Huu ni mwendelezo wa mafunzo ya database kwa kutumia MySQL na hili ni somo la nne katika mlolongo wa masomo haya. Katika somo hili utajifuza jinsi ya kubadili jina la database na kufuta database. Pia tutajifunza kutumia SQL kufanya hayo.
Katika somo hili la nne tutakwenda kujifunza mambo makuu matatu ambayo ni:-
Kama ulishiriki mafunzo katika somo la tatu ulijifunza namna ya kutengeneza database kwa kutumia MySQL na kwa mutumia SAL command. Sasa katika somo hili tutakwenda kutumia database zetu mbili ambazo tulizitengeneza katika somo la tatu.
1. Kuona orodha ya database:
Hili ni jambo rahisi tu, baada ya kuingia kwenye MySQL, angalia menu yako, kisha bofya databases hapo utaona orodha ya database zote ambazo umetengeneza.
Sasa tunataka kufanya kitu kama hicho cha kuona orodha ta database kwa kutumia SQL language. Kufanya hivi fuata hatuwa hiz:-
2. Kutumia database
Baada ya kuona orodha ya database zote hatuwa inayofata ni kuitumia hiyo database ama hizo database. Kutumia database maana yake ni kufanya hicho ambacho ulikusudia kwenye hiyo database kwa mfano kufuta, kubadili jiana ama kuweka data ama kuondoa na kubadili.
Kufanya hivi kwenye MySQL pia ni rahisi sana, unachotakiwa kufanya ni kubofya hiyo database yako. Ukishaubofya utaona umefunguka na kama kuna taarifa utaanza kuona majedwali yaliyopo.
Kufanya hivi kwa kutumia SQL pia ni rahisi, fuata hatuwa zifuatazo:-
3. Kubadili jina la database
Kwa kutumia MySQL baada ya kubofya hiyo database angalia kwenye menu tafuta neno oprrations, bofya hapo. Kisha tafuta palipoandikwa rename database to chini ya maneno hayo utaona kuna kabox. Kwenye hako kabox utaweka jina ambalo unataka kubadili. Kwa mfano database yetu inaitwa post sasa tunataka kuibadili jina kuiita makala.
Hivyo ingiza kwenye hicho kibox jina makala kisha bofya neno GO lipo upande wa kulia.kuna ujumbe utakuja unasema CREATE DATABASE makala / DROP DATABASE post hapo utabofya OK kukubali. Mpaka kufikia hapo utakuwa umemaliza kubadili jina na hapo database yako itakuwa imebadilika.
Kufanya hivi kwa kutumia SQL utatumia RENAME ila kwa sasa hatutajifunza kufanya hivi ni kwa sababu command hii iliondolewa kwenye MySQl kwa sababu za kiusalama. Hivyo utaendelea kutumia MySQL interface kubadili jina.
4. kufuta database
Kufuta database kwenye MySQL utakwenda kwenye operations kama ulivyofanya hapo juu. Kisha tafuta palipoandikwa Remove database chini ya hayo maneno utaona kuna maneno yanasomeka Drop the database (DROP) bofya hayo maneno kisha kuna ujumbe utakuja You are about to DESTROY a complete database! Do you really want to execute "DROP DATABASE `makala`"? hapo bofya OK kukubali. Kufikia hapo utakuwa umeifuta database yako na hutoweza kuirudisha tena lamda iwe umeshaifanyia backup.
Kufanya hivi kwa kutumia SQL fuata taratibu zifuatazo. Kwa kuwa database ya makala tumeifuta basi sasa tunakwenda kufuta ile ya mafunzo.
Kwa ufupi command ambazo zimetumika kwenye somo hili ni
Tukutane somo la tano tutakapojifunza Type of data in MySQL somo hili litakuwa ni muhimu sana na ni msingi hasa wa somo la sita. Pia kwa wale abao wanahitaji kujatumia database zao vilivyo wanatakiwa walifahamu vyema somo la tano.
Mafunzo haya yanakujia kwa ihsani ya
Bongoclass
Web: www.bongoclass.com
Email: mafunzo@bongoclass.com
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Karibu tena katika mafunzo yetu, na huu ni mwanzo wa mafunzoya DATABASE kwa kutumia MYSQL kwa lugha ya kiswahili. Na hili ni somo la kwanza, katka somo hili utajifunza jinsi ya kuandaa kifaa chako kwa ajili ya mafunzo.
Soma Zaidi...Ktika somo hili la 7 utajifunza namna ya kuandaa na kujiandaa kutengeneza website ama blog. Pia utajifunza maandalizi ya kuhost
Soma Zaidi...Huu ni muendelezowa mafunzo ya database kwa kutumia MySQl na hili ni somo la 12. katika somo hili tutajifunza namna ya kufanya mahesabu kwa kutumia SQl katika database
Soma Zaidi...Hili ni somo la nne katika mafunzo ya html basic level. Hapa tutakwenda kuona jinsi ya kuzifanyia kazi tag ambazo umejifunza katika somo lililotangulia.
Soma Zaidi...Katika somo hili la php level 1 somo la 6 utajifunza namna ya kutumia tarehe yaani function date() kwenye PHP
Soma Zaidi...Hili ni somo la saba, mafunzo ya php level 1. Katika somo hili utajifunza jinsi ya kuandika function yako mwenyewe.
Soma Zaidi...Karibu tena katika mafunzo haya ya html level 2 na hili ni somo la 5. Katika somo hili utajifunza zaidi kuhusu kuweka style kwenye html file.
Soma Zaidi...Huuu ni muendeleo wa mafunzo ya database kwa lugha ya kiswahili, na hili ni somo la nane. Katika somo hli utajifunza namna ya kuweka taarifa kwenye database, kuzfuta na kuziediti yaani kuzifanyia marekebisho.
Soma Zaidi...Mafunzo ya database kwa utumia software ya MySQL kwa lugha ya kiswahili na hili ni somo la 7.
Soma Zaidi...Haya ni mafunzo ya php na hili ni somo la tano. Katika somovhili utajifunza namna ya kutengeneza functions.
Soma Zaidi...