Hili ni somo la saba, mafunzo ya php level 1. Katika somo hili utajifunza jinsi ya kuandika function yako mwenyewe.
SOMO LA 7
USER DEFINE PHP FUNCTIONS
Katika somo lililotangulia tumejifunza namna ambavyo unaweza kuweka functions kwenye php. Sasa hapa tutaona kuweka function yako mwenyewe kulingana na matarajio yako.
Kanuni
1.Andika neno function mfano function
2.Kisha weka jina la function yako mano function salama
3.Kisha weka mabano () mfano function salamu() mapano haya huitwa curly barce
4.Weka mabano haya {} mfano function salama() {}. Mabano haya huitwa parentheses
5.Ndani ya mabano haya ya pili utaweka code angalia mifano hapo chini
6.Mwisho call function, yaani hapa ndipo utatumia function yako kuleta matokeo. Bila ya call hutaweka kupata matokeo. Kwa mfano salamu(); utaicall kwa kuitaja jina lake kama lilivyo mwanzoni mwa function ilipoanza.
Mfano 1
<?php
function salamu (){
echo "Habari Hujambo!!!";
}
salamu();
?>
Hii itakupa matokeo: Habari Hujambo!!!
KUWEKA VARIABLE NDANI YA FUNCTION
Katika function unaweza kuongeza taarifa zaidi, kwa kutumia argument, hizi ni sawa na varable. Na hizi huwekwa kwenye yale mabado ya parenthes (). kwa mfano unataka kuorothesha majina ya watoto ambao mama yao ni mmoja. Badala ya kuandika kila mtoto jina lake na la baba yake. Basi tutatumia function kuandika jina la baba kwa wote mara moja tu. Angalia mfan hapo chini:-
Mfano 2:
<?php
function b ($mtoto){
echo "$mtoto Saidi. <br>";
}
b ("Shukuru");
b ("Sikuzani");
b ("Neema");
b ("Pendo");
b ("Tabu");
b ("Subira");
?>
Hii itakupa matokeo
Shukuru Saidi.
Sikuzani Saidi.
Neema Saidi.
Pendo Saidi.
Tabu Saidi.
Subira Saidi.
Pia unaweza kutumia variable au argument zaidi ya moja. Kwa mfano unataka kujumlisha namba zaidi ya moja. Kumbuka kutenganisha kwa koma variable moja na nyingine. Unaweza kutumia variable 2 ndani ya mabano ya function. Angalia mfano hapo chini:-
Mfano 3:
<?php
function jumlisha($x, $z){
$jumla = $x + $z;
echo "jumla ni:- $jumla";
}
jumlisha(6, 7);
?>
Hii itakupa matokeo
Jumla ni:- 13
Pia tunaweza kupata matokeo ya function kwa kutumia ststement ya return value. Hata hivyo pia unaweza kutumia hii kwa zaidi ya variable mbili na kuendelea. Angalia mfano hapo chini:-
Mfano 4
<?php
function zidisha($a, $b, $c){
$jibu = $a * $b * $c;
return $jibu;
}
$return_value = zidisha(2, 3, 4);
echo "majibu ni:- $return_value";
Hii itakupamatokeo: majibu ni:- 24
Pia kwa kutumia function moja unaweza kupata matokeo mengi zaidi. Na hii ndio umuhimu wa kutumia function huna haja ya kukiandika kitu kimoja kila wakati. Angalia mfano hapo chini
Mfano 5
<?php
function jumlisha($a, $b){
$c = $a + $b;
return $c;
}
echo jumlisha(5, 2) . "<br>" ;
echo jumlisha(3, 9) . "<br>";
echo jumlisha(100, 101). "<br>";
echo jumlisha(9, 0.4). "<br>";
?>
Hii itakupa matokeo
7
12
201
9.4
Mafunzo haya yanakujia kwa ihsani ya bongoclass
Web: www.bongoclass.com
Email:mafunzo@bongoclass.com
Phone: 0774069753 unaweza kunicheki wasap kwa link hii https://wa.me/message/7CTQP5BSWBR5I1
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
katika somo hili la tano kwenye mafunzo ya HTML level 1 utajifunza jinsi ya 1.Kuweka picha 2.Kuweka rangi 3.Kuweka linki 4.Kupangilia position na alignment ya maandishi 5.Kuongeza ukubwa wa herufi 6.Kukoment
Soma Zaidi...Huu ni muendelezowa mafunzo ya database kwa kutumia MySQl na hili ni somo la 12. katika somo hili tutajifunza namna ya kufanya mahesabu kwa kutumia SQl katika database
Soma Zaidi...Karibu tena katika mafunzo haya ya html level 2 na hili ni somo la 5. Katika somo hili utajifunza zaidi kuhusu kuweka style kwenye html file.
Soma Zaidi...Huu ni mwendelezo wa mafunzo ya database na jinsi ya kutengeneza bloga na website na hili ni somo la tatu. hapa utajifunza jinsiya kutengeneza database yako kwa mara ya kwanza.
Soma Zaidi...Haya ni mafunzo ya HTML kwa wanaoanza level ya kwanza, na hili ni somo la kwanza katika masomo 8 yatakayokujia katika mtiririko wa course hii.
Soma Zaidi...Hili ni somo la mwisho mafunzo ya HTML level 2 (html full course for beginners)
Soma Zaidi...Karibu tena katika somo la nne la mafunzo ya HTML level2 html full course for beginners. Katika somo hili utajifunza kuhusu attributes na namna zinavyofanya kazi
Soma Zaidi...Mafunzo ya database kwa utumia software ya MySQL kwa lugha ya kiswahili na hili ni somo la 7.
Soma Zaidi...Katika somo hili la php level 1 somo la 6 utajifunza namna ya kutumia tarehe yaani function date() kwenye PHP
Soma Zaidi...haya ni mafunzo ya database kwa kutumia MySQl na hili ni somo la 9. katika soo hili utajifunza namna ya kusoma ama kutumia taarifa zilizomo kwenye DATABASE.
Soma Zaidi...