DALILI ZA HIV ZA MWANZO NA DALILI ZA UKIMWI ZA MWANZO Kama ilivyo magonjwa mengi hupitia hatua kadha kadha na kuonyesha dalili kadha katika hatua hizo.
DALILI ZA HIV ZA MWANZO NA DALILI ZA UKIMWI ZA MWANZO
Kama ilivyo magonjwa mengi hupitia hatua kadha kadha na kuonyesha dalili kadha katika hatua hizo. Basi HIV nayo ina hatua zake mpaka kuwa UKIMWI.
DALILI ZA MWANZO ZA HIV AMA UKIMW
Dalili hizi huanza kuonekana kuanzia wiki mbili mpaka nne na wakati mwingine mpaka sita toka kuingia mwilini. Mara chache sana huweza kuonekana mwanzoni mwa wiki ya kwanza. Katika kipindi hiki mtu anaweza kuona dalili zifuatazo:
1.kufimba kwa tezi za kwenye makwapa, mapaja na shingo
2.Homa
3.Uchovu
4.Kuharisha
5.Kupungua uzito
6.Kikohozi
7.Pumzi kutoka kidogodogo
8.Mafua
Dalili hizi pia zinaweza kuhusiana na maradhi mengine, hivyo inaweza kuwa vigumu kujuwa nini chanzo zaidi. Wengi katika wanaopata HIV wametaja kuwa kuvimba kwa tezi ndio dalili pekee walioweza kuopata mwanzoni mwa kuathirika kwao. Wengine wanataja mafua kuwa ndio dalili yao ya kwanza.
Baada ya kipindi hiki kupita mgonjwa hatapata dalili yeyote ile. Hiki ni kipindi hatari sana kwani mtu hataweza kujijua kama ameathirika. Kipindi hiki kinaweza kudumi mpaka miaka 10. katika kipindi hiki virusi vinaendelea kuathiri seli za mwili. Baada ya mwili kuwa umeathirika sana na kudhoofu mtu ataanza kupata dalili za UKIMWI.
DALILI ZA UKIMWI
1.kutokwa na jasho jingi wakati wa usiku
2.Kupata homa za mara kwa mara na kuhisi baridi
3.Kikohozi
4.Kushinwa kupumua vyema
5.Madoa madoa kwenye ulimi na mdomoni
6.Maumivu ya kichwa
7.Uchovu usiokuwa na sababu na usioisha
8.Kutokuona vyema
9.Kupungua uzito
10.Mapele na ukurutu kwenye ngozi
Umeionaje Makala hii.. ?
MATATIZO YA CHOO KIDOGO NA FIGOFigo ni kiungo muhimu sana katika uchujaji wa mkojo, na afya ya mfumo wa utoaji taka mwili.
Soma Zaidi...Pindi malaria isipotibiwa inaweza kufanya dalili ziendelee na hatimaye kusababisha kifo.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na sababu zinazopelekea kukosa choo ,yaani kinyesi kuwa kigumu au kukosa kabisa choo.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi namna Maambukizi kwenye milija na ovari ambayo yanatokea,Mara nyingi usababisha na bakteria wanaoweza kuingia kupitia sehemu mbalimbali.
Soma Zaidi...Ugonjwa sugu wa figo, pia huitwa kushindwa kwa figo sugu, huelezea upotevu wa taratibu wa utendakazi wa figo. Figo zako huchuja taka na Majimaji kupita kiasi kutoka kwa damu yako, ambayo hutolewa kwenye mkojo wako. Ugonjwa sugu wa figo unapofikia hatua
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia au hatua tatu muhimu anazopitia Mgonjwa wa gauni, kuanzia kwa Maambukizi mpaka kwenye hatua ya mwisho hasa kama Ugonjwa huu haujatibiwa mapema.
Soma Zaidi...joto la mwili wako linapungua, moyo wako, mfumo wa neva na viungo vingine haviwezi kufanya kazi kwa kawaida. Isipopotibiwa, Hypothermia hatimaye inaweza kusababisha moyo wako na mfumo wa upumuaji kushindwa kabisa na hata kifo.
Soma Zaidi...Fangasi hawa kitaalamu wanafahamika kama vagina yeast infection na majina mengine ya kitaalamu ni kama vagina candidiasis, u vulvovaginal candidiasis au candidal vaginitis.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya fikra potofu kuhusu vidonda vya tumbo
Soma Zaidi...