Pindi malaria isipotibiwa inaweza kufanya dalili ziendelee na hatimaye kusababisha kifo. Lakini kabla ya kutokea kifo malaria huanza kwa kuathiri maeneo nyeti sana ya kiafya na hivyo hupelekea athari kubwa ambazo huleta kifo. Hebu tuone maeneo ambayo malaria hushambulia:-
Ubongo, vimjidudud vya malaria vinapoingia kwenye mfumo wa damu huanza kushambulia seli hai nyekundu za damu. Kupitia damu vijidudu hivi vinaweza kuingia kwenye ubongo na kusababisha kuziba kwa vimishipa vijidogo ndani ya upongo. Vimishipa hivi ndivyo hupeleka virutubisho na hewa kwenye ubongo. Hali hii inaweza kumfanya mgonjwa achanganyikie na kupoteza fahamu kabisa.
Ini na figo, vijidudu hivi vinaweza kusababisha ini na figo kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi, ama tena kufa kabisa. Endapo hali hii ikitikea basi itakuwa ni athari kubwa sana katika afya ya mtu husika.
Mapafu, endapo malaria haitatibiwa na ikiendelea kuwepo mwilini inaweza kusababisha kujaa kwa majimaji kwenye mapafu. Hali hii inaweza kusbabisha mgonjwa kushindwa kupumua kwa ufanisi. Endapo hili litatokea itakuwa ni katika athari mbaya sana za malaria.
Damu, kwakuwa vijidudu hivi hushabulia seli hai nyekundu za damu, na seli hizi ndizo hubeba hewa ya oksijeni na kuisambaza mwilini. Hivyo malaria inaweza kusababisha upungufu wa hewa ya oksijeni mwlini na kusababisha ugonjwa unaotambulika kama anaemia.
Wakati mwingine malaria inaweza kuwa kali zaidi na kusababisha sukari kushuka, hali hii kitaalamu inajulukana kama hypoglycaemia. Na ni katika hali mbaya sana kwani mgonjwa anaweza kupoteza fahamu.