Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za ukimwi za kwenye ulimi na mdomo
DALILI ZA UKIMWI NA HIV KWENYE ULIMU NA MDOMO
HIV hivi ni virusi vilivyopata umaarufu sana kwa kufahamika kuwa ndio virusi pekee vinavyoweza kusababisha upungufu wa kinga mwilini yaani UKIMWI. Virusi hivi anaweza kuvipata binadamu yeyote yule. Zipo njia nyingi ambazo unaweza kupata virusi hivi kama kushiriki ngono zembe, kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kijifungua, kushiriki vitu vyenye ncha kali, kupewa damu yenye virusi, na njia nyingine kibao. Dalili za HIV na UKIMWI zinatofautiana kulingana na hatua ya mgonjwa. Lanini kuna wakati Ulimi na Mdomo kuweza kuonyesha dalili hizi wazi wazi.
Dalili za HIV na UKIMWI kupitia mdomoni zinaweza kuwa ni dalili za mwanzoni sana za UKIMWI kwa baadhi ya watu. Ukweli ni kuwa dalili hizi zinaweza kumpata yeyote lakini kuna watu wapo hatarini zaidi kama watoto wachanga, wazee na watu wenye upungufu wa kinga yaani UKIMWI. Dalili hizi tutaziona moja hadi nyingine hapo chini.
Dalili za HIV na UKIMWI kwenye mdomo na ulimi1.Kukauka kwa mdomo na kuoza kwa meno.Virusi vya HIV vinaweza kupelekea mdomo kukauka na kukosa mate ya kutosha. Hivyo miongoni mwa kazi za mate ni kulinda meno na mdomo. Hivyo kupelekea meno kuoza. Ni vyema mgonjwa kama anatatizo hili kuonana na daktari aweze kumpa ushauri. Unaweza kutumia dawa maalumu kwa ajili ya kuchochea mate ama kutafuna bigji ambazo hazina sukari.
2.Kupata fangasi wa kwenye mdomo wajulikanao kama candidiasis (thrush).Fangasi hawa wanaweza kusababisha madoa mekundu kwenye ulimi, ama mdoa meupe kwenye mdomo. Pia wanaweza kusababisha kupasuka kwa kona za mdomo na kutengeneza weupe kwenye kona za mdomo. Pia mdomoni kunaweza kuta buda la nyama lisilokuwa na maumivu. Fangasi hawa wanaweza kuhamia kwenye koo na kusababisha maumivu. Fangasi hawa ni rahisi sana kuondoka baada ya matibabu ila kwa baadhi ya sababu wanaweza kuwa sugu.
3.Vidonda kwenye mdomo na ulimiHivi ni vijidonda vijidogo ambavyo vipo duara. Vinaweza kutokea kwenye ulimi na kwenye mashavu kwa ndani. Pia vinaweza kutokea nyuma ya koo. Vidonda hivi vinakuwa na rangi nyekunu pembeni na rangi ya kijivu katikati. Misongo ya mawzo na baadhi ya vyakula vinaweza kuwa ni sababu.
4.Vidonda vya homa.Kama umeshawahi kushuhudia vidonda ambavyo vinatokana na homa. Vidonda hivi kwa watu wenye UKIMWI vina tabia ya kujirudia mara kwa mara. Dawa za ART huweza kusaidia hali hii kutotokea.
5.Maradhi ya ufinzi ama periodontitis or gingivitisHaya ni maradhi ya ufizi ambapo ufinzi unakosa nguvu na kushindwa kuzuia meno vyema. Hal hii inaweza kupelekea kung’oka kwa meno. Hali hii inaweza tokea mapema sana miezi 18 baada ya kupata HIV. Ukavu kwenye mdomo, kuvuta sigara kunaweza kufanya hali kuwa mbaya zaidi.
6.Kuota kwa kambakamba ama vinywele vinywele kwenye ulimi na pembeni ya ulimi.Kitaalamu hivi hujulikana kama Hairy Leukoplakia. Vikambakamba ama vinyweleo nyweleo hivi havina maumivu lakini pia haviwezi kutoka hata kwa kupiga mswaki. Hii inaweza kuwa ni katika dalili za mwanzo zaidi za UKIMWI. Vyenyewe vipo na rangi nyeupe
7.Madoa ya rangi ya dhambarau iliyowiva ama nyekundu kwenye mafinzi, sehemu ya juu ya mdomo na nyuma ya ulimi. Kitaalamu hufahamika kama Kaposi’s Sarcoma (KS Hii inaweza kuwa ni dalili ya kwanza kwa mtu ambaye hajapima HIV. Na kwa ambaye ameshaanza kutumia dawa dalili hizi ni si rahisi kujionyesha.
8.Kuota chunjua kwenye mdomo,na ulimi. Hizi husababishwa na virusi vinavyojulikana kama Human Papillomavirus, HPV. Kikawaida chunjua inaweza kuota popote pale kwenye mwili hasa hasa hutokea mara nyingi kwenye mikono. Watu wenye HIV chunjia hizi huweza kuvamia ulimi na kuhama maeneo mengine kwenye mdomo. Pia baadhi ya virusi wanao;eta hali hii wanaweza kusababisha saratani.
Mwisho nikufahamishe tu kuwa mdomo ni katika sehemu za kwanza kuonyesha dalili za HIV na UKIMWI. Ni vyema kwenda kupima endapo utagundua una moja ya dalili hizo hapo juu
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi njia au mbinu mbalimbali ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kuepukana na tatizo la ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dalili za mtu Mwenye tatizo la mkojo kushindwa kutoka kwenye kibofu Cha mkojo.ni dalili ambazo ujitokeza kwa mtu Mwenye tatizo la mkojo kushindwa kutoka kwenye kibofu Cha mkojo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa usafi katika maisha ya mwanadamu au mwili wa binadamu.
Soma Zaidi...Katika somo hili na yanayofuata utajifunz akuhusu ini. Post hii ina muendelezo wa post zinazofuat. Katika mfululizo huuutajifunz akuhusu ini na maradhi yake na kujiking nayo.
Soma Zaidi...post Ina onyesha madhara na matatizo ya Unene Utoto ni hali mbaya ya kiafya inayoathiri watoto na vijana. Inatokea wakati mtoto yuko juu ya uzito wa kawaida kwa umri na urefu wake
Soma Zaidi...Post hii inahusu Zaidi njia mbali mbali ambazo uweza kitumiwa na wataalamu ili kuweza kugundua tatizo la kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu.
Soma Zaidi...posti hii inazungumzia kuhusiana na Maambukizi kwenye mfumo wa mkojo ambapo kitaalamu hujulikana Kama UTI(Urinary Tract Infection (UTI)) hufafanuliwa kuwa ni maambukizo ya mfumo wa uzazi ambayo yanahusisha urethra.ΓΒ UTI ni maambukizi ya mfumo wa mkojo, m
Soma Zaidi...Post ya leo inaenda kufundisha dalili na hatari za presha ya kupanda. Presha ni ugonjwa unaosababishwa na baadhi ya vitu mbalimbali.pressure hujulikana kwa jina lingine ambolo ni hypertension (pressure ya kupanda). presha hugundulika pale ambapo presha ya
Soma Zaidi...