Mafunzo ya DATABASE MYSQL na SQL somo la 1
Karibu tena katika mafunzo yetu, na huu ni mwanzo wa mafunzoya DATABASE kwa kutumia MYSQL kwa lugha ya kiswahili. Na hili ni somo la kwanza, katka somo hili utajifunza jinsi ya kuandaa kifaa chako kwa ajili ya mafunzo.
MAFUNZO YA DATABASE SQL (MYSQL)
haya ni mafunzo ya DATABASE kwa kutumia software ya MYSQL. Katika mafunzo haya utajifunza namna ya kuthibiti taarifa kwnye database kwa kutumia software ya mysql. Pamoja na mafunzo ya php na html utaweza pia kuzitumia taarifa hizi moja kwa oja kwenye blog ama website yako.
Mafunzo haya yatakujia kupitia mfundishaji wako Mr. Rajabu kutoka bongoclass. Mwisho wa mafunzo haya utaweza kumilii database yeko ya online ambapo utaweza kuweka na kupata taarifa popote ulipo kutoka kwenye kifaa chochote kile. Kumbukacourse hii inakuji free kabisa bila ya malipo. Unachotakiwa ni kushiriki vyema tu.
VIGEZO VYA KUSHIRIKI MAFUNZO:
- Uwe na simu janja yenye kiendeshi cha Android au uwe na kompyuta
- Uwe mjanja
- Una uzoefu wa kutumia software ama android App mbalimbali kama excel,
- Uweze kusoma na kuandika angalau maneno marahisi ya kiiingereza kama create, drop, user, select, where, into, update, order na mengine yanayofanana na haya.
MAANDALIZI YA SOMO:
Ili kuweza kuendelea na somo hili hakikisha kuwa umesakinisha App zifutazo kwenye kifaa chako.
- Kama unatumia simu AWEBSERVER tumia link hii https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sylkat.apache
- Kama unatumia kompyuta download wampserver ama xamp vyema ukaanza na xamp maana wampserver wakati mwingine inasumbuwa kwenye kuinstall kama kompyta haipo update.
Baada ya kufukia hapo utakuwa umeshamaliza maandalizi ya somo.
JINSI YA KUANZA:
KAMA UNATUMIA SIMU:
- Funguwa App yako
- Bofya start kuanza huduma ya server iwe active
- Kwenye menu upande wa juu kuna kapicha kama suka sufuria kameandika Mysql bofya hapao.
- Bofya start ili kuanza huduma
- Utaona kulia mwa neno admin kuna link yenye sura hii 0.0.0.0:8080/mysqladmin
- Bofya kwenye link hiyo
- Utyaona kuna ukurasa ukekuja unakuhitaji kuweka user name na password
- Username weka root na password weka root
- Kisha bofya log in
- Utafunguka ukurasa mpya ambao utaona neno database kwa juu.
Kama umefika hatuwa hii HONGERA somo letu la kwanza litaanzia hapo
KAMA UNATUMIA KOMPYUTA:
Kama unatumia xamp
- Funguwa software ya xamp
- Kutafunguka kiukurasa kadogo kenye menu.
- Kwenye apache bofya start
- Kwenye Mysql bofya start
- Kisha kwenye Mysql bofya Admin
- Utaona kuna ukurasa mkubwa umefunguka kwenye browser yako.
- Neno databases utaliona kwa juu
- Hapa utakuwa upo tayari kwa somo lijalo.
KAMA UNATUMIA WAMPSERVER
- Ifunguwe hiyo software
- Nenda kwenye tray upande wa kulia utaikuta ipo active
- Right click
- Kwenye menu bofya phpmyadmin
- Ukurasa mpya utafunguka na neno database litaonekana kwa juu.
- Kama umefuka hatuwa hii upo tayari kwa somo linalofata.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Madrasa kiganjani 👉2 web hosting 👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉5 Kitau cha Fiqh 👉6 Kitabu cha Afya
Post zinazofanana:
PHP level 1 somo la tisa (9).
Somo la nane mafunzo ya php, katika somo hili utajifunza kuhusu array na jinsi ya kutengeneza array.
Soma Zaidi...Utangulizi wa Android App Development
Haya ni mafunzo ya muda mfupi katika kujifunza hasa ujuzi wa kutengeneza Android App hata kama haujui kitu kuhusiana na Android Development
Soma Zaidi...PHP level 11 somo la kumi na moja (11)
Katika somo hilivutajifunza namna ya kutumia HTML form. Namna ya kuookea taarifa kutoka kwenye madodoso ya html form.
Soma Zaidi...Mafunzo ya Database MySQL database somo la 10
Huu ni muendelezo wa mafunzo ya Database kwa kutumia MySQL na hili ni somo la 10. katika somo hili tutakwenda kuendelea namna ya kupangilia muonekano wa data zako kwenye database.
Soma Zaidi...Mafunzo ya HTML level 1 somo la 1 (HTML basic level FOR BEGINNERS)
Haya ni mafunzo ya HTML kwa wanaoanza level ya kwanza, na hili ni somo la kwanza katika masomo 8 yatakayokujia katika mtiririko wa course hii.
Soma Zaidi...Mafunzo ya HTML level 1 somo la 2 (HTML basic level FOR BEGINNERS)
Hili ni somo la pili katika mfululizo wa mafunzo ya html level ya 1 na hapa tutakwenda sasa kunanza somo letu rasmi, kwani katika somo la kwanza umejifunza jinsi ya kuandaa kifaa chako kwa ajili ya mafunzo.
Soma Zaidi...