Tufanyeje ili kuepuka kuaribika kwa figo?
Posti hii inahusu zaidi njia za kuzuia kuaribika kwa figo, hizi ni njia zinazotumika ili kuweza kupunguza tatizo la kuaribika kwa figo na hasa wale ambao hawajapata tatizo hili wazitumie ili tuone kama tutaweza kupunguza tatizo hili.
Fanya hivi ili kuilinda figo yako:
1. kula vyakula vyenye kuupa mwili wako afya. Vyakula hivi ni kama samaki, matunda, mbogmboga na kuepuka vyakula visivyo boresha afya kama vyenye mafuta mengi, chumvi nyingi ama vyenye sukari nyingi.
2. fanya mazoezi kwa mara kwa mara. Kufanya mazoezi sio tu kuwa kunaboresha afya ya figo bali kunaboresha afya ya viungo vingine kama moyo, misuli na mifumo mingine ya mwili. Pia mazoezi hufanya mwili kuwa imara.
3. hakikisha una uzito wa kawaida. Uzito kuzidi tofauti na kawaida kunaweza kusababisha shida nyingi za kiafya kama hatari ya kuweza kupata kisukari, pia huhatarisha afya ya moyo na figo. hakikisha uzito wako unaendana na urefu wako. Ongea na daktari kujuwa kama uzito wako umeendana na urefu wako.
4. Pata usingizi wa kutosha. Mwili unahitaji usingizi kwa ajili ya mambo mengi, usingizi husaidia mwili kutibu majeraha kwa ufanisi, kuboresha mfumo wa kinga na kufanya mwili ku starehe (relax). Mtu akikosa ukisngizi anaweza kuwa katika hatari ya kupata maradhi mbalimbali ikiwepo maradhi ya figo.
Njia nyingine za kulinda figo:
1. Wacha kuvuta sigara
2. Punguza kunywa pombe
3. Punguza misongo ya mawazo
4. Hakiisha sukari ya mwili ipo katika hali ya kawaida.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Kitau cha Fiqh π2 web hosting π3 Dua za Mitume na Manabii π4 ai web app π5 Kitabu cha Afya π6 Madrasa kiganjani
Post zinazofanana:
Sababu ya maumivu ya magoti.
Posti hii inahusu zaidi sababu za maumivu ambayo yanasikika kwenye magoti, huu ni ugonjwa ambao umewapata walio wengi na bado ni kilio kwa walio wengi kwa vijana na kwa wazee, Kuna wataalamu mbalimbali ambao wameweza kugundua sababu za maumivu kwenye mago
Soma Zaidi...ATHARI ZA KUTOKUTIBU MINYOO: maumivu ya tumbo, kichwa, kutapika damu, kichefuchefu, miwasho
ATHARI ZA KUTOKUTIBU MINYOO Kukaa na minyoo na kutoitibu kwa muda mrefu kunaweza kusababisha madhara mengi hususani kwenye ini na maeneo mengine ya mfumo wa kumengβenya chakula.
Soma Zaidi...Kumsaidia sliyepungukiwa na damu kwa sababu ya minyoo
Posti hii inahusu namna ya kumsaidia mgonjwa aliyepungukiwa na damu kwa sababu ya minyoo.
Soma Zaidi...Sababu za ugonjwa wa pumu, dalili zake na jinsi ya kujilinda na pumu.
Ugonjwa wa pumu ni ugonjwa unaoshambulia mfumo wa hewa ambapo mgonjwa hushindwa kupumua vizuri na hupelekea matatizo ya kudumu kama haujatibiwa mapema.
Soma Zaidi...Dalili za minyoo ya tumbo
Posti hii inaelezea kuhusiana na dalili za minyoo ya tumbo ambapo minyoo hawa husababishwa na mtu kula vyakula vichafu ambavyo havijaiva vizuri au maji machafu pia au bacteria.
Soma Zaidi...Ni nini husababisha mate kujaa mdomoni, na ni yapi matibabu yake
Hapa tutaangalia baadhi ya sababu zinazopelekea mdomo kujaa mate na namna ya kutibu tatizo la kujaa kwa mate mdomoni
Soma Zaidi...