Malaria inaweza kumpata mtu yeyote bila ya kujali mri. Lakini kuna watu endapo wakipata malaria inakuwa ni mbaya zaidi kwa afya yao binafsi ama na kwa ya watu wengine. Watu hao ni:-
Wajawazito: wajawazito ni katika watu ambao ni hatari sana kwao wakipata malaria. kwani inaweza ikahatarisha pia afya ya mtoto aliye tumboni. wajawazito wanashauriwa kulala kwenye chandarua tena kilichokuwa na dawa. hii itasaidia kupunguza uwezekano wa kupata malaria.
Watoto wadogo chini ya miaka mitano, tafiti zinaonesha kuwa wanaofariki kwa ugonjwa wa malaria wengi wao ni watoto tena walio chini ya umri wa miaka 5. kundi hili la watu ndilo ambalo bado halijakuwa madhubuti kiafya kiasi cha kuweza kupambana na athari za malaria. hivyo ni vyema kuhakikisha kuwa watoto siku zote wanalala kwenye chandarua chenye dawa.
Wazee; kundi jingine linaloathiriwa na malaria ni hili kundi la wazee. afya za wazee hazipo imara sana ukilinganisha na afya za vijana. huenda ni kwa sababu miili yao haipo active muda wowote, huenda kwa sababu wazee wengi hawana kawaida ya kufanya mazoezi ya hapa na pale.
Watu wanaotoka ameneo yasiyo na malaria, kundi la mwisho linawahusu sana wageni ambao wametoka katika maeneo yasiyo na mbu ama yasiyo na ugonjwa huu. watu hawa miili yao haina mazoea na ugo njwa huu hivyo hakuna walinzi walio tayari kwa ajili ya kupunguza athari za malaria.