Fahamu kuhusu fangasi za ukeni

Posti hii inahusu zaidi fangasi za ukeni, hili ni tatizo kubwa ambalo linawakumba watoto, akina dada na wanawake kwa hiyo na vizuri kujua Dalili zake na kuweza kuchukua hatua mapema.

Fangasi za ukeni

1. Dalili ya kwanza ya kuwepo kwa fangasi za ukeni ni kukojoa mara kwa mara, kwa kawaida tunajua wazi ili mtu akojoe ni lazima awe amekunywa kimiminika chochote,ila kuna kipindi mtu anakojoa mara kwa mara bila kunywa chochote cha zaidi.

 

2. Mkojo kuwa na harufu mbaya.

Kwa kawaida mkojo huwa na harufu yake ya kawaida ila kuna kipindi mkojo unakuwa na harufu mbaya sana, kwa hiyo ni vizuri kuangalia tatizo mapema.

 

3. Maumivu ya misuli ya tumbo hasa chini ya kitovu.kuna wakati mwingine tumbo linauma hasa kitovuni ingawa inaweza kuwa ni Dalili ya magonjwa mbalimbali lakini ni vizuri kufanya uangalizi.

 

4. Maumivu ya kiuno.

Kwa sababu ya kusambaa kwa fangasi mara nyingi kunakuwepo na maumivu ya kiuno kwa hiyo ni vizuri kuangalia mapema ili kuweza kufahamu tatizo ni nini.

 

5. Kuwepo kwa miwasho kwenye sehemu za siri.

Hii ni Dalili kubwa sana ambayo inatokea kwa walio wengi kwa sababu kuna kipindi mtu anawashwa sana kwenye sehemu za siri hasa hasa baada tu ya kukojoa.

 

6. Maumivu wakati wa kujamiiana.

Kuna wakati mwingine kunakuwepo na maumivu makali wakati wa kujamiiana, kwa sababu ya kuwepo kwa vidonda au majeraha yaliyosababishwa na fangasi kwa hiyo ni lazima maumivu kuwepo wakati wa tendo.

 

7. Kuwepo kwa vidonda ukenu.

Kwa sababu ya kuwepo kwa fangasi hasa wa mda mrefu usababisha vidonda ukeni na kusababisha mgonjwa awe anajikuna mara kwa mara.

 

8. Kuwepo kwa moto baada ya kujamiiana.

Kwa sababu ya kuwepo kwa fangasi usababisha kuwepo kwa moto baada ya kujamiiana.

 Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/06/03/Friday - 12:08:23 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 923


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-