HOMA YA DENGUEHoma ya dengue ni miongoni mwa maradhi hatari ambayo husambazwa na mbu.
HOMA YA DENGUE
Homa ya dengue ni miongoni mwa maradhi hatari ambayo husambazwa na mbu. Huweza kutokea katia maeneo ynye uoto wa kitropiki kama maeneo ya Afrika na Asia. Dengue kitaalamu pia hufahamika kama hdengue emorrhagic fever. Homa hii huweza kusababisha kushuka kwa presha ya damu, homa kali sana kutokwa na damu na hata kufariki.
Ugonjwa wa dengue huweza kuathiri mamilioni ya watu dunia nzima bado wataalamu wapo katika kutafuta chanjo ya ugonjwa huu. Kama ilivyo magonjwa mengine ya virusi dengue pia haina dawa maalumu, lakini mgonjwa atatibiwa kulingana na dalili anazoonyesha na hatimaye atapona. Wagonjwa wengi hupata nafuu dani ya wiki moja.
DALILI ZA UGONJWA WA HOMA YA DENGUE
1.homa kali sana inayofika nyizi 41 za sentigredi
2.Maumivu ya kicha
3.Maumivu ya misuli, viungio na mifupa
4.Maumivu nyuma ya macho
Pia unaweza ukaona dalili nyingine kama:-
1.kuenea kwa ukurutu mwilini
2.Kuchefuchefu na kutapika
3.Kutokwa na damu kwenye finzi na pua
ATHARI ZA KUCHELEWA KUTIBUWA KWA HOMA YA DENGUE
1.kutoka damu kwa wingi kwenye pua na mdomo
2.Maumivu makali sana ya tumbo
3.Kutapika kusikokoma
4.Kutokwa na damu chini ya ngozi
5.Matatizo kwenye ini, mapafu na moyo
6.Kifo
SABABU ZA HOMA YA DENGUE
Kama tulivyoona hapo juu kuwa homa ya dengue husababishwa na virusi ambao wanasambazwa na mbu. Pindi mbu kwenye virusi hawa akimng’ata mtu kumuachia virusi vya dengue.
NJIA ZA KUPAMBA NA NA HOMA YA DENGUE
Mpaka sasa hakuna chanjo ya homa ya dengue. Hivyo njia madhubuti na ya kipekee ni kujiepusha na kungwata na mbu aina ya Aedes aegypti. Kwa kutokomeza mazalia yote ya mbu karibu na maeneo unayoishi. Mbu hawa wanang’ata wakati wa mchana tofauti na mbu wanaoleta malaria ambao hung’ata wakati wa usiku.
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inaonyesha dalili na Mambo Hatari yanayosababisha homa ya ini Kali ya pombe.
Soma Zaidi...Manung'uniko ya moyo ni sauti wakati wa mzunguko wa mapigo ya moyo wako kama vile kutetemeka inayotolewa na damu yenye msukosuko ndani au karibu na moyo wako.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za kufanya figo kuharibika.hili ni janga ambalo linawakumba Watu wengi siku hizi na kusababisha kupoteza maisha kwa wagonjwa wa figo hasa hasa kwa wale ambao hawana uwezo wa kulipia hela ya kusafishia figo.
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za maumivu ya jino
Soma Zaidi...hapa utajifunza maradhi mbalimbali yanatopelekea kuwepo kwa maumivu ya tumbo
Soma Zaidi...Hepatitis B Ni maambukizi ya ini ambayo yamekuwa sugu kuanzia mwezi na kuendelea.
Soma Zaidi...Kaswende ni maambukizi ya bakteria kawaida huenezwa kwa kujamiiana pia ugonjwa huu hujulikana kama syphilis. Ugonjwa huu huanza kama kidonda kisicho na maumivu kwa kawaida kwenye sehemu zako za siri, rektamu au mdomo
Soma Zaidi...