KUJIKINGA NA MALARIA

 

Kwa kuwa mbu wanaosambaza malaria wanang’ata usiku sana ama alfajiri, hivyo tunaweza kujikinga na malaria kwa :-
Kulala kwenye chandarua, ni vyema kikatiwa dawa. pia ni vyema ukahakikisha kuwa chandarua hakina matundu yaani kiwe kizima. ha hakikisha unawatoa mbu kwenye chandarua kama wapo kisha ndipo ujiandae kulala.

 

Kupaka losheni ya mbu; hiki ni losheni ambazo zina harufu mbaya ambayo inawakera mbu. harufu hiki huweza kutofautiana. kuna nyingine ni kali na nyengine ni kawaida. kuna nyingine utapenda harufu zao na nyingine hutapenda. watu wengine wakipaka losheni hizi huwashwa hususani wanapopaka usoni. hakikisha haupaki mdomoni kiasi kwamba unaweza kuila losheni kwa bahati mbaya.

 

Kuvaa nguo ndefu zinazoziba viungo; nguo hizi zisiwe ndefu tu bali ziwe nzito kiasi kwamba zinaweza kuzuia mbu kuifikia ngozi yako. ni vyea zikafunika mikono na miguu, na maeneo mengine ambayo yanashambuliwa na mbu kama shingo.

 

Kutumia dawa za mbu; dawa hizi zipo za kupulizia kama pafyumu na zipo za kuchoma. unaweza kutumia za kupulizia wakati hupo ndani kwa muda wa dakika kama 30. dawa za kuchoma nazo pia ni vyema ukachoma ukiwa umetoka kisha baada ya dakika 30 kisha ingia ndani.

 

Fyeka vichaka, punguza nyasi na fukia madimbwi yaliyo karibu na nyumba. hakikisha hakuna makopo, vifuu ama chochote kinachoweka maji. hii itasaidia kupambana na mazalia ya mbu.