Posti hii inahusu zaidi madhara ya Tiba kemikali, ni madhara yanayotokea kwa wagonjwa wa saratani, madhara haya yanayoweza kuwa ni kwa Sababu mbalimbali kama vile kuaribika kwa seli zinazoendelea kufanya kazi kwenye mwili.
Madhara ya Tiba kemikali.
1. Miwasho ndani ya pua na mdomoni, miwasho hii utokea sehemu za pua na midomoni ambayo uendana na kuwepo kwa vipengele ndani ya pua na midomoni na puani hali hii ikitokea kwa wagonjwa wa saratani wanapaswa kutumia dawa za kawaida zinazotumika kutibu maupele kwenye mdomo na puani na pengine hali ikiendelea mgonjwa anapaswa kuonana na daktari wake kwa ushauri zaidi na pia mgonjwa anapaswa kutumia sana vyakula vya kujenga mwili.
2. Kupoteza nywele kichwani.
Wagonjwa wa saratani upotea nywele kichwani hii ni kwa sababu ya kemikali ambayo uharibu mfumo wa seli na kusababisha nywele kuisha kwa mda kichwani, lakini baadae urudi tena hali hii ikitokea kwa wagonjwa wa saratani jamii inabidi kuelewa kuwa ni Sababu ya madawa na waepuke kuwa na Imani potofu kuhusu wagonjwa wa Aina hii na pia wanapaswa kutumia vyakula vya kutosha Ili kuweza kurudisha afya zao kwenye hali ya kawaida na vyakula viwe na virutubisho vya kutosha.
3. Mgonjwa anakuwa na uchovu
Kwa kawaida wagonjwa wanaotumia dawa hii ya Tiba kemikali huwa na uchovu wa mara kwa mara kwa Sababu seli zao huwa zimearibiwa na kemikali na kwa hiyo wakati wa Tiba mgonjwa uhisi kuwa na uchovu kwa hiyo anapaswa kupumzika na sio kupumzika mda wote Bali anapaswa kutembea kwa mda wa dakika Kumi na Tano Ili kuupatia mwili mazoezi ya kutosha ingawa mazoezi yasiwe ya mda mrefu Bali kidogo kidogo na pia kutumia vyakula vinavyoongeza nguvu mwilini Ili kuondoa uchovu wa mara kwa mara.
4. Mgonjwa anayetumia Tiba kemikali huwa na kichefuchefu .hali hii utokea kwa sababu ya dawa zinazotumika kuharibu mfumo wa umengenyaji ambapo mgonjwa uhisi kurudisha kila kitu anachokula kwa hiyo mgonjwa anapaswa kula kidogo kidogo na mara kwa mara, anapaswa kutumia vitu vigumu kama vile mkate na chapati na anapaswa kuepuka kuinama akae wima na kuepuka vyakula ambavyo huwa havipendelei vinaweza kusababisha kutapika .
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowPosti hii inahusu zaidi mlo kwa wagonjwa wa figo wanaochujwa damu, ni wagonjwa ambao figo zao zimeharibika na zimeshindwa kufanya kazi au pengine kuna uchafu mwingi mwilini ambao uchujwa kwa hiyo kuna vyakula muhimu ambavyo wagonjwa wa figo wanapaswa kutu
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea kuhusiana na Damu kutokuganda ambalo hujulikana Kama Hemophilia, ni ugonjwa nadra ambapo damu yako haigandi kawaida kwa sababu haina protini za kutosha za kuganda. Ikiwa una tatizo la Damu kutokuganda, unaweza kuvuja damu kwa muda mre
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za Homa ya uti wa mgongo, ni dalili ambazo ujitokeza kwa mtu Mwenye maambukizi kwenye uti wa mgongo.
Soma Zaidi...Sty ni uvimbe mwekundu, chungu karibu na ukingo wa kope ambalo linaweza kuonekana kama jipu au chunusi. Sties mara nyingi hujazwa na usaha. Mtindo kawaida huunda nje ya kope lako. Lakini wakati mwingine inaweza kuunda kwenye sehemu ya ndani ya kope lak
Soma Zaidi...Makala hii itakufundisha maradho makuu ya macho, matibabu yake na tiba zake
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu faida za bamia mwilini
Soma Zaidi...Posti hii inahusu sababu za mwanamke kuumwa tumbo chini ya kitovu, ni tatizo ambalo limewapata wanawake wengi na pengine sababu ni vigumu kupata au pengine zinapatikana lakini kwa kuchelewa hali ambayo usababisha madhara mbalimbali kwenye mwili.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu minyoo na athari zao kiafya
Soma Zaidi...Post hii inazungumzia kuhusiana na Sababu zinazopelekea kuvimba kwa kope, kawaida huhusisha sehemu ya kope ambapo kope hukua na kuathiri kope zote mbili. Pia hutokea wakati tezi ndogo za mafuta ziko karibu na msingi wa kope huziba. Hii inasababisha kuw
Soma Zaidi...Posti hii inaonyesha mambo mbalimbali yanayoweza kusababisha Ugonjwa wa kifua kikuu kwa watoto chini ya miaka mitano.
Soma Zaidi...