Posti hii inahusu zaidi madhara ya Tiba homoni, ni madhara- ambayo utokea kwa mgonjwa anayetumia homoni kama Tiba kwenye kutibu saratani.
Madhara ya kutumia Tiba homoni
1. Kuongezeka Uzito kwa mgonjwa
Kuongezeka kwa uzito wa mgonjwa ni mojawapo ya madhara ambayo utokea kwa mgonjwa anayetumia Tiba homoni, tunajua kwamba hii Aina ya Tiba uzuia homoni ambazo usababisha saratani kushindwa kuzalishwa au kusambaa kwenye mwili, madawa haya umwongezea mgonjwa uzito kwa hiyo mgonjwa anapaswa kutumia sana Mazoezi Ili kuepuka kuongezeka kwa magonjwa mengine kwa sababu ya kuongezeka kwa uzito, kwa hiyo anapaswa kutumia vyakula ambavyo haviongezi Uzito kwa haraka.
2. Kupoteza kumbukumbu.
Kwa sababu ya kuwepo kwa madawa ambayo uzuia kuzalisha kwa homoni zinazosababisha kuongezeka kwa saratani haya madawa uingilia mfumo wa ubongo ambao usaidia kutunza kumbukumbu na kusababisha mgonjwa kupoteza kumbukumbu za mara kwa mara kwa hiyo wale wanaiwauguza wagonjwa wawasaidie katika kuwakumbusha mambo mbalimbali na ya maana na wasiwalaumu pale wanapotokea kusahau baadhi ya vitu na vya muhimu kwa sababu ya hali waliyonayo.
3. Mabadiliko ya hisia
Wagonjwa wanaotumia homoni kama dawa ya kutibu saratani Wana Tabia ya kubadilika kwa hisia mara nyingine utawakuta wamefurahi sana, mara nyingi utawakuta wamekasilika sana na hata mara nyingine kuwachagua watu wa kuwatunza na kuwakataa wengine, Hal hii ikitokea kwa wagonjwa wanaotumia homoni kama dawa ya kutibu saratani jamaa na wote wanaomuuguza wanapaswa kuchukualia kawaida walidhani na kuona ni kawaida na wasiwe wakali kwa Tabia za mabadiliko ya wagonjwa.
4. Kukosa hamu ya tendo la ndoa.
Wagonjwa wanaotumia homoni kama dawa ya kutibu saratani mara nyingi ukumbwa na tatizo la kukosa hamu ya ngono kwa sababu mara nyingine dawa zinazotumika kuharibu homoni za kansa hata hivyo uleta madhara katika mfumo mzima wa kujamiiana kwa hiyo mgonjwa anakosa hamu ya tendo la ndoa, kwa hiyo mwenza wake anapaswa kufahamu tatizo hili na kuelewa mwenzake kama Hana hamu ya tendo la ndoa.
5.kuwepo kwa uchovu
Kwa sababu ya ya dawa ambayo inafanya kazi mwilini na kwa sababu ya kuharibika kwa seli usababisha mwili ws binadamu kuchoka na mara nyingi mgonjwa uhishiwa nguvu kwa hiyo mgonjwa anapaswa kutumia vyakula vyenye wingi wa vitamin, madini na Aina zote za vyakula Ili kumrudisa mgonjwa afya yake ya kawaida
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi watu walio katika hatari ya kupata Maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi,ni kutokana na kazi zao pamoja na mazingira yao kwa hiyo wako kwenye hatari ya kupata Ugonjwa wa ukimwi.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na Ngozi kuwa kavu si mbaya, lakini inaweza kusumbua na isipendeze, ikitengeneza mistari laini na Mikunjo.
Soma Zaidi...Post hii inahusu Zaidi dalili za kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu, ni dalili ambazo zinaweza kujitokeza Kwa mgonjwa,Kwa hiyo baada ya kuona dalili hizi mgonjwa anapaswa kuwahi hospital mara moja Kwa ajili ya matibabu.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia ambazo VVU huambukizwa
Soma Zaidi...Makala hii inakwenda kukuletea somo linalozungumzia maumivu ya tumbo chini ya kitomvu, na tumbo la ngiri kwa wanaume, na tumbo la chango kwa wanawake
Soma Zaidi...Dalili za HIV na UKIMWI kwenye mdomo na ulimi utaziomna hapa. hizi zinaweza kuwa ndio za kwanza kwa ambaye hajapima HIV
Soma Zaidi...je na wewe ni mmoja katika wenye maumivu ya tumbo upande mmoja?. Basi post hii ni kwa ajili yako.
Soma Zaidi...Saratani ya Utumbo ni Saratani ya utumbo mpana (koloni), sehemu ya chini ya mfumo wako wa usagaji chakula. Kwa pamoja, mara nyingi hujulikana kama Saratani ya utumbo mpana. Visa vingi vya Saratani ya utumbo mpana huanza
Soma Zaidi...