Huu ni mwendelezo wa mafunzo ya database na jinsi ya kutengeneza bloga na website na hili ni somo la tatu. hapa utajifunza jinsiya kutengeneza database yako kwa mara ya kwanza.
Matumizi ya MySQL katika database.
Naamini umeshajifunzakuwa MySQL ni software ambayo hutumika katika kudhibiti database yako. Pia ulishaweza kuandaa kifaa chako katika somo la kwanza. Katika somo hili nitakwenda kukujuza sehemu muhimu za MySQL na namna ya kutengeneza database yako.
Kama ulishawahi kutumia database ya microsoft office inayojulukana kama microsoft access, basi itakuwa rahisi kwako kutambuwa nini kinachotokea. Kama ndio mara yako ya kwanza kutengeneza database somo hili ni kwa ajili yako.
Je unajuwa kuwa:
Chati zetu zote za facebook, wasap na instagram zimehifadhiwa kwenye database? Itambulie kuwa karibia mbog zote hutumia database. Hivyo somo hili ni moja katikamasomomuhmu sana ya wewe kujuwa nini kinachoendelea katika mitandao, na vipi taarifa zako zinahifadhiwa.
FUNGUWA MySQL
Pitia tena somo la kwanza namna ya kufunguwa MySQL kwenye simu ama kompyuta kisha uendelee na somo hili.kama umeshafika ile hatuwa ya kuona neno database basi tutaanzia hapo.
JINSI YA KUTENGENEZA DATABASE:
Kama umeshaifunguwa MySQL utaona kuna menu hapo juu. Hiyo menu utaona ina items hizi
Hizo ndio sehemu kuu za MySQL ambazo zitakwenda kutumika. Katika somo hili la leo tutajifunza menu ya kwanza na ya pili tu tu ambazo ni Databases na SQL. Hii ndio sehemu ambayo utaanza kutengeneza database kabla ya kujifunza kutumia SQL.
Create database
Tuanze somo letu sasa na kutengeneza DATABASE. Kama ulivyoifunza ni kuwa database ni mkusanyiko wa taarifa zilizopangiliwa na zinafikiwa kwa njia za ki electronic. Sasa kwa mfano una blog yako na unataka kutengeneza database kwa ajili ya blog. Kita cha kwanza mi kutafuta jina la hiyo database yako. Utaiita vipi?
Tuchukulie mfano jina la database yetu ni mafunzo. Sasa hatuwa inayofata ni kutengeneza database inayoitwa mafunzo. Katika menu yako bofya neno database. Utaona kuna sehemu kumeandikwa create database. Kisha chini kuna kabox ndani kana neno database name. Hapo ndani weka jina la database yako, mfano utaweka mafunzo. Kisha bofya neno create.
Baada ya hapo utaona kwenye orodha ya database kuna database inayoitwa mafunzo. Katika ukurasa huo pia kwa juu utaona kuna neno structure, pia kuna neno lingine limeandikwa no table found. Chini yake kuna neno limeandikwa CREATE TABLE IF NOT EXISTS. Hizi zote tutakuja ziona somo lijalo.
Mpaka kufikia hapo umeweza kutengeneza database yako kwa kutumia menu ya database. Sasa hatuwa inayofata ni kufuta database. Ila kabla ya kufuta database tunakwenda kutengeneza database nyingine kwa kutumia menu ya SQL.
Ili kfanya hivi tunatakiwa tujuwe kwanza kuwa SQL ni menu ambayo itakuletea uwanja wa kuingiza code za SQL language. Kwa kutumia sql unaweza kutengeneza database kwa kuandika create database kisha unaweka jina la database yako kwa mfano post kisha utamalza na alama hii ; hivyo itakuwa hivi create database post;. Ukiweka maneno haya maana yake unaiambia MySQL kuwa itengeneze database ambayo inaitwa post.
Ok hebu tuanze sasa.
Mpaka kufikia hapa tutakuwa na database mbili katika listi yetu. Katika somo la tatu nne tutakwenda kujifunza namna ya kufuta, na kubadili jina database yetu.
Mafunzo haya yamekujia kwa ihsai ya
Bongoclass.com
Web:bongoclass.com
Email: mafunzo@bongoclass.com
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Karibu tena katika mafunzo yetu, na huu ni mwanzo wa mafunzoya DATABASE kwa kutumia MYSQL kwa lugha ya kiswahili. Na hili ni somo la kwanza, katka somo hili utajifunza jinsi ya kuandaa kifaa chako kwa ajili ya mafunzo.
Soma Zaidi...Katika somo hili la php level 1 somo la 6 utajifunza namna ya kutumia tarehe yaani function date() kwenye PHP
Soma Zaidi...Haya ni mafunzo ya muda mfupi katika kujifunza hasa ujuzi wa kutengeneza Android App hata kama haujui kitu kuhusiana na Android Development
Soma Zaidi...somo hili la 4 katika mafunzo ya PHP level 1 utajifunza aina za data mabazo php inakwenda kuzitumia.
Soma Zaidi...katika somo hili la tano kwenye mafunzo ya HTML level 1 utajifunza jinsi ya 1.Kuweka picha 2.Kuweka rangi 3.Kuweka linki 4.Kupangilia position na alignment ya maandishi 5.Kuongeza ukubwa wa herufi 6.Kukoment
Soma Zaidi...Huu ni muendelezo wa mafunzo ya Database kwa kutumia MySQL na hili ni somo la 10. katika somo hili tutakwenda kuendelea namna ya kupangilia muonekano wa data zako kwenye database.
Soma Zaidi...Huu ni muendelezo wa mafunzo ya DATABASE kwa kutumia software ya MySQL na hili ni somo la tano. katika somo hili utajifunza type of data yaani aina ya taarifa ambazo unaweza kuzihifadhi kwenye database yako.
Soma Zaidi...huu ni muendelezo wa mafunzo ya Database klwa kutumia MySQL na hili ni somo la 11. katika somo hili tutaendelea kujifunza mpangilio wa muonekano wa data kwenye database.
Soma Zaidi...Karibu kwenye mafunzo ya PHP level 1 na hili ni somo la kwanza. Hapa utajifunza maana ya php, inavyofanya kazi pamoja na historia yake kwa ufupi
Soma Zaidi...Huu ni mwendelezo wa mafunzo ya DATABASE kwa kutumia MySQL na hili ni somo la pili. Hapa tutakwenda kuona kwa ufupi ni nini DATABASE
Soma Zaidi...