HOMA YA MANJANO (yellow fever)Homa ya manjano ni maradhi yanayosababishwa na virusi na husambazwa na mbu.
HOMA YA MANJANO (yellow fever)
Homa ya manjano ni maradhi yanayosababishwa na virusi na husambazwa na mbu. Homa hii ipo sana nchi za Afrika na Amerika ya Kusini. Kwa hali ya kawaida homa ya manjano huweza kusababisha homa, maumivu ya kichwa, kichefuchefu na kutapika. Pia homa ya manjano inaweza kuwa mbaya zaidi na kupelekea matatizo kwenye ini, figo na moyo pamoja na kutoka kwa damu yali inayotambulika kitaalamu kama hemorrhaging.
Inakadiriwa kuwa asilimia 50 ya wanaopata homa ya manjano wanafariki kwa maradhi maradhi haya. Tafiti zinaonyesha kuwa mpaka sasa hakuna tiba maalumu ya homa ya manjano, ila ipo chanjo kwa ajili ya kujikinga na virusi wanaosababisha homa hii.
Tafiti zinaonesha kuwa baada ya kungโatwa na mbu na kukuachia virusi hawa wa haoma ya manjano, virusi hivi huchukuwa siku tatu mpaka sita kumomaa. Kipindi hiki kitaalamu hufahamika kama incubation period. Katika kipindi hiki katu hutohisi dalili yeyote. Kisha hatua inayofuatainatambulika kama accute phrase kisha hatua ya meisho ni toxic phrase.
DALILI ZA HOMA YA MANJANO
A.Dalili za homa nya manjano katika hatua ya pili (Acute phrase)
1.Homa
2.Maumivu ya kichwa
3.Maumivu ya misuli hasa ya kwenye mgongo na magoti
4.Kutokufurahia mwanga wa jua
5.Vichefuchefu na kutapika
6.Kukosa hamu ya kula
7.Kuhisi kizunguzungu
8.Macho kuwa mekundu, uso na ulimu pia kuwa na rangi nyekundu
B. Dalili za homa ya manjano katika hatua ya pili (toxic phrase)
1.Macho na ngozi kuwa na rangi ya njano
2.Maumivu yasiyo ya kawaida pamoja na kutapika damu
3.Kuongezeka kukojoakojoa
4.Kutoka na damu kwenye mdomo, pua na macho
5.Kupungua kwa mapigo ya moyo (bradycardia)
6.Ini na figo kushindwa kufanya kazi
7.Ubongo kushinwa kufanya kazi, vyema na kusababisha matatizo kama kifafa (seizure), kupoteza fahami (coma) pamoja na kuchanganyikiwa (delirium)
SABABU ZA HOMA NA MANJANO (YELLOW FEVER)
Kama tulivyokwisha kuona kuwa homa ya manjano husababishwa na virusi wanaoenezwa na mbua aina ya Aedes aegypti. Mbu hawa hukaa karibu na maeneo ambayo watu huwa wanaishi na huzaliana kwenye maji yaliyo safi. Virusi vya homa ya manjano vinaweza pia kuwaathiri manyani.
KUJIKINGA NA HOMA YA MANJANO
Ijapokuwa asilimia 20 mapa 50 ya wanaopata homa ya manjano hufariki, lakini itambulike kuwa mgonjwa anauwezo wa kupona kabisa endapo atawahi kupatiw matibabu. Zifuatazo ni baadhi ya njia tu za kujikinga na homa ya manjano
1.pata chanjo ya homa ya manjano
2.Jikinge na kungโatwa na mbu kwa:
?Kulala kwenye chandarua kizima na chenye dawa
?Kupaka losheni ya kuzuia mbu
?Kuondoa majimaji yaliyotuwama na kukata nyasi
Umeionaje Makala hii.. ?
posti hii inazungumzia kuhusiana na Ugonjwa na Ugonjwa unaohusiana na joto ambao hujulikana Kama Anhidrosis ni kutoweza jasho kawaida. Usipotoa jasho mwili wako hauwezi kujipoza, jambo ambalo linaweza kusababisha joto kupita. wakati mwingine inaweza k
Soma Zaidi...Saratani ya Mapafu ni aina ya Kansa inayoanzia kwenye mapafu. Mapafu yako ni viungo viwili vya sponji kwenye kifua chako ambavyo huchukua oksijeni unapovuta na kutoa kaboni dioksidi unapotoa nje.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi matibabu ya kutibu ugonjwa wa maumivu chini ya kitovu.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi aina mbalimbali za michubuko,kwa Sababu michubuko utokea sehemu tofauti tofauti na pia Kuna aina mbalimbali kama tutakavyoona hapo mbeleni.
Soma Zaidi...Post hii inazungumzia zaidi kuhusiana na ugonjwa wa kipindupindu.kipindupindu ni ugonjwa unaosababishwa na mdudu ambaye kwa kitaalamu anaitwa vibrio cholera.mdudu huyu hushambulia utumbo mdogo na kusababisha madhara mengi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi magonjwa ya koo, ni ugonjwa unaoshambulia sana sehemu ya koo la hewa, na na huwa na dalili zake kama ifuayavyo.
Soma Zaidi...NAMNA YA KUISHI NA VIDONDA VYA TUMBO Unaweza kupata nafuu kutoka kwa maumivu ya kidonda cha tumbo ikiwa utafata taratibu za kiafya kama:- 1.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi jinsi magonjwa yanavyosambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
Soma Zaidi...Post hii fupi inakwenda kukujuza juu ya tatizo la fangasi na nini ufanye.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu athari za kutokutibu fangasi
Soma Zaidi...