye mahudhurio kwa kufanya hivyo tunaweza kuja maendeleo ya mtoto kwa kila mwezi.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi Ugonjwa wa kifafa cha mimba ambapo kwa kitaalamu huitwa eclampsia, utokea pale ambapo Mama anapokuwa na degedege wakati wa mimba na baada ya kujiunga.
Soma Zaidi...Watu wengi wanadhania kuwa kufanya tendo la ndoa katika siku hatari ni lazima kuwa utapata ujauzito. Hili sio sahihi kabisa. Post hii itakwenda kuangalia jambo hili zaidi.
Soma Zaidi...