somo hili la 4 katika mafunzo ya PHP level 1 utajifunza aina za data mabazo php inakwenda kuzitumia.
SOMO LA NNE
TYPE OF DATA IN PHP:
Kabla ya kuendelea mbele zaidi katika somo la PHP sasa kwanza lazima tujuwe aina za data ambazo tunakwenda kuzitumia kwenye php. Kila taarifa tunayotaka kuitumia aka kuionyesha lazima tujuwe ipo katika aina ipi ya data. Hii itakusaidia wewe katika kupanga actions. Pia katika kuweka fomu za madodoso.
Kwa ufupi katika php kuna aina kuu 7 za data ambazo tutakwenda kuziangalia.
1. STRING
String ni mkusanyiko wa herufi ama character. Mfano “hello” “I am a student”. Katika PHP string huwekwa ndani ya alama za semi yaani alama za kunukuu ambazo ni “ “. hata hivyo pia unaweza kuchaguwa eidha utumie alama ya kunukuu moja ama mbili mfano ‘ ’ au “ “. mfano wa string kwa alama moja ‘hello’ mfano wa string kwa alama mbili “hello”. pia string inaweza kuwa na mchanganyiko wa herufi, namba na character nyingine. Angalia mifano hapo chini.
2. INTEGER
Aina hii ya data ni zile data zote ambazo ni namba tu. Pia zinatakiwa ziwe namba ambazo hazina desimali. Pia integer zinaweza kuwa nmaba ambazo ni positive ama negative. Kitu cha kuzingatia hapa ni kuwa integer haitakiwi iwe na desimali. Mfano 6353
3. FLOAT
Hizi ni data ambazo ni namba zilizo na desimali ama exponent. Mgano 23.9
4. BOOLEAN
Hizi ni data ambazo hutumika katika kujaribu hali. Hizi zinaitwa condition test. Bolean zipo katika namna mbili ambazo ni TRUE au FALSE.
5. ARRAY
Hizi ni data ambazo zinahifadhi taarifa zaidia ya moja kwenye variable. Kwa mfano inaweza kuzungumzia variable miti kisha ikaendelea kutaja aina za mita ambayo itahusika kwenye variable hiyo moja.
6. OBJECT
Object ni aina ya data ambayo inahifadhi taarifa na namna ambavyo taarifa hiyo itachakatwa. Tutajifunza zaidi kwenye masomo yajayo.
7. NULL
Katika php data ambayo ni null ni data maalumu ambayo inakuwa na thamani moja tu a,bayo ni NULL. Na variable yake inakuwa tu. N endapo umeweka variable na hukuweka kuwa itafanya nini amba itatoa thamani ya kitu gani, basi automatic variable hii hubadilishwa kuwa NULL.
JINSI YA KUJUWA AINA YA DATA KATIKA PHP:
Ili uweze kujuwa aina ya data iliyotumika huwa tunatumia var_dump(). hii ni function ambayo hutumika katika kuonyesha aina ya data iliyotumika kwenye php. Angalia mifano hapo chini:-
Mfano 1:
<?php
$a = 7635262;
Var_dump ($a);
?>
Hapa utapata matokeo haya int(7635262) hii inamaana kuwa namba hizo ni integer ambayo ndio aina ya data iliyotumika
Mfano 2:
<?php
$a = "hello piga *112#";
Var_dump ($a);
?>
Hapa iakuletea: string(16) "hello piga *112#" hii inamaana kuwa data nilizotumia kwenye mfano huu ni string, ambazo ni mkusanyiko wa herufi, namba na alama kama * na #. hiyo 16 hapo ina maanisha kuwa string iliyotumika ina character 16.
Mfano 3:
<?php
$a = 626.9;
Var_dump ($a);
?>
Hii itakuletea matokeo: float(626.9) inamaana kuwa aina ya data iliyotumika ni float ambayo ni namba zenye desimali na exponent.
Mfano 4:
<?php
$mti = array("mpera", "muembe", "mchungwa", "mlimao");
Var_dump($mti);
?>
Hii itakupa matokeo array(4) { [0]=> string(5) "mpera" [1]=> string(6) "muembe" [2]=> string(8) "mchungwa" [3]=> string(6) "mlimao" } hii inamaana kuwa data iliyotumika ni array ambayo ndani yake kuna string 5.
Mfano 5:
<?php
$a = '';
$a = null;
Var_dump($a);
?>
Hii itakupa matokeo kuwa NULL
Tutajifunza zaidi katika viindi vijavyo, tutajifunza zaidi juu ya hizi aina za data. Tutaangalia namna ya kutumia string katika uandishi.
Mafunzo haya yanakujia kwa ihsani ya bongoclass
Web: www.bongoclass.com
Email:mafunzo@bongoclass.com
Phone: 0774069753 unaweza kunicheki wasap kwa link hii https://wa.me/message/7CTQP5BSWBR5I1
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
hili ni somo la pili katika mfululizo wa mafunzo haya ya php level 1 na hapa utajifunza namna ya kuandika faili klako la kwanza la php.
Soma Zaidi...Hii ni project ya HTML ambayo imetengenezwa kulingana na mafunzo ya HTML level1. Tunatarajia project hii kuboreshwa kadiri mafunzo yanavyozidi kusonga mbele.
Soma Zaidi...Huu ni muendelezowa mafunzo ya database kwa kutumia MySQl na hili ni somo la 12. katika somo hili tutajifunza namna ya kufanya mahesabu kwa kutumia SQl katika database
Soma Zaidi...Karibu tena katika mafunzo yetu, na huu ni mwanzo wa mafunzoya DATABASE kwa kutumia MYSQL kwa lugha ya kiswahili. Na hili ni somo la kwanza, katka somo hili utajifunza jinsi ya kuandaa kifaa chako kwa ajili ya mafunzo.
Soma Zaidi...hili ni somo la pili katika mafunzo ya HTML level 2 html full course for beginners. Katika somo hili tutaangalia utangulizi juu ya HTML na pia utajifunza faida za HTML.
Soma Zaidi...hili ni somo la tatu katika masomo ya php level 1. Hapa utajifunza zaidi kuhusu variable na namna ya kuitengeneza.
Soma Zaidi...Somo la 10 mafunzo ya php level 1. Katika somo hili utajifunza kuhusu condition statement.
Soma Zaidi...Hili ni somo la pili katika mfululizo wa mafunzo ya html level ya 1 na hapa tutakwenda sasa kunanza somo letu rasmi, kwani katika somo la kwanza umejifunza jinsi ya kuandaa kifaa chako kwa ajili ya mafunzo.
Soma Zaidi...Mafunzo ya php level 1 somo ka 12 mwisho wa mafunzo. Hapa utaona project ambazo unaweza kufanya kutokana na mafunzo haya.
Soma Zaidi...Hili n somo la tatu katka muendelezo wa mafunzo ya HTML LEVEL 2 kwa lugha ya kiswahili. Mafunzo haya yanakujia kwa Ihsani ya bongoclass
Soma Zaidi...